Je anachofanya Israel kinakuza au kuondoa Ugaidi ?

Je anachofanya Israel kinakuza au kuondoa Ugaidi ?

kuongelea Mandela hivi unajua mpaka 2013 alikuwa katika baadhi ya list za magaidi ?
Hiyo ya Mandela naifahamu ila naongelea kwa hapa Tanzania humu comments zote ni kuwa Hamas au Iran ni magaidi ila Mandela au FRELIMO ni freedom fighters sio magaidi.

Therefore napinga hii definition maana ipo subjective, ungesema tu ni wale freedom fighters ambao hawapatani na USA ndio magaidi!! Otherwise kuna makundi ni pro-USA mfano UNITA hakuitwa gaidi alipomsaidia USA huko Angola, same to RPF hawaitwi magaidi, au Khalifa Haftar kule Libya.
 
Kwenye nafasi ya Israel ungefanya jambo gani baada ya shambulio la October 7?
 
Mandela alipigania uhuru wa nchi yake
Uhuru gani wakati Afrika Kusini ilipata uhuru kabla vita kuu ya kwanza ya dunia!! Sema alipigania haki za watu weusi dhidi ya ubaguzi same to Palestina wanapinga kubaguliwa ndani ya ardhi yao wenyewe.
Israel ni nchi ya waisrael sio wapalestina
Wapalestina ni wavamizi

Hakuna taifa duniani la Palestina halijawahi kuwepo pale.
Hujitambui, kwahiyo kabla ya ukoloni wa Boers je kulikua na nchi inaitwa Afrika kusini? Au kabla ya uhuru wa Tanganyika kuliwahi kuwepo taifa la Tanganyika? Hii sio hoja kabisa. Hata kwenye Biblia ukisoma hao Israel ilivamia Canaan iliyokua na makabila kibao mfano Caphtorites, Gilagshites, Hivites, n.k na hao wapo mpaka leo so tukisema twende kwa nani alikua wa Kwanza basi Israel hawana haki kabisa.
 
Kwenye nafasi ya Israel ungefanya jambo gani baada ya shambulio la October 7?
Ningewapa uhuru palestina na kuwaachia ardhi yao. Mbona baada ya Mau Mau uingereza aliondoka au mbona baada ya ugaidi wa ANC wazungu walikubali yaishe!!

Unapisha watu nchi yao ndio suluhu,
 
Ningewapa uhuru palestina na kuwaachia ardhi yao. Mbona baada ya Mau Mau uingereza aliondoka au mbona baada ya ugaidi wa ANC wazungu walikubali yaishe!!

Unapisha watu nchi yao ndio suluhu,
Ni sawa Malawi wapige bomu pale Mbeya liuwe watu zaidi ya 2000. Then simple tu tuseme let it go.

Tunaongelea maisha ya watu. Halafu case study ya ANC na wazungu, Maumau na wazungu huwezi ukazirelate na kinachoendelea mashariki ya kati.
 
"Ugaidi" na ideologies vinashindika ikiwa upo tayari kufanya mauaji ya halaiki na scorched earth hadi adui abakie hawezi hata kuinua kidole.
Hauwezi kuua ideology kwa kuonyesha kwamba unaua wenye hoja na sio hoja zenyewe ukiua mmoja anayesema kwamba tunanyanyaswa wanazaliwa wengine kumi..., ila ukimshinda kwa hoja nayesema kwamba tunanyanyaswa au hata kumnunua na yeye awe champion wa unachosema mwisho wa siku na yeye atakuwa upande wako..., Wakoloni walitumia mabavu kuja kwenye shamba la bibi kuchota mali sasa hivi viongozi wetu na watu wenye uroho na umimi wanawapelekea mali hizo wenyewe....
Wamarekani waliwaangamiza Wenyeji,
Waliwaangamiza huku video zinasambaa ulimwengu mzima au waliwaangamiza kwa kuua chakula chao na kuondoa utamaduni wao kwamba ni wa kipumbavu na kuaminisha dunia nzima kwamba wale sio na ni for betterment of the world kuwaondoa..., ndio maana mpaka leo kuna movies za jinsi mtu mmoja (the good guy) anavyoweza kwenda na kuwacharaza marisasi wale mashetani na yeye ndio mtu mzuri (na hata dini indoctrination ikatumika kwa kuwapumbaza watoto wao kwamba wanachoamini hakifai) Sio mabavu pekee pale idoctrination na propaganda
Wajerumani walifanya hivyo wakati wa Maji Maji,
Unadhani ingekuwa dunia ya leo ambao kila kitu kinatangazwa watu kuona kinachotokea huko Iringa hata wakazi wapenda amani walipo Ujerumani wangekubali kinachotokea Au walikuwa wanadanganywa kwamba huko Africa kuna monsters ambao bila kuwamaliza wataua wafanyabiashara wote ambao wanailetea mali Ujerumani ? Na ikafika wakati kila mtu akaamini kwamba watu weusi ni inferior (Eugenics)
Wachina ni kama wanafanya hivyo huko kwa Uighurs, Wajerumani pia ni kama walitokomeza influence ya Wayahudi Ulaya, Wayahudi wenyewe enzi za agano la kale walikuwa wanachinja kila mtu kasoro wanawake mabikira tu, walikuwa wanaua watu malaki kwa malaki.

