Je anachofanya Israel kinakuza au kuondoa Ugaidi ?

Binafsi nachokiamini vita vya ideologia kamwe huwezi kushinda kwa Mabavu.., Hususan watu ambao wanaona kwamba wanaonewa na kunyanyaswa, kuwaondoa kwa mabavu na kuwauwa tena kwa waziwazi kunakoonekana kila kona, ni kwamba unawapa njia rahisi maghaidi wa kesho au maghaidi wa leo kuweza kufanya recruitment zaidi.

Binafsi nilikuwa naitetea sana Israel kwa kipindi kirefu ambapo kulikuwa na Anti-Semitism kila kona na jinsi Hitler alivyowanyanyasa na kuwafanya hawa watu kama sio binadamu...

Ingawa leo hii anachofanya sidhani kama kina manufaa yoyote kwa mustakabali na amani ya dunia ya leo na kesho sababu anazidi kuwatengeneza magaidi..

Ushauri
United Nations ipate meno na iwe na nguvu sawa bila VETO ya taifa lolote na nchi zote ziwe wanachama, ili kama kuna mtu / taifa litaleta za kuleta tuweze kudeal nalo kama dunia kwa pamoja.., kwa kufanya hivi kutakuwa hakuna uwezekano wa watu kuona kwamba wanaonewa, hivyo kuondoa ile fodder (Chakula) ambacho Fundamentalists wanaitumia kuwarubuni (brainwash) watu ili kujiunga nao...

“Justice must not only be done, but it must also be seen to be done.”​
Kwahiyo unazani kwani waisrael hawauliwi nawo wanakufa sana ila kisasi kinapunguza machungu kwahiyo waache wachapane kadli Wana yochapana na ww unaishi vzuri ila kama na ww ni mlevi au mlafi wa dini unatakiwa uchapwe tu
 
Kwahio kwa akili yako unadhani ugaidi unatokana na Dini na Israel na Palestine ni sababu ya Dini ?, Kwamba Ukiwa dini moja au nyingine basi unakuwa rafiki (Yaani its about converting people)?
 
Nani kasema mkae meza moja ?; na ugaidi ni nini ? Sababu magaidi wenyewe ambao wanajifanya kuongelea magaidi wengine nao pia ni magaidi...

Kwamba kulikuwa kuna law ya kuwa a communist au kulikuwa na sheria ya kujaribu ku overthrow the government ? Kumbuka there is a difference wewe ukiwa nchi ya Kikomusti kipindi hicho uanze kuongea mambo ya kipebari na kukusanya watu wenye mlengo kama huo hio itakuwa ni tafsiri ya ku overthrow the government

Kwahio utumwa ulikuwepo USA peke yake ? USA walipigana vita ya North and South sababu kuna walioamini waendelee kumiliki watumwa na wengine waliamini abolish ya watumwa kwahivyo it was two masters with different wants..., na hata baada ya North and South kupatana abolishment ya Utumwa haikuwa instantly-Emancipation Proclamation haikufuatwa na Confederates ambao wao walijiona sio part ya Sheria za States; Two years after na 13th Amendment bado Utumwa uliendelea kama kawaida..., The thing which practically ended slave trade kwa hatua kubwa worldwide ni Industrial Revolution as Nguvu kazi haikuhitajika kama mwanzo bali; bali kuondokana na ile superiority kwamba baadhi ya watu ni watwana na wengine mabwana iliendelea kwa muda mrefu sana

Na hao UK kwanini waliacha biashara hii ? Ghafla waliingiwa na Utukufu ? Au kulikuwa hakuna umuhimu na kuwepo kwa Sheria ya kupinga biashara ya utumwa ndio maana mtu aliyejihusisha na hii biashara akawa mtuhumiwa ? UK mwenyewe Colonialism ilimshinda and she could no longer sustain the empire

Kwahio wale magaidi waliopiga mabomu Ubalozi wa USA Tanzania na Kenya walikuwa watoto au ndugu wa Osama ? Au walishakutana na Osama au ni ile Sympathy kwa kuona kwamba USA anaharibu / nyanyasa hence kupoteza maisha yake yeye ni bora kuliko kuendelea na minyanyaso...

Waigereza waliwauwa sana Kenya kwenye MauMau lakini haikuwa kuwamaliza ni kwamba wangekuwepo mpaka leo wanawakandamiza nisingeshangaa wajukuu wa hao MAUMAU leo wakafanya revenge kwa Muingereza yoyote...

