JB: Mganda huyu ni nani na anafanya nini Tanzania?

JB being a Ugandan working (Entrepreneurship) in Tanzania is not a problem as long as he fulfills all the legal requirement of his citizenship. Any one with evidance of his ilegal stay and working in Tanzania?
Note: Responsible authorities, please use this as a clue and work on it. Ni hayo tu
 
nderingosha umenena.
 
Last edited by a moderator:
Tutajuaje kama kweli alikosana na Museveni? Maana hata Marehemu Shekhe Yahya alikaa sana Kenya sababu eti "aligombana Nyerere".

Cha ajabu ni Sheikh Yahya huyu huyu aliyefanikisha watu wa usalama wa taifa kumtia mbaroni Mtanzania aliye kimbilia Botswana au Swaziland (sikumbuki vizuri) kwa uhaini, kumbuka hiyo ilikuwa ni enzi za Nyerere. Swali ni je? Ni kweli Nyerere aliwahi kugambana na Sheikh Yaya kweli!
 
Ule msemo wa "uchumi tunao lakini tumeukalia" sasa ndio uko wazi kabisa. Wageni wanapoligundua hilo huja na kuhodhi tulivyonavyo wakituaja kulalamika. Sababu zinazowafanya WaTz kutowekeza Kenya na Uganda zinaweza kuwa ni pamoja na ama matajiri wetu hawana innitiatives au huko sheria za uwekezaji ni makini zaidi.

Hapo nyekundu, tusiwalaumu hawa wanaoingia na kufanya wanayofanya, bali tulaumu mfumo wetu unaowaruhusu kufanya wanayofanya. Nakubaliana na wachingiaji waliosema kuwa WaTz tunachojua ni kulalamika, kutaka kila kitu kwa njia ya mkato na ndio maana tukihongwa kidogo tu tunawachia.
Tunawalaumu wanaume wa kigeni kwa "kutuharibia dada zetu" kama kwamba wanawabaka kumbe wanajipeleka.
Tunawalaumu wageni kutuibia rasilimali zetu, kama kwamba wanatuwekea bastola kisogoni kumbe tunawapa wenyewe.
Tunawalaumu Wakenya na Waganda kwa kuwekeza Tz, kama kwamba sisi tumekatazwa kuwekeza kwao kumbe sisi ni domokaya tu.

Tuna woga wa kujiunga kikamilifu na EAC kwa sababu hatujiamini, hatutaki kujituma, tunaogopa ushindani.
Tunaogopa Wakenya kuja kuchukua ardhi yetu, lakini viongozi wetu wanaitoa ardhi hiyo hiyo kwa Wakenya, Waganda, Wasomali, Wataliana n.k. kwa njia za panya.
 
nderingosha, Paradise Bagamoyo hotel kweli iluungua moto na mmiliki alisema (mbele ya vyombo vya habari) kuwa wataijenga kama ilivyo ndani ya mwaka mmoja. Na kilio chake kikubwa ilikuwa ni kuokoa ajira watanzania. But we know, baada ya moto waliondoka Bagamoyo na kuanza kuwekeza ndani ya jiji kwa kuanzia wakachukua City Garden, then hapo Benjamin Mkapa na pia wana investment Nyerere Rd.

We also know wakati wa moto biashara ya Paradise Hotel Bagamoyo was going down maana seminar nyingi za serikali zilikuwa zinapungua. Watu walishachoka kwenye kwenye same hotel, same smile, same mapokezi ya vingoma! Na service ilikuwa inadorora kila kukicha, including chakula ambacho watu wengi walikuwa wanalalamika.

Kwa sasa wasomali hawa wamejikita kwenye biashara katikati ya jiji na huku ndiko walikokutana na JB.

Maoni yangu. Sina tatizo kabisa uwekezaji wa hawa wasomali au wa bwana JB au mtu mwingine yoyote toka nje ya mipaka ya nchi hii. Na sina shida na wadada wanapata 'pleasure' toka kwa JB, maana kila mtu ana uhuru wa kupata kitu roho inataka. Tatizo langu na kichefuchefu changu ni screening or lack of it kuhusu baadhi ya wawekezaji. Ukiachilia Cuba, Tanzania ina human intelligence nzuri sana, lakini kwa mshangao watu, mbu, vifaru, vumbi vyote vinaingia nchini na bado wakubwa wanasimama mbele za watu na kusema nchi iko salama! Hakuna linalofanyika watu hawajui na ndio sababy hapa watu wanahoji JB, lakini mambo yanawekwa kapuni. Siku yakimwagika wote tutapata hasara.
 
Last edited by a moderator:

Wiki nne zilizopita nilikuwa naongea na mdau mmoja pale kituo cha mafuta karibu na posta tukilitazama jengo la NPF la Benjamin William Mkapa, nikawa nasema pesa hizi za wafanya kazi si sahihi kupwa tu kwa mkupua mafao ya milioni 10-15 badala yake wawe wanalipwa kila mwezi hadi mtu anazeeka.

Mdau aliniambia jengo hilo la Benjamin William Mkapa upande mmoja limepangishwa kwa Mganda, ni hotel. Kwangu sioni tatizo kama waafrika wenzetu wanafanya mambo kama hayo, maana pesa yake ipo kwenye mzunguko hapa hapa easta africa badala ya wazungu kuhamishia pes zetu huko kwao. Utawaona wazungu wanacheza na mitumwi kwenye mito na mabwawa na huko beach wakistarehe kwenye campers zao huku afrika tukivuja jasho kuwafanyia kazi.
 
