Umeuliza maswali mengi hadi inanipa shida kuyajibu kwa pamoja, unakiwa uulize kwa awamu (in installments).
Nilipotaja sayansi sikuwa na maana kwamba nimethibitisha kwamba Adam (as) hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa bali nilitaka ujue kuwa kama ilivyokuwa historia ni yenye faida kwetu na ndivyo ilivyokuwa sayansi.
Unaposema kuwa sayansi na Imani ni tofauti kabisa na sayansi eti inapinga kuwepo Mungu---huo ni uongo mkubwa sana, hakuna Sayansi inayopinga Mungu bali wapo WANASAYANSI kwa ujinga wao wanapinga uwepo wa Mungu. Sayansi ni elimu iliyotoka kwa Mungu na inatusaidia kuyakabili mazingira yetu ili tuweze kuishi vizuri na tumusbudu Mungu vizuri pia sayansi inatusaidia kujua utukufu wa Mungu katika kusoma na kutafiti maumbile ya Mungu,hivyo sayansi na Imani (vinashikamana) na vyote vimetoka kwake.
Mada yetu ni Nabii Adam (عليه السلام) alikuwa ni mtu wa kwanza kuumbwa duniani?.
Wewe ulisema ungeleta utetezi wako kutoka kwenye Qur'an lakini hadi saa hii hujaleta hata aya moja kutetea hoja yako bali umeamua kunitukana (الجنون فنون), je hivyo ndivyo ulivyofundishwa na Mtukufu Mtume (saw) kumtusi mwislamu mwenzako??. (هناك خطأ في رأسك).
Eti,unauliza je hawezi kuanza kuja nabii kabla ya qaumu yake? ,wewe ndio unatakiwa ulete aya inayokuunga mkono katika hiyo hoja yako na wala siyo mimi!! Mimi ninanukuu Qur'an pale iliposema;-
و لقد ضل قبلهم أكثرر الأولين و لقد أرسلنا فيهم منذيرين yaani:- Na bila shaka hapo kabla (watu) walipopotea na bila shaka tuliwatumia waonyaji (37:71-72).
[emoji1312]Angalia hiyo aya inasema watu wa kabla ya Mtume (saw) walipokuwa wamepotea Mungu aliwatuma waonyaji (manabii na Adam akiwemo) kuwaonya watu wao na kama Adam ni nabii basi hawezi kuepuka hiyo kanuni iliyotajwa na Qur'ani hivyo nabii anakuja kuwafundisha watu aliowakuta katika upotevu.
Unauliza eti, kama ni hivyo ina maana manabii waliotangulia hawatuhusu??, ukiwa Muislamu lazima uwakubali manabii wote na kila nabii alikuja kwa ajili ya Qaumu yake na akaongea na watu wake katika lugha aliyowakutanayo (14:4) na hata Mtume mtukufu (saw) naye alitumwa kwa duniani nzima lakini kwanza alianza kuwaonya ndugu zake waarabu kwa lugha aliyowakutanayo kiarabu.
Unataka aya inayoonyesha kwamba umma wake ulianza kuwepo kabla nabii Adam (as) hajatokea, wewe unanishangaza sana kwani huioni hiyo aya (An nahl:36) maudhui yake??, inasema; و لقد بعثنا في كل أمة رسل --- yaani , na bila shaka tulituma kwa kila ummat mtume---.
Hivi unapoambiwa kwa mfano, "tumemtuma mjumbe kupeleka barua ofisi ya kata" inaingia akilini kwamba hiyo ofisi ya kata inaweza isiwepo lakini ikawepo baada ya mjumbe kutumwa??, Hoja gani za ajabu ajabu unazoleta hapa??.
Eti unataka kujua tofauti ya kuumbwa kimwili na kiroho kwa mujibu wa Qur'an, nasema hivi hata pia utataka kujua kwa mujibu wa Qur'an kwamba ni wapi imeandikwa kuikanyaga Qur'an kwa miguu ni dhambi!!.
Tumia "common sense" tu, mtu anapokuwa ni mchamungu roho yake inakuwa na "khulqa" njema hivyo anakuwa roho yake imeumbika na ndiyo maana Mungu amemsifu mtukufu Mtume (saw) katika Qur'an pale alipomuambia; "hakika unazo hulka njema za kipekee" (sikumbuki aya). Na kuumbika ki mwili ni "khalaqa" katika lugha ya kiarabu, sasa angalia hayo maneno, khulqa na khalaqa la kwanza linahusu roho na la pili linahusu mwili.
Unasema eti, mimi ninataka kumfanya mola eti akiona watu wamekosea ndipo atume mjumbe!!
[emoji1312]Mimi ninanukuu Qur'an kama yeye mwenyewe Allah mtukufu alivyosema:- kwamba hapo kabla watu wengi walipoasi aliwapelekea waonyaji (37:71-72) na nabii Adam (as) alikuwa muonyaji wa kabla ya Mtukufu mtume (saw) hivyo naye pia kanuni hii ya Allah inamshika kwamba aliwakuta watu wake kwenye upotevu ndipo Allah akamtuma aende kuwaonya hivyo basi hakuwa ni mtu wa kwanza kuumbwa.
Ukumbusho: Bado hujaleta aya inayothibitisha madai yako kwamba Nabii Adam (as) alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa.