Narudia tena kama watu wanaona wanaonewa kwa mabavu kuongeza mabavu ni ujuha..., inabidi hata kama ni mabavu yatumike indirectly na kwa chinichini kutumia mabavu na kutunisha misuli ni kuongeza fodder ya recruitment....
Tangazo la ukombozi lilitolewa 1963 na vita iliendelea hadi 1965 so inaingia akilini kwa nini utumwa uliendelea miaka miwili baada ya kutangazwa kwa tangazo hilo. Mpaka wamiliki watumwa waliposhindwa kwa kipigo ndipo utumwa ulipokoma.

Hao magaidi wa ubalozini ilipigwa Al Qaeda na Afghanstan. Yaani walikotoka. Usiogope kuzaliwa "magaidi" wengine, usidhani ukiwapa wanachotaka ndiyo wataacha ugaidi wao au ndiyo utakuwa na amani. We wapige kadri unavyoweza, wakizaliwa wengine wapige vikali vile vile. Siku ukichoka kama ambavyo wakoloni walichoka basi unawapa wanachotaka. Kama unaona kuwapa wanachotaka kutakuumiza basi endelea kujiongezea nguvu na kuwapiga vikali.

Suala la kuonewa ni subjective hivyo haliwezi kusuluhishwa kwa mdahalo. Ni kupigana, anaeshindwa anatulia. Akiinuka anapigwa tena, mpaka siku moja akiwa na nguvu ya kushinda. Hii ndiyo lugha ambayo binadamu anaielewa toka kuumbwa kwa dunia. Hayo mambo ya majadiliano ni nyongeza tu.
 
And that is what and why Slavery ended in the World ?

Waliopiga ubalozi wa Kenya na Tanzania walikuwa watu wa Afghanistan ? Na aliyekwambia USA ameondoka Afghanistan baada ya kumaliza kazi ni nani ? Au aliondoka baada ya anachofanya wala alikuchokuwa anafanya watu kuona hakina tija..., na it can be argued kwa kuondoa Al Qaeda ndio kulizasiaha ISIS an even worse entity

Kuonewa ni Subjective ?
 
Binafsi nachokiamini vita vya ideologia kamwe huwezi kushinda kwa Mabavu.., Hususan watu ambao wanaona kwamba wanaonewa na kunyanyaswa, kuwaondoa kwa mabavu na kuwauwa tena kwa waziwazi kunakoonekana kila kona, ni kwamba unawapa njia rahisi maghaidi wa kesho au maghaidi wa leo kuweza kufanya recruitment zaidi.

Binafsi nilikuwa naitetea sana Israel kwa kipindi kirefu ambapo kulikuwa na Anti-Semitism kila kona na jinsi Hitler alivyowanyanyasa na kuwafanya hawa watu kama sio binadamu...

Ingawa leo hii anachofanya sidhani kama kina manufaa yoyote kwa mustakabali na amani ya dunia ya leo na kesho sababu anazidi kuwatengeneza magaidi..

Ushauri
United Nations ipate meno na iwe na nguvu sawa bila VETO ya taifa lolote na nchi zote ziwe wanachama, ili kama kuna mtu / taifa litaleta za kuleta tuweze kudeal nalo kama dunia kwa pamoja.., kwa kufanya hivi kutakuwa hakuna uwezekano wa watu kuona kwamba wanaonewa, hivyo kuondoa ile fodder (Chakula) ambacho Fundamentalists wanaitumia kuwarubuni (brainwash) watu ili kujiunga nao...

“Justice must not only be done, but it must also be seen to be done.”​
Israel anashambuliwa nanmagaidi ya kiislamkila kukicha nanyeye kama alivyosema ananhaki ya kujilinda.Hezbollah karusha zaidi ya makombora 50,000 kutafuta sababu ya vita.Vita kapelekewa mnaanza kulialia.
Israel yuko sahihi kabisa.Magaidi yaache kukaa nyuma ya raia.
 
Ni nini chanzo au muendelezo wa hivi Vita vya Palestina na Israel sababu kama ni mfuatiliaji havijaanza leo wala jana..., na kama nilivyosema hapo juu kwa mabavu wala havitamalizwa ni kuweka pause...
 
And that is what and why Slavery ended in the World ?