Sema kwa sasa sheria za kivita haziruhusu mbinu kama hizo, lakini bado zinatumika kwenye counterinsurgency.
Tofautisha vita vya watu kupambana mitaani au ile ideology kwamba tunaonewa pia kumbuka hivi vita unapigana na invisible enemy.. leo hii wewe au mke wako au ndugu yako anaweza akawa sympathizer wa kinachotokea akaamua kuanzisha a terrorist cell ambayo haina connection na kiongozi yoyote akafanya mambo ya hatari..., kwahio such a war huwezi kuishinda kwa kuendelea kuua au kwa mabavu ni kwa education na kuangalia ni nini watu wanakitaka au wanasema wanakipigania na kushindana nao kwa kuonyesha upande wa pili wa sarafu kwamba wanachopigania ni unreasonable..., sababu kuendelea kuua mmoja wengine nane watajichipukia kinachowaunganisha ni common belief (na kama hio belief ni unreasoble ni kuonyesha jinsi ilivyo unreasonable thus making it harder for them to recruit)
 
Uhuru gani wakati Afrika Kusini ilipata uhuru kabla vita kuu ya kwanza ya dunia!! Sema alipigania haki za watu weusi dhidi ya ubaguzi same to Palestina wanapinga kubaguliwa ndani ya ardhi yao wenyewe.
Hakuna mtu anawabagua wapalestina Israel

Israel ina waislamu wengi sana

Mfano kuna eneo la Nazareth asilimia kubwa ni waislamu sio wayahudi misikiti iko kila kona Nazareth kila baada ya hatua chache lakini hawana shida na Israel wanaishi kwa amani tu miaka nenda rudi hawajawahi gombana na wayahudi sherehe za waislamu wayahudi huenda na sherehe za wayahudi waislamu hurnda kula pilau

Tatitizo liko Gaza vibaraka wa Irani

Wapalestina wana mamlaka yao inaitwa mamlaka ya Palestini na wana Raisi kabisa anaitwa Mahamoud Abbas kodi zote wanakusanya zao za kuendesha mambo yao wala Israel hawahitaji

Sasa utasemaje Israel inawabagua? Israel ina serikali ya majimbo kila mtu haingilii mwingine kipesa nk
Tatizo la Gaza ni Iran Iran ikitwangwa barabara tatizo la Gaza litaisha sababu Iran ndie kajaza Wapiganaji siasa kali Gaza na ndio mfadhili wao
 
Kwenye nafasi ya Israel ungefanya jambo gani baada ya shambulio la October 7?
Unadhani kwa kufanya waliyofanya sasa wametengeneza mashambulio potential kama haya kiasi gani huko mbeleni ? Kumbuka issue za kwamba upo safe ni kwenye movie tu..., mtu hashindwi kuvaa bomu na kwenda kwenye hospitali na kumaliza watu wote...,ila ndio hivyo kuendelea kukemea yanayotokea na kuwamaliza wanaofanya hivyo Surgically ndio way to go.., Dunia nzima ilikemea kilichotokea October 7, ila kuendelea kushangilia kinachoendelea kwa civilians kuuwawa inahitaji kujitoa ufahamu...
 
