Je, Aga Khan Sea View, ni kwa wahindi, wabunge, mawaziri na viongozi wa juu wa Serikali tu?

Je, Aga Khan Sea View, ni kwa wahindi, wabunge, mawaziri na viongozi wa juu wa Serikali tu?

P

Pesa yako ndiyo inaamua utibiwe wapi uishi wapi, mwanao asome shule gani, utembee na mwanamke gani. Hospitali ya Agha Khan haimbagui mtu kutibiwa pale. Hiyo bima yako haina sifa ya kukubalika pale lakini ziko bima zingine zinakubalika kwa sababu ya package ya hizo bima. Bima uliyonayo gharama inazolipa ni za chini kuliko viwango vinavyochajiwa na hiyo hospitali.

Acha kuingiza siasa kila mahali.
Unao uhakika, inakuaje naweza kutibiwa kwenye hospitali za Aga Khan walizofungua uswazi ambazo wao wenyewe hawatii mguu huko, yaani huko wametenga wafanyakazi waswahili tu.
Ukitaka kumbagua mtu unaweza ukatengeneza vikwazo ambavyo vipofu kama wewe hawawezi kuvitambua, mimi binafsi nilikuwa natibiwa hapo Sea View na ubaguzi kati ya wafanyakazi wahindi na waswahili nilikuwa ninauona, pia na kwenye kuhudumiwa.
 
Mkuu Hismastersvoice , Aga Khan main hapo, hawatubagui kabisa sisi akina REGULAR JOE/JUMA. Ila wana operate kutokana na makubaliano yao na NHIF.

NHIF bima zao zina category nyingi. Wana bima za mashirika kama BOT, TPA, TANESCO n.k halafu kuna bima zile za walimu, wahudumu wa afya nk (standard). Hizi ndizo zinaamua huduma zipi upate na zipi usipate.

So Aga Khan wamekubaliana na serikali yetu, watanzania watakaotibiwa hapo ni wenye bima za mashirika tuu. Hizi standard ( za walimu, ma-dr sumbawanga, manesi mwananyamala, n.k zitapokelewa Aga Khan za mitaani huku.

Kingine tunachotakiwa kujua ndugu wananchi, hata hizi hospital na polyclinic za pembeni, dawa tunazopata wakati mwingine zinatofautiana kutokana na aina ya bima yako.

Mfano mimi ni mwalimu, nimeenda polyclinic X na mfanyakazi wa TPA ameenda hapo hapo X. Wote tuna kikohozi, na wote tumeandikiwa cough sysrup. Tukienda kuchukua dawa, mimi nitapewa Zecuf yangu ya 3,000. Lakini mwenzangu atapewa Benyln ambayo inauzwa mpaka 20,000
Sawa, je na viwango vya madakitari wa Sea View na uswazi vikoje tukiacha bima.
 
Mnao tetea ubaguzi huu wa tiba naomba mfafanue pia kuhusu hizo hospitali za Aga Khan zilizotengwa uswazi na wafanyakazi wa kiswazi tu, je, wanauhusiano wowote na viwango vya malipo ya huduma? Kwanini wahindi hawahudumu kwenye hospitali hizi?
 
Mhindi akifariki waswahili hujaa nyumbani kwake japi wenye nyumba hawapendi, mswahili akifariki hautamuona mhindi hata mmoja.
 
Mnao tetea ubaguzi huu wa tiba naomba mfafanue pia kuhusu hizo hospitali za Aga Khan zilizotengwa uswazi na wafanyakazi wa kiswazi tu, je, wanauhusiano wowote na viwango vya malipo ya huduma? Kwanini wahindi hawahudumu kwenye hospitali hizi?
Nakupa mfano kaka, Ukila chakula cha uswazi 1500, Chakula kilekile utakula kwa 5000 Masaki... Pengine yawezekana mmiliki wa migahawa hii akawa mmoja ila kinachoangaliwa ni brand/hadhi ya eneo husika.
 
Good observation.Na hicho chakula cha 5000,kinakua na quality nzuri pia.
Nakupa mfano kaka, Ukila chakula cha uswazi 1500, Chakula kilekile utakula kwa 5000 Masaki... Pengine yawezekana mmiliki wa migahawa hii akawa mmoja ila kinachoangaliwa ni brand/hadhi ya eneo husika.
 
Mkuu vipimo ni gharama kubwa sn, siyo kwamba alikuwa hataki kufanya checkup isipokuwa ni urasimu wa wizara ya afya ndiyo tatizo
Ulichoandika ni kweli.Nilielezwa alikua akilalamika kua anaumwa,lakini ndo hivyo anajikazakaza,anatumia dawa anatuliza maumivu,kumbe ndani anaisha,umaskini ni mbaya sana,mwishowe ndo hivyo.May her soul R.I.P
 
Ulichoandika ni kweli.Nilielezwa alikua akilalamika kua anaumwa,lakini ndo hivyo anajikazakaza,anatumia dawa anatuliza maumivu,kumbe ndani anaisha,umaskini ni mbaya sana,mwishowe ndo hivyo.May her soul R.I.P
Kuna dada yupo twitter anahitaji 90M kwenda India arudi normal leo mwaka wa 12 yupo kitandani maza yupo busy na kununua magoli ya Simba
 
Katikati ya mwaka huu yaani 2023 mwezi wa sita nilikwenda hospitali ya Aga Khan iliyopo Sea View Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu, kama taratibu zilivyo niliwasilisha kadi yangu ya bima ya afya ilipokelewa na nikapewa jibu kuwa siwezi kutibiwa kwenye hospitali hiyo!

Haikuwa shida kwangu, nikaenda hospitali ya Shree Hindu Mandal iliyopo Upanga na nikapata tiba kwa kutumia kadi hiyohiyo.

Mwezi huu wa kumi nilienda kwenye tawi la hospitali ya Aga Khan lililopo uswahilini na nikisema uswahilini ni uswahilini kweli kwani madakitari, manesi na wafanyakazi wengine ni waswahili wenyewe wanakili wahindi wa uzao wa Aga Khan hawakanyagi huku uswazi!

Baada ya kupata tiba kwenye hilo tawi letu la hospitali ya Aga Khan nikamuuliza dakitari kuhusu hospitali mama ya Sea View, naye hakusita kuniambia kuwa kule ni kwa wahindi, wabunge, mawaziri na viongozi wa juu wa serikali, nikajua kuwa ukiwapendelea hawa basi jambo lako litakwenda vizuri bila kuhojiwa.

Miaka iliyopita tulikuwa tukitibiwa bila tatizo kwenye hospitali hiyo ya Aga Khan Sea View licha ya tatizo la hawa wazalendo watanzania wenzetu kutokujua kiswahili vizuri, lakini walipoona tunawabana wakatufungulia matawi uswazi na madakitari wetu wakiswazi tumaliziane huku huku.
Hayo ni matokeo ya kuiharibu hospitali iliyoandakiwa Kwa ajili ya kundi hiLo MUHIMBILI MLONGAZILA
 
Back
Top Bottom