Waliopiga ubalozi wa Kenya na Tanzania walikuwa watu wa Afghanistan ? Na aliyekwambia USA ameondoka Afghanistan baada ya kumaliza kazi ni nani ? Au aliondoka baada ya anachofanya wala alikuchokuwa anafanya watu kuona hakina tija..., na it can be argued kwa kuondoa Al Qaeda ndio kulizasiaha ISIS an even worse entity

Kuonewa ni Subjective ?
Kuhusu utumwa, haukuisha kwa watu kukaa mezani na kuona kuwa "Utumwa ni mbaya jamani, tuuache. " Nguvu ndiyo ilipunguza utumwa duniani maana kuna nchi kama Mauritania bado upo. Sababu ya kukomesha utumwa ni kitu kingine, lakini kilichokomesha ni nguvu.

ISIS nao wanapigwa, na watakaokuja baada yao nao wanapigwa vilevile. Ndiyo njia pekee ya kudeal na "Ugaidi"

Ndiyo. Mfano Wapalestina wanaona wanaonewa lakini Waisraeli wanaona hawamuonei mtu bali wana haki. Makaburu waliona wana haki wakati watu weusi waliona wanaonewa. Masetla wa Kenya waliona wana haki zote wakati watu wa Mau Mau waliona kuwa wanaonewa na kudhulumiwa. Hata wamiliki watumwa waliona kuwa wana haki ya kumiliki watumwa. Kwenye mazingira kama hayo huwezi kupata suluhu zaidi ya kupigana.
 
Utumwa at large scale ulikwisha sababu it was no longer fit for purpose Industrial Revolution was among those things na utumwa ungeendelea mpaka leo watu wangekuwa wanariot sababu ile cause / sababu ya wao kuriot bado ipo basi wangeendelea mpaka kesho.., na ingekuwa ni vita basi kwanini usingeisha baada ya vita vya kwanza kutokea...

Na hao unaosema wanawapiga si wameondoka huko kote Afghanistan, Iraq na hata Libya na wameondoka kwa kuacha things worse than they were before

Kwahio sababu mwizi au mbakaji yeye anajiona yupo sawa kubaka au slave trader au mmiliki wa Mtumwa sababu yeye anaona ni sawa kwake kufanya hivyo basi it makes it okay ? Is that your definition ? Do you know anything about natural justice ?
 
Haijalishi sababu iliyofanya watu watake kukomeshwa utumwa lakini ukweli ni kuwa ulikomeshwa kwa nguvu. Bila nguvu na kipigo usingekoma. Ndiyo maana nchi kama Mauritania hadi leo upo, hadi nguvu itakapotumika ndiyo utakoma.

Wakiacha Afghan worse kuliko walivyoikuta wao haiwahusu, wametimiza lengo lao la kupiga maficho ya "Magaidi."

Kuwa sawa au kutokuwa sawa kunaamuliwa na nyakati tu, si kwamba ni jambo lisilobadilika. Zamani utumwa ulikuwa sawa leo tunaona siyo sawa, si ajabu huko mbele ukawa sawa tena. Kuna jamii ubakaji siyo kosa na mbakwaji ndiye anashutumiwa. Kuna jamii kula watu wengine ilikuwa ni sawa kabisa. definition ya kilicho sawa na kisicho sawa inabadilika kila siku.
 