Hauwezi kuua ideology kwa kuonyesha kwamba unaua wenye hoja na sio hoja zenyewe ukiua mmoja anayesema kwamba tunanyanyaswa wanazaliwa wengine kumi..., ila ukimshinda kwa hoja nayesema kwamba tunanyanyaswa au hata kumnunua na yeye awe champion wa unachosema mwisho wa siku na yeye atakuwa upande wako..., Wakoloni walitumia mabavu kuja kwenye shamba la bibi kuchota mali sasa hivi viongozi wetu na watu wenye uroho na umimi wanawapelekea mali hizo wenyewe....

Waliwaangamiza huku video zinasambaa ulimwengu mzima au waliwaangamiza kwa kuua chakula chao na kuondoa utamaduni wao kwamba ni wa kipumbavu na kuaminisha dunia nzima kwamba wale sio na ni for betterment of the world kuwaondoa..., ndio maana mpaka leo kuna movies za jinsi mtu mmoja (the good guy) anavyoweza kwenda na kuwacharaza marisasi wale mashetani na yeye ndio mtu mzuri (na hata dini indoctrination ikatumika kwa kuwapumbaza watoto wao kwamba wanachoamini hakifai) Sio mabavu pekee pale idoctrination na propaganda

Unadhani ingekuwa dunia ya leo ambao kila kitu kinatangazwa watu kuona kinachotokea huko Iringa hata wakazi wapenda amani walipo Ujerumani wangekubali kinachotokea Au walikuwa wanadanganywa kwamba huko Africa kuna monsters ambao bila kuwamaliza wataua wafanyabiashara wote ambao wanailetea mali Ujerumani ? Na ikafika wakati kila mtu akaamini kwamba watu weusi ni inferior (Eugenics)

Tofautisha vita vya watu kupambana mitaani au ile ideology kwamba tunaonewa pia kumbuka hivi vita unapigana na invisible enemy.. leo hii wewe au mke wako au ndugu yako anaweza akawa sympathizer wa kinachotokea akaamua kuanzisha a terrorist cell ambayo haina connection na kiongozi yoyote akafanya mambo ya hatari..., kwahio such a war huwezi kuishinda kwa kuendelea kuua au kwa mabavu ni kwa education na kuangalia ni nini watu wanakitaka au wanasema wanakipigania na kushindana nao kwa kuonyesha upande wa pili wa sarafu kwamba wanachopigania ni unreasonable..., sababu kuendelea kuua mmoja wengine nane watajichipukia kinachowaunganisha ni common belief (na kama hio belief ni unreasoble ni kuonyesha jinsi ilivyo unreasonable thus making it harder for them to recruit)
Mtu hakatazwi kuwa na ideology. Ila kama anaitumia kufanya "Ugaidi" au uasi anaweza kumalizwa. Sehemu kuwa ya vikundi vya kikomunisti vya Amerika Kusini vimemalizwa kabisa, kwa kipigo tu. Hata Israel hawakatazi wapalestina kuwa na Ideology yoyote. Ila wakiitumia kama msingi wa kufanya "ugaidi" anaweza kuwamaliza au waache huo "ugaidi." Kama nilivyosema, sheria na mazingira ya kisasa haviruhusu scorched Earth na mauaji ya halaiki.
 
Hata tunapofanya usafi wa mazingira huwa tunajaribu kuzuia kipindu pindu au madhara yake, ingawa hakiishi lakini huwa ni zoezi endelevu. Israel inachofanya ni kuzuia na kuondoa UGAIDI. Maisha bila UGAIDI inawezekana.
 
Mtu hakatazwi kuwa na ideology. Ila kama anaitumia kufanya "Ugaidi" au uasi anaweza kumalizwa. Sehemu kuwa ya vikundi vya kikomunisti vya Amerika Kusini vimemalizwa kabisa, kwa kipigo tu.
Communism na ugaidi wapi na wapi ? Na kikundi gani cha Kikomunisti kimemalizwa na sababu ya kipigo; Communism ilimalizwa kutokana na propaganda na watu kuona kwamba what they are preaching is different from reality..., kwahio haikuwa kipigo bali mbinu nyingine ikiwemo na propaganda ya ku paint kwamba everything bad is communism and everything great is capitalism
Hata Israel hawakatazi wapalestina kuwa na Ideology yoyote. Ila wakiitumia kama msingi wa kufanya "ugaidi" anaweza kuwamaliza au waache huo "ugaidi." Kama nilivyosema, sheria na mazingira ya kisasa haviruhusu scorched Earth na mauaji ya halaiki.
Israel anachofanya sasa hivi ni ugaidi ambao unazalisha magaidi wengine and that is why hawawezi kuishi pale peacefully mtu unaishi kila dakika ukitegemea unaweza kulipuliwa kuingia sehemu mpaka upigwe search ya kufa mtu..., In short no one is winning, and what has been done has even made the World less safer....
 
