Je, akili inaweza kuudhibiti moyo?

Je, akili inaweza kuudhibiti moyo?

Mkuu utakuja kuchekwa coz unajibu kwa hisia zinavyokutuma na sio kwa elimu ya kibaiolojia uliyo nayo
Basi tufanye upo sahihi kwa upande wako.
Nimesoma topic ya cordination kwenye biology A Level vizuri sana naelewa vyema nachokisema sijakurupuka,usijali nikichekwa ni vitu vidogo sana huwezi ukaogopwa kuchekwa ukiwa unajielezea hutakiwi kujali nani anacheka nani anakuinaje jambo la msingi ni nini unachokiamini na kukielewa ni hivyo tu
 
Umekubaliana na jibu langu au unanipinga?
Bado nasema moyo ndiyo boss wa viungo vyoto vya binadamu ukifa moyo ukiacha peleka damu mwilini hata hiyo akili haitafanya kazi,hisia huvebwa moyoni akili inatekeleza simple
 
eti unavunjika vunjika ila pastor😅😅😅
😂😂😂😂 ndiyo moyo huleta masikituko makubwa 😀,uachwe unazimia ulazwe then unamka unamkumbuka kilitokea nini tena unakumbushwa unazimia tena😂😂
 
😂😂😂😂 ndiyo moyo huleta masikituko makubwa 😀,uachwe unazimia ulazwe then unamka unamkumbuka kilitikea nini tena unakumbushwa unazimia tena😂😂
😆😆😆😆 sitaki kuamini kama kuna watu wanafikiaga hiyo stage walah, naona cycle yangu inawatu mioyo migumu😀
 
“Kuna minyororo ambayo haionekani kwa macho, lakini humfunga mtu kuliko chuma.

Minyororo hiyo ni hisia.”
Moyo unataka kile kinachokufurahisha leo.
Akili inapaswa kujiuliza: “Hiki ninachotaka leo, kitanigharimu nini kesho?”

Ndiyo maana mtu anaweza kujua kabisa kwamba jambo fulani linamuumiza, lakini bado akarudi kulifanya.
Anaweza kujua mtu fulani hamfai, lakini bado akampenda.
Anaweza kujua matumizi fulani yanamfilisi, lakini bado akaendelea kutumia.
Anaweza kujua hasira itamletea matatizo, lakini bado akasema maneno ambayo baadaye atayajutia.

Kwa nini?
Kwa sababu katika maamuzi ya mwanadamu, hisia na fikra za kimantiki hufanya kazi kwa kushirikiana; maeneo kama amygdala yanahusika katika thamani na hisia, huku prefrontal cortex ikihusika sana katika kupanga na kutathmini hatua zinazowezekana.

Kama akili inajua jambo ni baya lakini moyo bado unalitaka, nani anapaswa kushinda?
👉 Moyo unaosema: “Nataka.”
au
👉 Akili inayosema: “Usifanye, utajuta.”
Na je, kujizuia kufanya jambo unalolitamani ni udhaifu wa moyo—au ni nguvu ya akili?

Huenda ushindi mkubwa wa mwanadamu si kupata kila kitu anachokitamani.
Huenda ushindi mkubwa ni kuwa na uwezo wa kusema “HAPANA” kwa kitu ambacho moyo wako unakitamani sana, kwa sababu akili yako imeona madhara yake.

Sasa wewe unaonaje: JE, AKILI INAWEZA KUUUDHIBITI MOYO, AU MWISHO WA SIKU HISIA NDIZO HUWA NA NENO LA MWISHO?
Kwa muktadha wako unamaanisha nini unaposema neno "moyo na pia neno Hisia"

Kwakua mkuu hou moyo unaouzungumzia hapa sio Moyo ni hisia[emotions] ambazo nazo zinazalishwa na huohuo UBONGO ukiwa katika hali fulani...

Moyo tunaoujua sote kwa mujibu wa sayansi yasasa jukumu lake ni kusukuma damu. Nao pia utaathiliwa na hali ya ubongo katika mapigo yake na kutengeneza various electromagnetic waves.

Kwa kifupi sana Moyo ni pump ya damu mwilini inayoongozwa na ubongo.