Haijalishi sababu iliyofanya watu watake kukomeshwa utumwa lakini ukweli ni kuwa ulikomeshwa kwa nguvu. Bila nguvu na kipigo usingekoma. Ndiyo maana nchi kama Mauritania hadi leo upo, hadi nguvu itakapotumika ndiyo utakoma.
Kwanza kabisa hapa naona tunaendelea kutoka nje ya point polepole mpaka sasa tumefika in the middle of nowhere.., Moja katika utumwa nani ni oppressor na nani ni oppressed ? Kwa muktadha huo ni kwamba Utumwa ungekuwepo mpaka leo wale watu oppressed hata wangepigwa kiasi gani ni kama magugu bila kuyangoa na kuondoa mizizi wangeendelea ku riot mpaka kesho kutwa..., na kama jinsi yao ya ku riot ni kwa kufanya mashambulizi kwa civilians (terrorization) basi wataendelea kufanya hivyo mpaka hio oppression
Wakiacha Afghan worse kuliko walivyoikuta wao haiwahusu, wametimiza lengo lao la kupiga maficho ya "Magaidi."
Kupiga maficho ya magaidi wakati kwa kufanya kwao hivyo kulizidisha ugaidi (kuna picha zilikuwa zinasambaa ambapo walikuwa wanadhalilisha watu) hizo picha ndio zilitumika kusajiri wengine..., na unaongelea maficho ya magaidi waliolipua Dar na Nairobi walikuwa wamejificha wapi ? Au Dar nayo ni maficho kwahio tupapige mabomu ?
Kuwa sawa au kutokuwa sawa kunaamuliwa na nyakati tu, si kwamba ni jambo lisilobadilika. Zamani utumwa ulikuwa sawa leo tunaona siyo sawa, si ajabu huko mbele ukawa sawa tena. Kuna jamii ubakaji siyo kosa na mbakwaji ndiye
Biashara ya utumwa haijawahi kuwa sawa no matter katika nyakati hizo kuweza kufanya justification lakini hio haikuwa sawa. Bali waliamua kujiridhisha kwamba wengine ni inferior na wengine superior ila huwezi kusema ilikuwa sawa kwa yule ambaye alikuwa oppressed
anashutumiwa. Kuna jamii kula watu wengine ilikuwa ni sawa kabisa. definition ya kilicho sawa na kisicho sawa inabadilika kila siku.
Kwahio sababu watu waliendekeza tabia za ajabu za kuwa oppress wengine ilikuwa sawa kwa wale ambao wanaliwa..., yaani hapa siongelei walaji naongelea wanaoliwa..., na kama wangeendelea kuliwa mpaka leo unadhani wasinge react by any means necessarly and one that means being terrorizing the oppressors ?

Kwahio narudia tena kumaliza hiki kitu ni kuondoa injustices au kuonyesha so called injustices they are not injustices... hilo likieleweka unaondoa fodder ya recruitment
 
Yaani israel ndio taifa pekee linalochangia na magaidi wa mataifa 7 ili wamfute halafu anaitwa mchokozi?
Usilo lijua ni kwamba Israel ni msukule wa Marekani na uingereza Ili kuchafua amani mashariki ya kati Kwa maslahi ya Marekani na uingereza

Vita vya Gaza ni vita vya kisiasa na udini Marekani na uingereza wanaona Palestine wakipewa uhuru wao na kuwa nchi huru uislam utastawi vizuri Palestine hatimaye hizotoria ya dini zao za uongo walizozianzisha zitazidi kupotea

Vita ya Lebanon ni vita ya kiuchumi Lebanon ipo eneo muhimu ambalo ndio njia anayoitegrmea Marekani kuenda kuiba Mafuta

Haya yote Ili yafanikiwe ndio wanamtumia msukule wao Israel na ndio maana wanamsapoti Kwa Kila kitu

Netanyau hana tofauti na Zeresk wamekubali nchi zao ziwe uwanja wa vita Kwa manufaa ya Marekani
 
Kwanza kabisa hapa naona tunaendelea kutoka nje ya point polepole mpaka sasa tumefika in the middle of nowhere.., Moja katika utumwa nani ni oppressor na nani ni oppressed ? Kwa muktadha huo ni kwamba Utumwa ungekuwepo mpaka leo wale watu oppressed hata wangepigwa kiasi gani ni kama magugu bila kuyangoa na kuondoa mizizi wangeendelea ku riot mpaka kesho kutwa..., na kama jinsi yao ya ku riot ni kwa kufanya mashambulizi kwa civilians (terrorization) basi wataendelea kufanya hivyo mpaka hio oppression

Kupiga maficho ya magaidi wakati kwa kufanya kwao hivyo kulizidisha ugaidi (kuna picha zilikuwa zinasambaa ambapo walikuwa wanadhalilisha watu) hizo picha ndio zilitumika kusajiri wengine..., na unaongelea maficho ya magaidi waliolipua Dar na Nairobi walikuwa wamejificha wapi ? Au Dar nayo ni maficho kwahio tupapige mabomu ?

Biashara ya utumwa haijawahi kuwa sawa no matter katika nyakati hizo kuweza kufanya justification lakini hio haikuwa sawa. Bali waliamua kujiridhisha kwamba wengine ni inferior na wengine superior ila huwezi kusema ilikuwa sawa kwa yule ambaye alikuwa oppressed

Kwahio sababu watu waliendekeza tabia za ajabu za kuwa oppress wengine ilikuwa sawa kwa wale ambao wanaliwa..., yaani hapa siongelei walaji naongelea wanaoliwa..., na kama wangeendelea kuliwa mpaka leo unadhani wasinge react by any means necessarly and one that means being terrorizing the oppressors ?

