Je, akili inaweza kuudhibiti moyo?

Je, akili inaweza kuudhibiti moyo?

Mtu akipigwa heartbreak kumbe maumivu yanaenda kwenye ubongo sio moyo?
😁
min -me
Japo umeuliza kwa kejeli kwa kuweka emoji ya kucheka,ukimaanisha kua mimi ni mjinga na wewe ndiye mwerevu zaidi,ila nitakujibu ili na wengine wafaidike,

Tatizo hii issue mnaichukulia kimazowea,hii ni sayansi,ni issue ya Biological and chemical reaction behind emotion pain,
hii mada inahitaji majibu ya kisayansi sio majibu ya kufikirika,

Heart break inaanzia kwenye Brain,pale unapoachana na mpenzi wako,hii ni biological process inayoanzia kwenye brain.
 
“Kuna minyororo ambayo haionekani kwa macho, lakini humfunga mtu kuliko chuma.

Minyororo hiyo ni hisia.”
Moyo unataka kile kinachokufurahisha leo.
Akili inapaswa kujiuliza: “Hiki ninachotaka leo, kitanigharimu nini kesho?”

Ndiyo maana mtu anaweza kujua kabisa kwamba jambo fulani linamuumiza, lakini bado akarudi kulifanya.
Anaweza kujua mtu fulani hamfai, lakini bado akampenda.
Anaweza kujua matumizi fulani yanamfilisi, lakini bado akaendelea kutumia.
Anaweza kujua hasira itamletea matatizo, lakini bado akasema maneno ambayo baadaye atayajutia.

Kwa nini?
Kwa sababu katika maamuzi ya mwanadamu, hisia na fikra za kimantiki hufanya kazi kwa kushirikiana; maeneo kama amygdala yanahusika katika thamani na hisia, huku prefrontal cortex ikihusika sana katika kupanga na kutathmini hatua zinazowezekana.

Kama akili inajua jambo ni baya lakini moyo bado unalitaka, nani anapaswa kushinda?
👉 Moyo unaosema: “Nataka.”
au
👉 Akili inayosema: “Usifanye, utajuta.”
Na je, kujizuia kufanya jambo unalolitamani ni udhaifu wa moyo—au ni nguvu ya akili?

Huenda ushindi mkubwa wa mwanadamu si kupata kila kitu anachokitamani.
Huenda ushindi mkubwa ni kuwa na uwezo wa kusema “HAPANA” kwa kitu ambacho moyo wako unakitamani sana, kwa sababu akili yako imeona madhara yake.

Sasa wewe unaonaje: JE, AKILI INAWEZA KUUUDHIBITI MOYO, AU MWISHO WA SIKU HISIA NDIZO HUWA NA NENO LA MWISHO?
Boresha swali lako liwe hivi "JE,AKILI INAWEZA KUDHIBITI HISIA?".

JIBU:Ndio, akili inaweza kudhibiti hisia lakini Ubongo hauwezi kudhibiti hisia kwa sababu unafanya kazi kwa Karibu Sana na hisia.

Kwa mfano. Umepatwa na hasira,ubongo unakupush uue ili upate relief(ahueni) lakini Akili(Ufahamu) kwa kujua madhara mabaya yatakayotokea baada ya kuua ikakushauri usiue ingawa bado maamuzi ya mwisho yanabaki mikononi mwako kwamba uchague kuua(kutekeleza) au la!
 
Inaonekana hata hujui kazi ya moyo,
hakuna uhusiano wowote kati ya moyo na akili/Brain katika maamuzi ya Binadamu,

Moyo ni Pump inayo sukuma damu through your body,

Kazi ya kufikiri,memory,movement feeling na automatic action kama kupumua na mapigo ya moyo hufanywa na part of the brain inayoitwa Celebrum,

Huo moyo wenyewe unafanya kazi kwa maamuzi ya brain kwa kupokea tiny electrical and chemical signal kwa kupitia kwenye nerves kutoka kwenye brain,hata mapigo ya huo moyo hupata amri kutoka kwenye brain ''Celebrum''
SINOATRIAL NODES tunaiweka upande gani hapo? ambayo ni sehemu ya moyo upande wa kulia chini kwenye ukuta wa ventrical.
 
Ukimpendea mtu kwa kuwa ana hela hiyo ni tofauti mapenzi hayo hayajaanzia moyoni so akili ina controll kila kitu maana hakuna hisia hapo so akili inaweza kukuambia namchuna tu huyu hela zake,na upande wa pili atajua tu humpendi kutokana na vitendo vyako utasikua hunipendi ni kweli humpendi maana akili na hisia za moyo hujitenga maana ni jambo halijaanzia moyoni,

Moyo ucontroll hisia na akili uleta matekelezo so the reall boss here ni moyo mkatae tu ila ndiyo hivyo
 
Ukimpendea mtu kwa kuwa ana hela hiyo ni tofauti mapenzi hayo hayajaanzia moyoni so akili ina controll kila kitu maana hakuna hisia hapo so akili inaweza kukuambia namchuna tu huyu hela zake,na upande wa pili atajua tu humpendi kutokana na vitendo vyako utasikua hunipendi ni kweli humpendi maana akili na hisia za moyo hujitenga maana ni jambo halijaanzia moyoni,

Moyo ucontroll hisia na akili uleta matekelezo so the reall boss here ni moyo mkatae tu ila ndiyo hivyo
Unalazimisha mambo ya dini yaumeze ukweli
 
Sio kama umekosa maarifa ya kuchakata majibu umebaki njia panda hivi kweli unaanza kupenda kutumia akili au hisia zilibebwa kwenye moyo,akili inaweza kukuambia yule mwanamke ni mkubwa ki umri kwangu lakini nampenda hiyo lakini nampenda ni hisia zilizopo kwenye moyo
Mkuu utakuja kuchekwa coz unajibu kwa hisia zinavyokutuma na sio kwa elimu ya kibaiolojia uliyo nayo
Basi tufanye upo sahihi kwa upande wako.
 
Hii ni issue ya kisayansi sio issue ya kidini,
Toka lini Moyo ukabeba hisia? Kama ni imani basi endelea kuamini ila uhalisia haupo hivyo,

Huwezi kusema kinachokula chakula ni miguu wakati chakula hupitia mdomoni,yani kazi inayofanywa na brain wewe unataka kutuaminisha kua kazi hiyo hufanywa na Moyo!
Nakupata vizuri sana, Kuna mahali Biblia imetumia neno moyo ila inazungumzia roho
 
Back
Top Bottom