Bado narudia tena الجنون فنون kwamba uwendawazimu upo wa namna nyingi sana kwa sababu hakuna katika mitume wala masahaba wala wafasiri wa quran wakutegemewa wote ambae kasema adam hakuwa mtu wa mwanzo kuumbwa,hivyo wewe unawakhaalif hawa kwa kujifanya unaamini quran kumbe una ajenda zako zinakuoeleka,sasa vipi nisipatie nikisema uwendawazimu uko wa namna nyingi?
Ili ujitetee ilibidi useme kwamba kuna wafasiri wamenitangulia wakutegemewa ambao wana maono kama yangu akiwemo fulani na fulani jee hawa nao wana aina ya uwendawazimu? Hapo ningekosa majibu kabisa
Alafu jambo la pili sasa katika ilmu ya kisheria ya quran kuna kitu kinaitwa العموم والخصوص ujumla na umaalumu.
Kuna aya zinakuja kwa ujumla wake bila kukhusisha jambo,lakini kuna zingine zinakuja kwa umakhususi kuhusisha jambo fulani.
Mfano aya hii imekuja kwa العموم(kwa jumla)
وإن خفتم ألا تقسطوا في اليتامى فانكحوا ما طاب لكم من النساء مثنى وثلاث ورباع فإن خفتم ألا تعدلوا فواحدة..
[ AN-NISAAI - 3 ]
Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu,....)
Hii aya imekuja kwa عموم (jumla)wala haikufafanua kwamba hao wanawake ni wepi na wepi ama wawe vipi,hivyo mtu anaweza akasimamia aya hiyo kumuoa mwanamke yeyote yule madhali tu ni mwanamke.
Lakini kuna aya hizo hapa chini
ولا تنكحوا المشركات حتى يؤمن ولأمة مؤمنة خير من مشركة ولو أعجبتكم ولا تنكحوا المشركين حتى يؤمنوا ولعبد مؤمن خير من مشرك ولو أعجبكم..
[ AL - BAQARA - 221 ]
Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni...)
ولا تنكحوا ما نكح آباؤكم من النساء إلا ما قد سلف إنه كان فاحشة ومقتا وساء سبيلا
[ AN-NISAAI - 22 ]
Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu na uchukizo na ni njia mbaya.
Aya hizi zinafannya takhsiys(zinakhusisha)kwamba hao wanawake waliotajwa kwa ujumla tunaoweza kuwaoa ndiyo hawa hapa wanaelezwa wawe na sifa zipi hapo juu katika aya.
Kwanza mwanamke asiwe mshirikina mpaka aamini
Pili asiwe mwanamke ambae alishamuoa baba yako tayari na zifa zingine katika aya ila naweka hizi kwa ikhtiswaar
Sasa mtu atakuwa wa ajabu sana kuing'ang'ania aya ambayo imekuja kwa lafdhi ya ujumla wakati zipo ambazo zimekuja kwa lafdhi ya umaalumu kuhsuisha jambo hilo.mfano mtu akang'ang'ana kwamba kwa mujibu wa aya inafaa kumuoa hata mke alomwacha baba na mshirikina kwa sababu aya imetaja tuwaoe wanawake tunaowapenda na wala haikusema mwanamke yupi na yupi tusiwaoe,tutamuambia kuna aya khaaswaa zilizofafanua jambo hilo.
Hiyo ilikuwa ni mifano sasa tuje katika aya ambazo unastadilli nazo.
Kwanza aya zote unazostadili nazo hazikuja kwa lafdhi(tamko)la umaalumu bali zimetaja kwa ujumla na ndyo maana unamuingiza na Nabii Aadamعليه السلام katika ujumla huo,ila sasa kumbuka kama tulivosema kwamba katika aya muna kitu jumla na umaalum.
Aya unazotegemeea zimekuja kwa ujumla ambao lau kusingekuwa na umaalum wa aya zingine kuhusu jambo hilo basi inafaa kustadilli na ujumla huo.
Tuzione kwanza
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللَّهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ ۚ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ
(AN NAH'L - 36)
Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
Aya hii imekuja kwa ujumla wala hakutajwa mtume fulani na fulani
Na mfano wa aya hzo zote zimekuja kwa ujumla wake ya kwamba kila uuma ulikuwa na Mtume.
Sasa basi mkuu kwa taarifa yako wale mitume wote waliotajwa katika quran(isipokuwa aadam) wameelezewa kwamba kulikuwa na watu ambao anaishi nao
Mfano Nabii Mussa na Haaaroun aya zinaonyesha alikuwa na kina firauni na wana israel,kwa hvyo mussa walikuwepo qaumu.