Kwahio narudia tena kumaliza hiki kitu ni kuondoa injustices au kuonyesha so called injustices they are not injustices... hilo likieleweka unaondoa fodder ya recruitment
Achana na habari za huyu mwema na huyu siyo mwema. Angalia practicality. Ugaidi unaweza kudhibitiwa kwa kipigo na mabavu, au kufanya hivyo kunaukuza?

Kwanza. Usifikiri watumwa wa Marekani hawakuwahi kupigania uhuru wao kabla ya 1865. Walipigana tena walikuwa "magaidi" hasa. Kuna watu walichinja familia nzima iliyokuwa inawamiliki na kutoroka. Walichinja hadi watoto wasio na "Hatia." Ni kama tu Hamas mwaka jana walivyoua watu wasio na "Hatia" ili kupinga ukoloni wa Israel.

Mapambano ya watumwa na ya watu kama Hamas au ANC yanafanana kuliko unavyodhani, na wote walitumia mbinu za kigaidi. Sasa ni mbinu gani zilitumika/zinatumika kuwadhibiti wote? Wote walidhibitiwa kwa mkono wa chuma na njia hii ilifaulu vizuri tu japo wewe unasema inazalisha magaidi zaidi. Wale watumwa waliofanya ugaidi wa kuchinja familia inayowamiliki walisakwa, wakakamatwa na kuuawa kinyama. Wala usidhani ugaidi wa Umkoto wa Sizwe ndiyo uliwaletea wasouth uhuru. Ugaidi wao ulidhibitiwa vilivyo.

Hitimisho langu: Njia bora ya kudhibiti na kuondoa ugaidi ni kuwalipa kadri ya matendo yao. Anachofanya Israel kinaondoa ugaidi wala hakiukuzi. Mtu hakatazwi kuwa na ideology anayotaka, lakini matendo yake yanayochochewa na hiyo ideology yanaweza kudhibitiwa kwa nguvu.
 
Kama mabavu hayo ndio causative ya ugaidi unadhani kuendelea na mabavu kutamaliza hicho kitu... Jambo ambalo unashindwa kuelewa hapa its a battle of ideas with concrete evidence or not (na kama kuna concrete evidence kwamba kuna kunyanyasa the only thing itakayomaliza hio belief kwamba tunanyanyaswa ni either kuacha kunyanyaswa au kuonyesha kwamba the so called thing you call unyanyasaji sio unyanyasaji)
Kwanza. Usifikiri watumwa wa Marekani hawakuwahi kupigania uhuru wao kabla ya 1865. Walipigana tena walikuwa "magaidi" hasa. Kuna watu walichinja familia nzima iliyokuwa inawamiliki na kutoroka. Walichinja hadi watoto wasio na "Hatia." Ni kama tu Hamas mwaka jana walivyoua watu wasio na "Hatia" ili kupinga ukoloni wa Israel.
Kwahio utumwa ungekuwepo leo at that scale wasingechinja watu ? Au kuondokana na huo utumwa kumemaliza the need for the to protest ?
Mapambano ya watumwa na ya watu kama Hamas au ANC yanafanana kuliko unavyodhani, na wote walitumia mbinu za kigaidi. Sasa ni mbinu gani zilitumika/zinatumika kuwadhibiti wote? Wote walidhibitiwa kwa mkono wa chuma na njia hii ilifaulu vizuri tu japo wewe unasema inazalisha magaidi zaidi. Wale watumwa waliofanya ugaidi wa kuchinja familia inayowamiliki walisakwa, wakakamatwa na kuuawa kinyama. Wala usidhani ugaidi wa Umkoto wa Sizwe ndiyo uliwaletea wasouth uhuru. Ugaidi wao ulidhibitiwa vilivyo.
Kwahio walivyodhibiti wa kwanza waliacha au walijipanga na kurudi tena baada ya muda, na mara nyingine hata kuruka generations kwamba wale waliobagua babu zetu na kuwabaka ndio hawa wanatubaka leo ? Kwamba Apartheid ingekuwepo mpaka leo watu wa South wangenyoosha mikono sababu babu zao walidhibitiwa kwa mabavu ? Kilichoondoa Protest ya wa SA na hao watumwa ni kuondoa causavative iliyowafanya wafanya hayo in the first place...
Hitimisho langu: Njia bora ya kudhibiti na kuondoa ugaidi ni kuwalipa kadri ya matendo yao. Anachofanya Israel kinaondoa ugaidi wala hakiukuzi. Mtu hakatazwi kuwa na ideology anayotaka, lakini matendo yake yanayochochewa na hiyo ideology yanaweza kudhibitiwa kwa nguvu.
Huwezi ukawa na beliefs ambazo ni kero na detrimental kwa wenzako au watu wa aina fulani alafu ukategemea wataacha kureact sababu eti unaweza kuwapiga..., Kwanza kabisa kuwapiga huwezi sababu huenda ulinao kwenye himaya yako potentially wanaweza wakakugeuka sababu unachofanya is Terrorism (hurting and terrorizing innocent civilians)
 