Hivyo UBONGO ndio unaamua kila kitu itategemea na utashi wa mtu kama anaendeshwa na hisia[moyo] au logic. [Ubongo] hivi ndivyo umemaanisha.
 
Watu wengi hudhani moyo hua una feel au ndio wenye maamuzi kama vile kupenda! hakuna kitu kama hicho,kila kitu kinaanzia kwenye Brain,

Eti utasikia Moyo wangu umekupenda,
Toka lini moyo ukawa na hisia ya kupenda!

“Hoja yako ina sehemu ya ukweli, lakini kuna kuchanganya maana ya ‘moyo’.
Kisayansi, hisia kama mapenzi, huzuni, furaha na hofu hutengenezwa na kuchakatwa hasa na ubongo, kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo limbic system

Ndiyo maana mtu akiwa katika mapenzi au hofu, ubongo huweza kuufanya moyo upige kwa kasi.
Lakini swali ni hili: kwa nini tangu zamani binadamu ametumia ‘moyo’ kuelezea hisia? Kwa sababu tunapopata hisia kali, mabadiliko ya mwili huonekana sana kwenye moyo—mapigo kwenda kasi, kwenda taratibu, au kuhisi presha kifuani.

Kwa hiyo kusema ‘moyo wangu umekupenda’ ni lugha ya kuelezea hisia, si madai kwamba moyo wenyewe ndio unaendesha mchakato wa kufikiri kama ubongo.
Kwa kifupi: ubongo ndio kitovu kikuu cha kutengeneza na kuchakata hisia, wakati moyo huathiriwa na hisia hizo na pia hutuma taarifa za mwili kwenda kwenye ubongo.
Sasa swali la msingi ni: kama tunakubaliana kuwa mapenzi yanahusisha ubongo, je hilo linaondoa kabisa maana ya ‘moyo’ katika lugha, fasihi na dini? Au tunatumia neno moyo kwa maana pana zaidi ya kiungo cha kusukuma damu?”
 
Kwa muktadha wako unamaanisha nini unaposema neno "moyo na pia neno Hisia"

Kwakua mkuu hou moyo unaouzungumzia hapa sio Moyo ni hisia[emotions] ambazo nazo zinazalishwa na huohuo UBONGO ukiwa katika hali fulani...

Moyo tunaoujua sote kwa mujibu wa sayansi yasasa jukumu lake ni kusukuma damu. Nao pia utaathiliwa na hali ya ubongo katika mapigo yake na kutengeneza various electromagnetic waves.

Kwa kifupi sana Moyo ni pump ya damu mwilini inayoongozwa na ubongo.

Hivyo UBONGO ndio unaamua kila kitu itategemea na utashi wa mtu kama anaendeshwa na hisia[moyo] au logic. [Ubongo] hivi ndivyo umemaanisha.
Kwahiyo hisia hazitoki kwenye MOYO?
 
SINOATRIAL NODES tunaiweka upande gani hapo? ambayo ni sehemu ya moyo upande wa kulia chini kwenye ukuta wa ventrical.
Mkuu hii Sinoatrial Nodes ni Natural Pacemaker,ingawa hua inafanya kazi on its own but still inapokea command kutoka kwenye brain,

Mfano,pale mtu anapokua anakimbia au amepatwa na hofu,brain hupeleka signal ''Sympathetic System'' ili ku speed up mapigo ya moyo,
Unapokua umerelax,Brain hupeleka signal kwenye moyo ''Parasympathetic System'' ili kushusha mapigo ya moyo,to slow don heart beat when you are rest,

Kwa kifupi Heart Rate Speed inakua adjusted by brain to match what your body needs.
 
haswaaaaa nataka kushuhudia maana mi huwa naona kwenye movie tu najua ni maigizo😅
Miaka ya nyuma kidogo nipo chuo jamaa alitaka kujirusha ghorofani kisa mapezi yani alidakwa chapu bila kumzuia alikua anajitupa,jamaa alipenda halafu alikua mbishi kuamini alimuhudumia sana yule demu hadi ada wakati wote walikua wanachuo,akaambiwa kuwa mpenzi wake ana mwanaume mwingine,watu wabaya wakamletea ushahidi 😁😁 ah acha banah ,ila sahivi anajiona alikua mjinga
 
Back
Top Bottom