Nabii Issa nae tunaona walikuwepo mayahudi
Nabii ibraahim tunaona naye alikuwa na baba yake kuonyesha wapo ambao walimtangulia
Nabii ismaail yupo baba yetu Ibraahim kuonyesha walimtangulia tayari
Nabii is'haaka na Yaakub wametanguliwa na Baba yetu ibraahim
Kadhaalika hata Mtume waMwisho Muhammad (s.a.w)katanguliwa na baba zake kuonyesha wapo waliokuwa kabla yake
Sasa hutakuta aya katika quran inasema kwamba Nabii Adam alitanguliwa na watu kama ilivyo kwa manabii wengine,kama ipo ilete hapa.
BaliBALI WEWE UNATUMIA UJUMLA WA AYA KUMTIA AAADAM KATIKA UJUMLA HUO.
AYA ZINAZOSEMA KILA UUMA ULITUMIWA MJUMBE BASI HAZIKUTAJA NABII MAULUM BALI ZIMEKUSANYA UJUMLA.
Jee aya ipi inamtoa adam katika ujumla huo?
KWANZA KABISA katika kutajiwa mitume na quran Adam ndiye nabii wa kwanza kisha baada ya mda kupita akatumwa Nuhu sasa na kuteremshiwa Wahyi ili awaonye watu wake waache shirki
Sasa hapa UKITAKA UNAWEZA KUNIPA NINI TAFSIRI YA WAHYI.
Asema Allah
إنا أوحينا إليك كما أوحينا إلى نوح والنبيين من بعده وأوحينا إلى إبراهيم وإسماعيل وإسحاق ويعقوب والأسباط وعيسى وأيوب ويونس وهارون وسليمان وآتينا داوود زبورا
[ AN-NISAAI - 163 ]
Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe(muhammad) kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi.
Aya inathibitisha kwamba hata nabii Adam hakupewa wahyi kama manabii waliokuja baada yake kwa sababu Kizazi cha Adam hakikuzama katika shirki bali ilifanyika kosa la kuuwana ambalo ilikuwa ni sababu ya ufisadi.
ALAFU UNATUAMBIA KWAMBA ALIKUWA WA KWANZA KUUMBWA KIROHO?
SASA TUAMBIE HIYO KIROHO NI VIPI SIO UNAVUNGA VUNGA TU ..
Aya ambazo zinathibitisha kuumbwa kwa Nabii adam kuwa mtu wa mwanzo zipo ila sasa tu nina mashaka isije kuwa utasema UNATAKA AYA AMBAYO INASEMA "nabii adam ndiyo mtu wa kwanza"
Aya hiyo ilosema moja kwa moja hivyo haipo kama vile ambavyo hakuna aya ya moja kwa moja ilosema kwamba nabii adam aliwakuta watu kabla yake.
BALI AYA zinaonyesha yeye ndo aliumbwA mwanzo kwa wenye akili ambao wameepukana na uwendawazimu
Allah asimulia
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ
(AL - BAQARA - 30)
Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua.
Duniani mwanzo walikuwako majini wakafanya ufisadi,hivyo malaika waliposema kwamba watamwagana damu walikuwa wanafananisha na yale matendo ya majini ila Allah akawajibu kwamba anajua wasoyajua.aya hapo imetaja kwamba Allah alikusudia kumuumba binadamu.
Kisha akasema baada ya kumuumba
وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
(AL - BAQARA - 31)
Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli.
Kisha akasema katika aya ingine
وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ
[ AL - A'RAAF - 11 ]
Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.
Aya inaonyesha kwamba Adam aliumbwa akatiwa sura kisha ndipo akawaambia malaika wamsujudie adam
Japo imekuja lafdhi ya jam,u(jumla)kuonyesha na sisi kwamba alituumba na kututia sura lakini wa mwanzo ni Adam ndyo mana akasema kisha akawaambia malaika wamsujudie.
Sasa huyu nabii Adam sasa kuonyesha kwamba adam ndiye ambaye alitakiwa asujudiwe Allah anathibitisha
قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
[ AL - HIJR - 33 ]
Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura.
Kumbe unaona kwamba ibilisi alikataa kumsujudia yule aliyeumbwa kwa udongo,sasa huoni hapo ibilisi ndo alikataa kumsujudia Adam?
Kisha akasema tena Allah
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
[ AL - HIJR - 28 ]
Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
Bila shaka aya hizi anakusudiwa wa mwanzo kuumbwa aliumbwa kwa udongo.
SASA WEWE ULETE AYA ZINAZOSEMA KWAMBA HUYU HAKUWA WA KWANZA KUUMBWA WAPO WALOMTANGULIA...
Nilichelewa kujibu kwa sababu nilikuwa natafakari huyu ninayejadiliana naye ni mtu aliye sawasawa au!!-- kwa sababu hajengi hoja bila kutukana ambapo ni kinyume kabisa na mafundisho ya Qur'an, katika (16:125) Allah anasema:-
"Ita katika njia ya mola wako kwa hekima na mawaidha yaliyomema--"
Hivyo Allah anatunasihi kutumia hekima na lugha nzuri ttunapofikisha ujumbe wake.