Na huwezi kuwa na beliefs au ideologies ambazo ni kero kwa wenzako halafu ukategemea wataacha kukupiga sababu kufanya hivyo kutazidi kukuza hizo beliefs. Ipo hivi, magaidi siyo kwamba wanafanya ugaidi wao sababu ya kunyanyaswa na kuonewa. Achana na habari ya kunyanyaswa na kuonewa. "Magaidi" wengine wao ndiyo wananyanyasa na kuonea watu. Kama Boko Haram. Wao wanaimani kwamba elimu ya magharibi ni haram na wanatumia violence kuiondoa. Serikali ya Nigeria iogope kuwapa kipigo kwa kuogopa kuwa ideology yao itazidi kukua?

Basi ipo hivyo duniani kote. Gaidi anaona anaonewa hivyo anachofanya ni kujilinda, na yule anayepambana na ugaidi anaona anaonewa na anchofanya ni kujilinda. Hebu niambie, unapambana vipi na mtu anayetumia violence?
 
Ushasema magaidi wengine na ndio hapo nikasema ni chizi pekee ambaye atakubaliana na hizo itikadi na fundamentalism na ndio hapo kila siku kuanzia watu wa Imani zote na wenye Busara wanakemea hao Boko Haramu na in short ni waharifu ambao wanahitaji kudhibitiwa.., sasa tunawadhibiti vipi..., kwa kupiga mabomu sehemu zote na mitaa yote bila kujali casualities ?

Sababu beliefs zao ni za kipuuzi na ambazo zinatesa wengine ni zaidi ya mabavu yanayotumika ndio hivyo hivyo kama watu walivyokemea Apartheid SA, na kila Mwenye Busara mpaka UN sasa hivi wanavyokemea anachofanya Israel...

Ndio hapo nimekwambia kuna natural justice which is not subjective.., everyone should be treated fairly na ndio maana nikasema tangia mwanzo UN iwe na meno na kila nchi awe mwanachama na awe na kura sawa bila VETO ili nchi yoyote wakileta za kuleta waweze kudhibitiwa kwa umoja (fairly)
 
Tunarudi nyuma. Nimeishakwambia definition ya kilicho sawa na kisicho sawa inabadilika kila leo. Pia inategemea mtendewa na mtendewaji. Zamani utumwa ulikuwa sawa na unakubalika. Leo ni kosa. Israel wanaona wana haki ya kukaa pale, Hamas na wapalestina wanaona wameporwa nchi. Natural Law na Natural Justice vyote vimekuwa vikibadilika badilika kwenye historia ya binadamu. Wala usifikiri wakati tuliopo ndiyo kilele cha haki.

Unataka UN yenye watu wenye mitazamo tofauti juu ya kilicho sawa na kisicho sawa waje pamoja kumuadhibu "Mkosefu?"
 
Tunarudi nyuma. Nimeishakwambia definition ya kilicho sawa na kisicho sawa inabadilika kila leo. Pia inategemea mtendewa na mtendewaji. Zamani utumwa ulikuwa sawa na unakubalika. Leo ni kosa.
Tofautisha Sawa, Haki na Sheria..., Utumwa ulikuwa order of the day Kisheria ila haijawahi kuwa sawa mtu kumuuza mtu mwingine..., na leo hii ukiangalia Israel tangia ilivyokuwa 1948 na ilivyo leo hata Kisheria haipo sawa Palestinians are subjugated
Israel wanaona wana haki ya kukaa pale, Hamas na wapalestina wanaona wameporwa nchi. Natural Law na Natural Justice vyote vimekuwa vikibadilika badilika kwenye historia ya binadamu. Wala usifikiri wakati tuliopo ndiyo kilele cha haki.
Natural Justice..., haijawahi kubadilika hata ukiitungia Sheria na ukajiridhisha kwamba ni okay legally does not make it Just...., Natural Justice means being fair without biasness... All Human Being are Equal, making it different (kama kipindi cha Utumwa Hususan wa Africans) did not make it factual kwamba they were not entitled with the same Justice (though not legally)
Unataka UN yenye watu wenye mitazamo tofauti juu ya kilicho sawa na kisicho sawa waje pamoja kumuadhibu "Mkosefu?"
Unajua maana ya One Nation one Vote; Hata kipindi cha USA alivyomvamia Iran alivyotaka kuvamia Kuwait it was United Nations which decided on the thing....
 
