Je, baba alitutesa au alitufundisha maisha?

Mkuu sikupingi Yale malezi yamenisaidia Sana kupambana na maisha na kuwa makini na nidhamu kwa kila jambo
 
Alifanya hivyo ili siku nyingine umakini na uwajibikaji uongezeke; sipati picha angekuwa amepotea au kuliwa na wanyama usiku huo ; nadhani mngepewa zamu ya kuwika kama jogoo alfajiri
Mkuu kweri kabisa
Kuku asingeonekana sijui Ile siku ingekuwaje
 
Kongole kwake, hayo maisha kawaida sana kwa watoto wa kota
 
Hilo la kwako dogo... mimi nikiwa std 1 nilikua nafuga nguruwe wa mzee.

Ole wako aje ucku saa 6 angurume... uatenda tafuta magimbi na majani ucku huo huo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ukiishi na mtu anaedhaniwa kuwa ni katili kuna vingi sana unajifunza na hutoshindwa kuishi mazingira yoyote
 

Hongereni sana

Mwamba aliwajenga
 
Natumai ushakuwa mtu mzima sasa. We unaonaje, mliteswa ama mlifundishwa maisha?
 
Kuna kaumri washua wakifika huwa na ukali ukali sometimes hata usio na maana ila wakizeeka wajukuu wanawachezea sana
 
Mdingi hawezi kukutesa ulimtafsiri vibaya shukuru Mungu umebahatika kuishi na mshua mpaka anazeeka
Miss you Dad
 
Kama malezi uliyopitia yalikuwa sahihi basi ungejua jibu la hili swali lako bila kuja kuuliza hapa ila inaonekana malezi aliyowalea baba yenu hayajaleta matokeo chanya au aliyoyadhania kwa asilimia 100%. Maana yake kuna sehemu mzee wako alikosea. Mfano unatumia jibu alilotoa member numbisa kujibu members wengine.

Malezi kama haya mara nyingi yanafanya baba na mtoto wasipatane ukubwani kitu ambacho sio kizuri kwa mzazi lakini hasa mtoto. Mimi sitaki hata kufikiria malezi yangu lakini ndio yamenifanya niwe jasiri na katili, real fighter lakini sio hapo tu bali kwenye akili pia. Tatizo mahusiano ya baba na mtoto ndio hayapo, kitu muhimu zaidi kwenye maisha.

Malezi kama haya yana uzuri na ubaya wake, ukipatia mtoto atakuwa jasiri, fighter na anayetumia akili kufanya maamuzi binafsi na ukikosea sehemu mtoto atakuwa muoga, asiyejiamini na asiyetumia akili yake kufanya maamuzi binafsi bali ataendeshwa kwa hisia na mitazamo ya watu.
Bila shaka umepata jibu lako hapo.

NB: Mzee alikuwa mjeshi vilevile.
 
Kunyauka kisa ugonjwa au cio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…