Katika Dini ya Kiislamu Adam anajulikana kama Nabii (mtume), hivyo basi kwa taratibu za kawaida ni kwamba Nabii hutokea (hutokana) miongoni mwa watu wake ili aje kuwaonya na kuwafundisha maagizo aliyotumwa kutoka kwa Mungu, hivyo Nabii huwa anazaliwa katika umma atakaokuja kuuonya na jambo hili tunaliona hata kwa mitume wengine.
Kwa muktadha huo, Adam hawezi kuwa mtu wa kwanza kuumbwa,bali ukisema kwamba yeye alikuwa ndiye mtu wa kwanza (katika manabii wote) kufunuliwa/kupata wahy kutoka kwa Mungu au ukasema Yeye alikuwa ni Nabii wa kwanza kutumwa na Mungu hapo ni SAWA kabisa na ninaunga mkono hiyo rai. Lakini yeye hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa bali alikuwa nabii wa kwanza kabisa.
Na hii imewachanganya sana watu wakidhani kwamba Yeye ndiyo mtu wa kwanza kuumbwa---Yeye ni nabii wa kwanza kutumwa (au unaweza kusema yeye ni mtu wa kwanza kuumbwa KIROHO). Kuumbwa kiroho maana yake ni kupokea ufunuo kutoka kwa Mungu ili awapelekee watu (ujumbe).