Communism na ugaidi wapi na wapi ? Na kikundi gani cha Kikomunisti kimemalizwa na sababu ya kipigo; Communism ilimalizwa kutokana na propaganda na watu kuona kwamba what they are preaching is different from reality..., kwahio haikuwa kipigo bali mbinu nyingine ikiwemo na propaganda ya ku paint kwamba everything bad is communism and everything great is capitalism

Israel anachofanya sasa hivi ni ugaidi ambao unazalisha magaidi wengine and that is why hawawezi kuishi pale peacefully mtu unaishi kila dakika ukitegemea unaweza kulipuliwa kuingia sehemu mpaka upigwe search ya kufa mtu..., In short no one is winning, and what has been done has even made the World less safer....
Tunazungumzia iwapo ideology inaweza kuuliwa kwa mabavu. Ukommunist nao ni ideology. Huko America Kusini imekomeshwa kwa kipigo. Kama propaganda juu ya uzuri wa ubepari imeshinda basi leo NK na Cuba zisingekuwa za kicommunisti. ANC nao waliitwa magaidi lakini walikuwa na ideology yao. Njia pekee ya kumaliza migogoro ya binadamu ni kipigo mpaka mmoja akae kwa kutulia. Wajerumani walimpa kichapo Abushiri na kumnyonga. Nchi ikatulia. Waliwapa kichapo wazee wa majimaji nchi ikakaa sawa na wakarudi kulima pamba. Hakuna ideology inayoweza kusimama mbele ya kichapo kisichokoma. Hakuna ideology inayoweza kusimama mbele ya jeshi lililotayari kuangamiza mpaka mtu wa mwisho.

Ni vile kwa sasa kelele ni nyingi, lakini inawezekana kabisa kuwadhibiti "magaidi" kwa kipigo.
 
sawa Malawi wapige bomu pale Mbeya liuwe watu zaidi ya 2000. Then simple tu tuseme let it go.
Sasa kile kijiji kilichovamiwa ni ardhi ya palestina.... yaani kuna kitu kinaitwa WALOWEZI nenda kagoogle. Hawa ni raia wa Israel wanaovamia makazi ya wapalestina bila idhini ya serikali ya Israel. Mfano kule Westbank kuna walowezi laki 5 in fact hata zipo cases mfano 2004 ambapo serikali ya Israel ilienda kuwaondoa hao walowezi huko Gaza!! Sasa hao hawana tofauti na Idd Amin alivyoikalia Kagera au Wakoloni kuikalia Tanzania ni lazima uwaondoe. Kwahiyo case ya Malawi haina mfanano na ukoloni ambao ndio upo Israel.
Tunaongelea maisha ya watu. Halafu case study ya ANC na wazungu, Maumau na wazungu huwezi ukazirelate na kinachoendelea mashariki ya kati.
Zina relate maana wasauzi walikaliwa kimabavu na Boers, same to Israel kukalia kimabavu Palestine. Violence iliisha pale tu walipokubali kutoa uhuru, ila kudhani vita itaisha kwa kurusha mabomu ni kujidanganya. Subiri tu mwakani utasikia Hamas imeanza upya!! In fact mayatima wote waliobaki watarevenge vifo vya wazazi wao.
 
Hakuna mtu anawabagua wapalestina Israel
Hii sentensi yako pekee ina shida, kitendo tu cha nchi ya palestina kuitwa Israel ina sum up hoja yangu!! Kule westbank hata huwezi toka mji mmoja kwenda mwingine mpaka upate kibali mind you unaweza ondolewa kwenye ardhi yako bila fidia na hao walowezi!!

Hivi unajua umeme na maji viko regulated na Tel Aviv mpka misaada ya chakula ni Tel Aviv ndio wana maamuzi ya mwisho? Unasemaje wanaishi kwa uhuru?

Unasemaje hakuna ubaguzi?
 