Anasema eti,tutegemee wafasirina kufasiri Qur'an!!, wapi mtume (saw) alisema hivyo??. Qur'an yenyewe na hadithi za mtume (saw) zinatosha wala mtume (saw) hakusema popote tuwafuate wafasirina.
Elimu ya sheria ya Qur'an,eti inasema العموم و الخصوص yaani ujumla na umaalum unapatikana katika aya za Qur'an!!!🤔🤔-- wewe unaota (day dreams) ,hivi ni wapi mtume (saw) alifundisha jambo hilo??, tukufuate Wewe unayetaka kudanganya umma au Qur'an ??. Qur'an yenyewe inasema inazo aya za aina mbili:-
Muhkamat na Mutashabiat (محكمات و متشابهات) na muhkamat ni mama wa kitabu (هن ام الكتاب) yaani ni aya zenye maana za msingi zilizo wazi, hivyo basi aya niliyoitoa ya An nahl:36, ni miongoni mwa aya muhkamat kwa sababu ni aya iliyowazi kueleweka ila tu kwa sababu watu wanataka kushikilia upotevu wao "dogmatically" ndiyo maana wanalazimisha kuwa katika hiyo aya nabii Adam (as) huyumo hata uoga wa Allah hawana kwa kujaribu kumkosoa Allah. Aya ipo wazi inasema:-
Kwa hakika kwa KILA UMMA tuliutumia mtume kwamba, muabuduni Allah na mwepukeni shetani-----" (An nahl:36).
👆🏻Hapo maana yake kila mtume alikuwa na umma wake ambao kwao alitumwa hivyo basi kwa mujibu wa hiyo aya umma unakuwepo ndipo nabii anatumwa na tunakuliana kuwa Adam (as) alikuwa nabii.
👆🏻Hapo hakuna mtu atapinga labda aliyekuwa na kibri na ujeuri kumkosoa Allah, mtu yule aliyetunga sheria zake za kuhukumu aya za Allah eti, (ujumla na makhsusi) eti, Allah ni kipofu asijue kuwa hiyo aya Adam (as) hausiki na ashindwe kumtaja kwamba hahusiki !!??.
Eti,anataka nilete aya inayosema Nabii Adam (as) alitanguliwa na watu!!, huioni hiyo (An nahl:36)??.
Nashukuru umekiri wewe mwenyewe kuwa:- "aya inayosema moja kwa moja nabii Adam ndiyo mtu wa kwanza haipo"
Na mimi ninaongezea hata inayosema kwa mbali kuwa nabii Adam (as) ni mtu wa kwanza kuumbwa haipo.
Umetoa aya (2:30) kutetea hoja yako kwamba nabii Adam (as) alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa, ni kichekesho kikubwa, aya inasema:-
"Na kumbuka mola wako alipowaambia Malaika; mimi nitamuweka katika ardhi khalifa----"
Hapo bila shaka neno khalifa ndiyo limekuchanganya, khalifa ni neno lenye maana kadha kama, kiongozi,mtawala,muwakilishi nk, sasa kama ni kiongozi ni lazima kwanza wawepo wale watakaoongozwa, kama ni mtawala hawi mtawala hadi watawaliwa wawepo kwanza na kama ni mwakilishi ni lazima amwakilishe muhusika kwa watu ambao wapo kwa sababu mwakilishi anatumwa kumwakilisha mtu (mfano) kwenye mkutano uliokuwepo na anakwenda kumuwakilisha hivyo nabii Adam (as) alikuwa anamuwakilisha Allah kwa qaumu yake, katika Qur'an nabii Daudi (as) kaitwa khalifa pia kwa sababu alikuta umma upo na akawa mtawala juu yao kwa sababu pia alikuwa mfalme.
Umetoa aya; Al aaraf:11 na Al hijr: 26.
Hizo aya zinazungumzia uumbaji wetu sisi sote na jinsi Ibilisi alipokataa kumsujudia (kumsaidia) Adam (as) wala haziainishi kwamba Adam (as) alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa.
Yeye Adam (as) alikuwa ni nabii wa kwanza lakini kamwe hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa na aliishi takriban miaka 6,000 na ushee iliyopita na kabla yake watu wameishi mamilioni ya miaka kabla yake ambao hawakuwa na miongozo ya Allah.
Ukikadiria miaka iliyopita kwa baadhi ya manabii (as) utakuta kwamba:-
Adamu-----miaka 6,000 na ushee
Nuhu---
Ibrahim---
Ismael---
Ishaaq--
Yakuub----
Yusuf----
Mussa-----miaka 4,000 na ushee
Issa-----miaka 2,000 na ushee
Muhammad (saw)-----1,400 na ushee.
Hujaleta aya inayoonyesha kuwa Adam (as) ni mtu wa kwanza kuumbwa.
Angalizo:- mtukufu mtume (saw) alisema tulinde ndimi zetu. Yaani tuepuke maneno machafu na hiyo ndiyo taswira ya muislamu safi.