KIU ni chuo cha Mzee (M7) ila hao wengine wanatumiwa kama kuficha mambo

Mkuu juzi nilikuwa Gongo la Mboto, nikawa na shahuku ya kutembelea KIU yaani kitu nilicho kiona pale kilinistaajabisha kweli kweli - Basajja Balaba si mchezo! Sijuhi kwa sasa hivi hapa Tanzania kama kuna Chuo chochote Kikuu ambacho kimejengwa kwa umahili mkubwa kiasi hicho, chuo chenyewe kime-cover area kubwa sana-kinaweza kuwa cha pili kwa ukubwa wa eneo kikifatia UDSM. Vitivyo vimepangwa kwa ustadi mkubwa, barabara, bustani nk - jamaa huyu mkali kweli kweli na akifanikiwa kuwapata walimu makini basi chuo chenyewe kitakuwa moto wa kuotea mbali.

Basajja Balaba ni Mganda na M7 ni Myankole kama alivyo Baguma - sasa uswahiba wa B.Balaba na M7 unatoka wapi? Inawezakana wakawa wanashirikiana kama joint venture lakini atuwezi kuwa na uhakika, ungesema Baguma anashirikiana na M7 katika ventures nyingine, hilo linawezekana na hakuna ubaya wowote; na vitu kama hivyo M7 huwa ashughuliki navyo sana mtu mwenye business acumen ni Mdogo wake Kanali Salim Salahe ndiye mwenye ujuzi katika mambo ya biashara.
 
Pesa za Gaddafi nyingi sana UG.
 
Jinsi historia yake inavyodokolewa japo kwa vipande vipande inaonyesha jamaa anapiga dili zake halali tu, hana noma.
 
Kwa taarifa wasomali wa paradise walikuwa nayo sambamba na City Garden ambayo nayo walishaibadilisha jina. Kama kweli hakuna fishy business ni kwa nini wanabadilisha majina ya vitega uchumi vyao ilihali bado wanavimiliki? Na je ile hotel nyingine TANSOMA iliyopo hapa mataa ya kamata ni ya nani? Tena walilifuta jina hili baada ya kuonekana ni controversial hasa baada ya kuhusisha hela za maharamia na mushrooming tourist investments za wasomali. Tanzania imekuwa ikilaumiwa kuwa wanahifadhi vitega uchumi vya wasomali maharamia!!! Na ikumbukwe kuwa tangu tumewaruhusu wasomalii na biashara zao za vivuli tumakaribisha mfumuko wa hela maana kuna hela nyingi katika mzunguko ambazo ni illigal na hazina mutliplier effect kea uchumi matokeo yake mfumuko wa bei unaelekea 30%!!!! ambayo tumeshausahau tangu maiaka ya 95 onward. Kumekuwa na tabaka la walionacho na wasionacho na kwa kuwa biashar hizi zina nguvu fulani, who cares about majority living in abject poverty.
 

Well said Mkuu. Well done, na mimi concern yangu ni hiyo hiyo siyo kwamba nachukia wawekezaji wa KWELI wasiyo na an hidden AGENDA.
 
Mzee Mwanakijiji.

Mbona Wazungu matajiri wa Tanzania utaki kufahamu habari zao wewe na weusi tu.

Mbona hujauliza yule Mzungu mmiliki wa Hoteli ya Sleep Way, ni nani na anafanya nini Tanzania.

Kama una habari za huyo mzungu tujuze sio mpaka uulizwe
 

Mkuu ukitoa analysis makini kama hiyo utahambiwa Watanzania walalamishi, wana wivu, wavivu nk. Tunashindwa kuona mbali - kwamba mambo kama haya tukiyanyamazia TAIFA letu linaweza kupata zahama za kutisha.
 
Be careful! Sio kila utajiri ni safe made...wengine wako kwenye mission tofauti under the guise of being entrepreneurs.

1. JB alikuwa mwanajeshi wa Uganda?
2. JB ana mahusiano ya karibu/mazuri tu na wasomali?
3. JB anafanya biashara na akiwa na mafanikio makubwa?
4. JB anamahusiano ya karibu na wakubwaa wa nchi yetu Tz?

Hapo penye red "Ndahani" jaribu kukumbukia wale waganda wa Kinondoni karibu na kituo cha mafuta cha Mwanamboka waliokuwa wanafanya Biashara yao ya mafriji etc waliishia na kesi gani...kweli we must be careful
 

Mkuu wangu Kimbunga.

Bob Justus Baguma, ni kichwa sana mie huwa nina mfananisha na (Wapopo).

Kainunua Paradise Hotel Bagamoyo, kutoka kwa kile kichwa ch kisomali kilikuwa waziri kule Somalia wakati wa utawala Said Bare.

Mwaka 2011 nilikuwa Kampala Uganda, huyo jamaa Bob JB, alikuwa anafunguwa mgahawa wa MacDonalds.

Mwaka 1999 ana kampuni tatu Uk.

Jamaa ni mfanyabiashara kweli kweli sio mchezo.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…