Je, Allah alikuwepo kabla ya kushuka Quran?

Tatizo siyo dini tatizo naloliona hapo ni elimu yetu duni inayofanya mtanzania kutojua kwamba duniani kuna lugha mbali mbali

Pili ungejua misingi au maana ya uislamu usingejiuliza hayo maswali yako,maa uislamu msingi wake ni kwamba mungu ni mmoja ,na alitumia mitume kugikisha ujumbe duniani kuanzia adam, musa hadi muhammad
Allah kwa kiarabu ni mungu, awe mkristo awe muislamu wote wanatumia neno allah kumaanisha mungu
Na mungu hajawahi kubadilika na ni mmoja tu hata ukiwauliza watu wa musa yani jews watakwambia mungu ni mmoja ambao kwao mungu ni yahweh,ikimaanisha mungu, na hakuna mungu watatu kama wazungu wanavyowadanganya
Na mungu alileta amri kumi ,na masharti ya chakula kama kula wanyama wanaocheua na wenye kwato zilizogawanyika ukienda kwa watu wa musa watakwambia waliambiwa hivyo, na ukiangalia quran utakuta hivyo hivyo
Swala haponi elimu tu hakuna kinachochanganya
 
kwani kati ya shahawa na binadam nini kilianza?
 
Mzee si umesema Allah alikuwepo,na Abdullah alikuwa mtumwa wa Allah na uislamu ulikuja baada ya yeye kufariki..je Alikuwa anamtumikia Allah yupi maana yeye alikuwa mpagani
Kwa bahati mbaya Mimi Nimejibu swali ulilouliza!

Ambalo niki "Recall" limeuliza Kuwa

"Je, Allah alikuwepo kabla ya kushuka Quran?"​


Na Nimekujibu Ndiyo kwa Mujibu wa Historia..
Swala la nani alikuwa Anamuabudu huyo allah ni swali Ambalo Mikono yangu Imefungwa Kulijibu..

Ila tu ningependa Kujua Definition yako Ya Upagani hasa ni nini? (Maana Ni neno Jipya uliloliweka Ambalo sikulizungumza)
 
Ngoja waje
 
Mzee si umesema Allah alikuwepo,na Abdullah alikuwa mtumwa wa Allah na uislamu ulikuja baada ya yeye kufariki..je Alikuwa anamtumikia Allah yupi maana yeye alikuwa mpagani
Naweka Record Sawa Tena..
Abdullah hakuwa Mtumwa wa Allah..

Ila neno Abdullah kwa Lugha ya Kiarabu Limetokana na Maneno mawili Abdu na Allah ambayo tafsiri Yake ni Mtumwa wa Allah
 
Sawa je Allah ayezungumziwa kwenye Biblia na huyu aliyezunguzmiwa kwenye quran ni sawa? na kama ni sawa kwa nini Biblia izungumzie kusulubiwa kwa Yesu halafu Allah wa quran aje kukataa?
 
Muhammad siyo.mtume wa mungu anaye bisha anyoshe kidole juu nimshushie nondo ...mimi siyo shabiki wa ukristo wala uislamu hivyo ninapo sema kitu kuhusu dini ninakuwa ki logic zaidi
 
Wataalamu wa dini na wana historia wabobevu naomba mnisaidie hii mada maana imekuwa ikiniumiza kichwa kwa muda mrefu.Inasemekana uislamu ulikuja enzi za nabii Muhammad na ndio kipindi ambacho ilishushwa qurani.
Na Nani atajitenga na Mila ya Ibrahim isipokuwa anayeitia nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na hakika yeye akhera atakuwa miongoni mwa watu wema.
Qur'an 2:130

Na Mola wake mlezi alipo mwambia : Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu,nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu wote. Qur'an 2:131

Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii,basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu,wanyenyekevu. Qur'an 2:132

Je; Mlikuwepo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: mtamuabudu Nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu mmoja tu,na sisi tunasilimu kwake. Qur'an 2:133.
Hivyo hoja yako ya Muhammad kuwa muislamu wa Kwanza kwa mujibu wa hizo Aya haina mashiko.
Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipoinyanyua misingi ya Ile nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika wewe ndiye msikizi Mjuzi. Qur'an 2:127

Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako,na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio Silimu kwako. Na utuonyeshe njia za Ibada yetu na utusamehe. Bila Shaka wewe ndiye mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
Qur'an 2:128

Enyi watu muabuduni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni nyingi na wale wa kabla yenu ili mpate kuokoka. Qur'an 2:21

(Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko,na mbingu kama paa,na akateremsha maji kutoka mbinguni,na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika,na hali nyinyi mnajua. Qur'an 2:22

Na ikiwa man Shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni Sura moja ya mfano wake,na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu ikiwa manasema kweli. Qur'an 2:23


Na mkitofanya na wala hamtofanya kamwe. Basi uogopeni Moto ambao kuni zake ni watu na mawe walioandaliwa hao wanao kanusha.
 
Mzee hivi unajua wamepita manabii wangapi tangu Ibrahimu mpaka kuja kwa Issa..au Issa hakuwa muislamu?
Issa hakuwa muislamu na ushahidi ni Muhammad mwenyewe na maandiko ya uislamu
 
Kabla ya kuja kwa Yesu si kulikuwa na watu wazuri wanafanya ibada kama MARIAM, Yohana, zakaria walikuwa wanafuata mafundisho gani
umeshasema kabla ya kuja kwa Yesu..mimi nazungumzia baada ya kuja kwa Yesu,iweje ampuuzie Yesu ambaye alikuja kuutangaza uislamu akabaki na utaratibu wa Ibrahimu ambaye alikuwa mtume wa kale sana?
 
Mleta mada fanya kwanza utafiti kabla ya kuuliza uislam hakuja enzi za Muhammad na Muhammad kwenye umri huo hakupewa uislamu walipewa utume vitabu vya uislam vilikua taurat injili zaburi na qur an na hivyo vilikua ama viliharibiwa sababu uislamu ulikua haujakamilika mpaka ulipo kukamila chini ya s a w na ahadi ya Allah juu ya kuilinda qur yake dhidi ya machafu au njama zozote ilizofanywa kwa vitabu vyengine ndio maana akawaambia kama mnaweza mtengeneze mfano wa aya moja tu kama mtaweza kwakua qur an imekamilika na haiwezekani kuchakachuliwa qur an haijakopi vitabu vyengine imeelezea tu baadhi ya vitabu ama matukio yalotokea kwenye vitabu vyengine ama zama nyengine mwisho qur an inakataa kua Yesu ama masih issa alisulubiwa Allah katika Quran ana jielezea ama kujipea sifa yake kua yeye ndio ya mwanzo na wa mwisho
 
Wao wanadai hata Yesu alikuwa muislamu. Ukiwaambia mbona yesu alikuwa havui malapa anapoenda hekeluni wanaanza braah braah kibao na ukali juu
Hata nabii Muhammad s a w alikua akiingia msikitini na viatu hii ni moja ya sunna kubwa kabisa za mtume s a w ambazo kwa sasa hazifuatwi kwa makasudi ama bahati mbaya nabii issa alikua muislam
 
Umedanganya. Mungu aliyemtuma Yesu ni tofauti na allah au wa Muhamad. Waislamu sijajua why wanapenda kumfananisha mungu wao na wa Wakristo. Wakristo wao HAWAMTAMBUI ALLAH, HAWAMTAMBUI MUHAMAD, HAWAITAMBUI QURAN.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…