Tatizo la Gaza ni Iran Iran ikitwangwa barabara tatizo la Gaza litaisha sababu Iran ndie kajaza Wapiganaji siasa kali Gaza na ndio mfadhili wao
We kumbe ndio hujui, Hamas ilianzishwa na Israel kwa minajili ya kubalance power huko Palestina na kumneutralize Arafat na baadae Abbas ni vile tu wakaja kugeukana. Hata hayo mahandaki ya Gaza yalijengwa na Israel.
https://www.timesofisrael.com/for-years-netanyahu-propped-up-hamas-now-its-blown-up-in-our-faces/

Siasa za divide and rule zipo miaka yote sasa Iran inaingiaje kwenye project ya Israel?

Hii link ni maneno ya Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ehud barak akikiri walijenga mahandaki huko Gaza!!
 
Tunazungumzia iwapo ideology inaweza kuuliwa kwa mabavu. Ukommunist nao ni ideology. Huko America Kusini imekomeshwa kwa kipigo. Kama propaganda juu ya uzuri wa ubepari imeshinda basi leo NK na Cuba zisingekuwa za kicommunisti.
At one time theluthi ya dunia nzima walikuwa one way or another of communist country je ni nani aliwapiga hao kwa mabavu; At one time about one-third of the world's population lived under communist governments, most notably in the republics of the Soviet Union. Today communism is the official form of government in only five countries: China, North Korea, Laos, Cuba, and Vietnam. However, none of these meet the true definition of communism.

Ni Kwamba Communism is the system of social organization it either works or don't work and at the time it was not working while the other form capitalism was seen to be working obviously kutakuwa na struggle from within kuondokana na hio system just like capitalism as we know it will fail with the rise of automation and technology (no more trickle down and creation of labor); So naturally it failed
ANC nao waliitwa magaidi lakini walikuwa na ideology yao. Njia pekee ya kumaliza migogoro ya binadamu ni kipigo mpaka mmoja akae kwa kutulia.
ANC walikuwa wanagombania kuachana na Ubaguzi wa Rangi na sio wao tu dunia nzima iliwaunga mkono na mpaka leo hii makaburu wasingebadilika wangeelenda kushutumiwa kwahio kama makaburu wangeendelea kutumia mabavu mpaka leo hii SA would not be safer for anyone...
Wajerumani walimpa kichapo Abushiri na kumnyonga. Nchi ikatulia. Waliwapa kichapo wazee wa majimaji nchi ikakaa sawa na wakarudi kulima pamba.
Moja nyakati zile Africa was there to be divided among the big nations it was the order of the day kama vile utumwa ulikuwa the order of the day..., na wala hakuna kumalizika ni kwamba ukiwazima leo kesho watanyanyuka the struggle continues ndio struggle ilivyoendelea huko HAITI na ndio Struggle ilivyoendelea huko INDIA na kina Gandhi until the colonialists could not handle it anymore
Hakuna ideology inayoweza kusimama mbele ya kichapo kisichokoma. Hakuna ideology inayoweza kusimama mbele ya jeshi lililotayari kuangamiza mpaka mtu wa mwisho.

Ni vile kwa sasa kelele ni nyingi, lakini inawezekana kabisa kuwadhibiti "magaidi" kwa kipigo.
Moja ugaidi ni nini ? Na mbili unampiga vipi enemy asiyeonekana..., Kumbuka mtu anayegombania Himaya yake, au his state of being has nothing to loose na sababu kitu kinachosimama ni idea fulani; Idea hii inapingwa kwa hoja na kuonyesha kwamba haifai.., narudia tena leo hii ndugu yako au mtoto wake anaweza akavaa Bomu na kwenda kuangamiza watu fulani sababu tu na wao anaona wanamkandamiza (sasa kwa Israel kuendelea kuangamiza civilians ni kwamba wanazalisha watu ambao watatumia kila mbinu ya kupambana hata kupoteza kwao maisha)

The only way to win a war of ideas is to KILL that Idea, not the people with ideas because by killing them you make them martyrs
 
At one time theluthi ya dunia nzima walikuwa one way or another of communist country je ni nani aliwapiga hao kwa mabavu; At one time about one-third of the world's population lived under communist governments, most notably in the republics of the Soviet Union. Today communism is the official form of government in only five countries: China, North Korea, Laos, Cuba, and Vietnam. However, none of these meet the true definition of communism.

