Watu wa dini wameamua na kuamrishwa kuamini bila kufikiria wala kuuliza, na walifundishwa hivyo tangu utotoni na wazazi wao. Hiyo concept imepandikizwa ndani kabisa vichwani mwao kama maana nzima ya maisha yao na uwepo wao hapa duniani.
Kuwaambia vinginevyo ni sawa na kuangamiza maisha yao. Hivyo wanaogopa, wanaogopa maswali yanayohoji ukweli kuhusu uhalisia wao.
Walioleta hizi dini walilitambua hilo, ni moja ya njia effective sana ya kumuamrisha mtu kwa hiari yake mwenyewe.
Cha kuchekesha ni ukienda UK, Russia na USA utakuta watu wengi ni wadini jina, atheist au hawajali kabisa. Wanachulia Bible kama kitabu ancient kilichojaa hadithi za kufikirika sababu ya worldy naivety ya kipindi hicho. Nadhani hichi kitu kinatokana na average IQ na socioeconomic status ya mataifa husika ukilinganisha na Afrika.
Sababu umasikini unachochea kwa kiasi kikubwa ukuaji wa dini au imani. Hiyo ina-explain kwanini waarabu bado wameshikana na dini yao mpaka leo. Hivyo taarifa njema ni kwamba kadri maendeleo ya technology na economy yanavyokuwa, ndivyo uwepo wa dini unavyopungua. Ukilinganisha hizi ni za kuletwa hapa kwetu, reaction itakuwa kubwa zaidi.
Future generations, kuanzia 2000 na 2010 zitakuja kucheka na kushangaa jinsi past generations zilikuwa zimejaa ujinga wa viwango vya kutisha. Reaction imeshaanza, it's what we do right now.