Tofautisha Sawa, Haki na Sheria..., Utumwa ulikuwa order of the day Kisheria ila haijawahi kuwa sawa mtu kumuuza mtu mwingine..., na leo hii ukiangalia Israel tangia ilivyokuwa 1948 na ilivyo leo hata Kisheria haipo sawa Palestinians are subjugated

Natural Justice..., haijawahi kubadilika hata ukiitungia Sheria na ukajiridhisha kwamba ni okay legally does not make it Just...., Natural Justice means being fair without biasness... All Human Being are Equal, making it different (kama kipindi cha Utumwa Hususan wa Africans) did not make it factual kwamba they were not entitled with the same Justice (though not legally)

Unajua maana ya One Nation one Vote; Hata kipindi cha USA alivyomvamia Iran alivyotaka kuvamia Kuwait it was United Nations which decided on the thing....
Natural Justice inamaanisha haki ya kusikilizwa bila upendeleo au kuonewa kwenye vyombo vya sheria. Haimaanishi binadamu amezaliwa na haki ambazo binadamu wote wanakubaliana kuwa hizi ni haki za msingi za binadamu wote. Kukubali kuwa hizi ni haki za msingi za binadamu na hizi sizo inategemea mambo mengi na watu wenyewe.

Kama wewe unaona si sawa kuuza na kununua watumwa, au kula watu haimaanishi wengine wanaona hivyo. Wewe utaamini binadamu wote ni sawa lakini wahindi wana caste system ambayo haiamini kama binadamu wote ni sawa.

Kutokukubaliana huko ndiko kunafanya suluhisho pekee la migogoro yetu iwe kuchapana. Na usitegemee UN kutatua migogoro sababu nayo inaundwa na watu wanaotofautiana juu ya lililo sawa na lililo haki.
 
Sasa kama kila mtu anakubalika kusikilizwa bila upendeleo wala kuonewa..., na kuna kitu ambacho yeye anaona anaonewa hapo huwezi kusema mmoja ana haki ya kumtendea ndivyo sivyo mwingine jambo ambalo yeye binafsi angetendewa asingekubaliana nalo
Kama wewe unaona si sawa kuuza na kununua watumwa, au kula watu haimaanishi wengine wanaona hivyo. Wewe utaamini binadamu wote ni sawa lakini wahindi wana caste system ambayo haiamini kama binadamu wote ni sawa.
Wahindi wamekubaliana na hio hali kama kipindi cha Ufalme watu walivyokubaliana kwamba kuna ukoo wa Kifalme na wapo pale ili wengine kuwatumikia..., and it was peacefully so long as watu waliokuwa subjugated walikubaliana na hio hali..., leo hii ufalme ungekuwepo wakati watu wana fikra za demokrasia basi pasingekuwa na amani sababu watu wangestruggle ili kuondoa huo udhalimu; Kwahio dawa ingekuwa ni kuondokana na huo mfumo na sio kuendelea kuwapiga watu ili waendelee kukabaliana na kitu ambacho hawakubaliani nacho
Kutokukubaliana huko ndiko kunafanya suluhisho pekee la migogoro yetu iwe kuchapana. Na usitegemee UN kutatua migogoro sababu nayo inaundwa na watu wanaotofautiana juu ya lililo sawa na lililo haki.
UN wanatofautiana na lililo sawa na lililo Haki, Yaani hawana Sheria zao...? Pili unajua kitu kinatiwa Kupiga Kura.., Ndio maana nimesema ondoa VETO kila Taifa liwemo na iwe one Country One Vote within legal frameworks sio mnapigia Kura vitu vya ajabu na kuleta Tranny of the Majority
 
Back
Top Bottom