Ni Kwamba Communism is the system of social organization it either works or don't work and at the time it was not working while the other form capitalism was seen to be working obviously kutakuwa na struggle from within kuondokana na hio system just like capitalism as we know it will fail with the rise of automation and technology (no more trickle down and creation of labor); So naturally it failed

ANC walikuwa wanagombania kuachana na Ubaguzi wa Rangi na sio wao tu dunia nzima iliwaunga mkono na mpaka leo hii makaburu wasingebadilika wangeelenda kushutumiwa kwahio kama makaburu wangeendelea kutumia mabavu mpaka leo hii SA would not be safer for anyone...

Moja nyakati zile Africa was there to be divided among the big nations it was the order of the day kama vile utumwa ulikuwa the order of the day..., na wala hakuna kumalizika ni kwamba ukiwazima leo kesho watanyanyuka the struggle continues ndio struggle ilivyoendelea huko HAITI na ndio Struggle ilivyoendelea huko INDIA na kina Gandhi until the colonialists could not handle it anymore

Moja ugaidi ni nini ? Na mbili unampiga vipi enemy asiyeonekana..., Kumbuka mtu anayegombania Himaya yake, au his state of being has nothing to loose na sababu kitu kinachosimama ni idea fulani; Idea hii inapingwa kwa hoja na kuonyesha kwamba haifai.., narudia tena leo hii ndugu yako au mtoto wake anaweza akavaa Bomu na kwenda kuangamiza watu fulani sababu tu na wao anaona wanamkandamiza (sasa kwa Israel kuendelea kuangamiza civilians ni kwamba wanazalisha watu ambao watatumia kila mbinu ya kupambana hata kupoteza kwao maisha)

The only way to win a war of ideas is to KILL that Idea, not the people with ideas because by killing them you make them martyrs
Unafikiri "magaidi" wa MKIRU wangeweza kushindwa kwa maneno matupu? Unafikiri nchi zinaposema haziwezi kukaa meza moja na magaidi hazina akili?

Ideology ya ukommunist haijashindwa kwa hoja. Nchi kama Cuba imepigwa kwa vikwazo vikali, Vietnam na Korea vita kali ilipigwa. Unafikiri vita baridi ilikuwa baridi kweli? Vita vilikuwa vikipiganwa kila mahali, vya silaha na fitna. CIA, WB, IMF wote walikuwa vitani. Ideology ya ukomunisti haikushindwa kwa propaganda. Hata ndani ya Marekani yenyewe kulikuwa na Red Scare, wakomunisti waliwindwa kama adui wa taifa.

Utumwa wenyewe haukuisha kwa maneno matupu. US ilipigana vita kali ya wenyewe kwa wenyewe ndipo utumwa ukakoma. UK alipita bahari zote kukamata meli za watumwa ndipo ukakoma. Haukukoma sababu Watu walikaa wakaaminishwa kuwa utumwa ni ukosefu wa ubinadamu, kipigo ndicho kilikomesha.

Ngoja nikupe mfano jinsi nchi zinavyodeal na wajitoa mhanga. Kuna wa Uighurs walifanya ugaidi China kwa kuchoma watu visu. China ikaenda huko kwenye chimbuko lao Xinjiang, kamata wote wenye muelekeo wa uasi na kuwaweka kwenye makambi. Ikajaza wahan ili kuwaneutralize wauighurs, na hdi leo jimbo hilo linafanyiwa survuilence ya kufa mtu. Ndizo nchi zote zinavyodeal na wajitoa mhanga ambao hawajali hata wakifa, zinaenda kwenye chimbuko walikotokea, kama ni Afghanstan, Chechnya, Gaza, Iraq, Sudan, Congo, Townships walikojificha "Magaidi" wa ANC nk nk.

Usifikiri nchi zinazoamua kupambana na "Ugaidi" na ideologies zao kwa violence hazina akili. Hiyo ndiyo lugha pekee inayoeleweka kwao.
 
Unafikiri "magaidi" wa MKIRU wangeweza kushindwa kwa maneno matupu? Unafikiri nchi zinaposema haziwezi kukaa meza moja na magaidi hazina akili?
Nani kasema mkae meza moja ?; na ugaidi ni nini ? Sababu magaidi wenyewe ambao wanajifanya kuongelea magaidi wengine nao pia ni magaidi...
Ideology ya ukommunist haijashindwa kwa hoja. Nchi kama Cuba imepigwa kwa vikwazo vikali, Vietnam na Korea vita kali ilipigwa. Unafikiri vita baridi ilikuwa baridi kweli? Vita vilikuwa vikipiganwa kila mahali, vya silaha na fitna. CIA, WB, IMF wote walikuwa vitani. Ideology ya ukomunisti haikushindwa kwa propaganda. Hata ndani ya Marekani yenyewe kulikuwa na Red Scare, wakomunisti waliwindwa kama adui wa taifa.
Kwamba kulikuwa kuna law ya kuwa a communist au kulikuwa na sheria ya kujaribu ku overthrow the government ? Kumbuka there is a difference wewe ukiwa nchi ya Kikomusti kipindi hicho uanze kuongea mambo ya kipebari na kukusanya watu wenye mlengo kama huo hio itakuwa ni tafsiri ya ku overthrow the government
Utumwa wenyewe haukuisha kwa maneno matupu. US ilipigana vita kali ya wenyewe kwa wenyewe ndipo utumwa ukakoma.
Kwahio utumwa ulikuwepo USA peke yake ? USA walipigana vita ya North and South sababu kuna walioamini waendelee kumiliki watumwa na wengine waliamini abolish ya watumwa kwahivyo it was two masters with different wants..., na hata baada ya North and South kupatana abolishment ya Utumwa haikuwa instantly-Emancipation Proclamation haikufuatwa na Confederates ambao wao walijiona sio part ya Sheria za States; Two years after na 13th Amendment bado Utumwa uliendelea kama kawaida..., The thing which practically ended slave trade kwa hatua kubwa worldwide ni Industrial Revolution as Nguvu kazi haikuhitajika kama mwanzo bali; bali kuondokana na ile superiority kwamba baadhi ya watu ni watwana na wengine mabwana iliendelea kwa muda mrefu sana
UK alipita bahari zote kukamata meli za watumwa ndipo ukakoma. Haukukoma sababu Watu walikaa wakaaminishwa kuwa utumwa ni ukosefu wa ubinadamu, kipigo ndicho kilikomesha.
Na hao UK kwanini waliacha biashara hii ? Ghafla waliingiwa na Utukufu ? Au kulikuwa hakuna umuhimu na kuwepo kwa Sheria ya kupinga biashara ya utumwa ndio maana mtu aliyejihusisha na hii biashara akawa mtuhumiwa ? UK mwenyewe Colonialism ilimshinda and she could no longer sustain the empire
Ngoja nikupe mfano jinsi nchi zinavyodeal na wajitoa mhanga. Kuna wa Uighurs walifanya ugaidi China kwa kuchoma watu visu. China ikaenda huko kwenye chimbuko lao Xinjiang, kamata wote wenye muelekeo wa uasi na kuwaweka kwenye makambi. Ikajaza wahan ili kuwaneutralize wauighurs, na hdi leo jimbo hilo linafanyiwa survuilence ya kufa mtu. Ndizo nchi zote zinavyodeal na wajitoa mhanga ambao hawajali hata wakifa, zinaenda kwenye chimbuko walikotokea, kama ni Afghanstan, Chechnya, Gaza, Iraq, Sudan, Congo, Townships walikojificha "Magaidi" wa ANC nk nk.

Usifikiri nchi zinazoamua kupambana na "Ugaidi" na ideologies zao kwa violence hazina akili. Hiyo ndiyo lugha pekee inayoeleweka kwao.
Kwahio wale magaidi waliopiga mabomu Ubalozi wa USA Tanzania na Kenya walikuwa watoto au ndugu wa Osama ? Au walishakutana na Osama au ni ile Sympathy kwa kuona kwamba USA anaharibu / nyanyasa hence kupoteza maisha yake yeye ni bora kuliko kuendelea na minyanyaso...

Waigereza waliwauwa sana Kenya kwenye MauMau lakini haikuwa kuwamaliza ni kwamba wangekuwepo mpaka leo wanawakandamiza nisingeshangaa wajukuu wa hao MAUMAU leo wakafanya revenge kwa Muingereza yoyote...

Narudia tena kama watu wanaona wanaonewa kwa mabavu kuongeza mabavu ni ujuha..., inabidi hata kama ni mabavu yatumike indirectly na kwa chinichini kutumia mabavu na kutunisha misuli ni kuongeza fodder ya recruitment....
 
Back
Top Bottom