Bado narudia tena الجنون فنون kwamba uwendawazimu upo wa namna nyingi sana kwa sababu hakuna katika mitume wala masahaba wala wafasiri wa quran wakutegemewa wote ambae kasema adam hakuwa mtu wa mwanzo kuumbwa,hivyo wewe unawakhaalif hawa kwa kujifanya unaamini quran kumbe una ajenda zako zinakuoeleka,sasa vipi nisipatie nikisema uwendawazimu uko wa namna nyingi?
Ili ujitetee ilibidi useme kwamba kuna wafasiri wamenitangulia wakutegemewa ambao wana maono kama yangu akiwemo fulani na fulani jee hawa nao wana aina ya uwendawazimu? Hapo ningekosa majibu kabisa
Alafu jambo la pili sasa katika ilmu ya kisheria ya quran kuna kitu kinaitwa العموم والخصوص ujumla na umaalumu.
Kuna aya zinakuja kwa ujumla wake bila kukhusisha jambo,lakini kuna zingine zinakuja kwa umakhususi kuhusisha jambo fulani.
Mfano aya hii imekuja kwa العموم(kwa jumla)
وإن خفتم ألا تقسطوا في اليتامى فانكحوا ما طاب لكم من النساء مثنى وثلاث ورباع فإن خفتم ألا تعدلوا فواحدة..
[ AN-NISAAI - 3 ]
Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu,....)
Hii aya imekuja kwa عموم (jumla)wala haikufafanua kwamba hao wanawake ni wepi na wepi ama wawe vipi,hivyo mtu anaweza akasimamia aya hiyo kumuoa mwanamke yeyote yule madhali tu ni mwanamke.
Lakini kuna aya hizo hapa chini
ولا تنكحوا المشركات حتى يؤمن ولأمة مؤمنة خير من مشركة ولو أعجبتكم ولا تنكحوا المشركين حتى يؤمنوا ولعبد مؤمن خير من مشرك ولو أعجبكم..
[ AL - BAQARA - 221 ]
Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni...)
ولا تنكحوا ما نكح آباؤكم من النساء إلا ما قد سلف إنه كان فاحشة ومقتا وساء سبيلا
[ AN-NISAAI - 22 ]
Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu na uchukizo na ni njia mbaya.
Aya hizi zinafannya takhsiys(zinakhusisha)kwamba hao wanawake waliotajwa kwa ujumla tunaoweza kuwaoa ndiyo hawa hapa wanaelezwa wawe na sifa zipi hapo juu katika aya.
Kwanza mwanamke asiwe mshirikina mpaka aamini
Pili asiwe mwanamke ambae alishamuoa baba yako tayari na zifa zingine katika aya ila naweka hizi kwa ikhtiswaar
Sasa mtu atakuwa wa ajabu sana kuing'ang'ania aya ambayo imekuja kwa lafdhi ya ujumla wakati zipo ambazo zimekuja kwa lafdhi ya umaalumu kuhsuisha jambo hilo.mfano mtu akang'ang'ana kwamba kwa mujibu wa aya inafaa kumuoa hata mke alomwacha baba na mshirikina kwa sababu aya imetaja tuwaoe wanawake tunaowapenda na wala haikusema mwanamke yupi na yupi tusiwaoe,tutamuambia kuna aya khaaswaa zilizofafanua jambo hilo.
Hiyo ilikuwa ni mifano sasa tuje katika aya ambazo unastadilli nazo.
Kwanza aya zote unazostadili nazo hazikuja kwa lafdhi(tamko)la umaalumu bali zimetaja kwa ujumla na ndyo maana unamuingiza na Nabii Aadamعليه السلام katika ujumla huo,ila sasa kumbuka kama tulivosema kwamba katika aya muna kitu jumla na umaalum.
Aya unazotegemeea zimekuja kwa ujumla ambao lau kusingekuwa na umaalum wa aya zingine kuhusu jambo hilo basi inafaa kustadilli na ujumla huo.
Tuzione kwanza
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللَّهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ ۚ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ
(AN NAH'L - 36)
Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
Aya hii imekuja kwa ujumla wala hakutajwa mtume fulani na fulani
Na mfano wa aya hzo zote zimekuja kwa ujumla wake ya kwamba kila uuma ulikuwa na Mtume.
Sasa basi mkuu kwa taarifa yako wale mitume wote waliotajwa katika quran(isipokuwa aadam) wameelezewa kwamba kulikuwa na watu ambao anaishi nao
Mfano Nabii Mussa na Haaaroun aya zinaonyesha alikuwa na kina firauni na wana israel,kwa hvyo mussa walikuwepo qaumu.
Nabii Issa nae tunaona walikuwepo mayahudi
Nabii ibraahim tunaona naye alikuwa na baba yake kuonyesha wapo ambao walimtangulia
Nabii ismaail yupo baba yetu Ibraahim kuonyesha walimtangulia tayari
Nabii is'haaka na Yaakub wametanguliwa na Baba yetu ibraahim
Kadhaalika hata Mtume waMwisho Muhammad (s.a.w)katanguliwa na baba zake kuonyesha wapo waliokuwa kabla yake
Sasa hutakuta aya katika quran inasema kwamba Nabii Adam alitanguliwa na watu kama ilivyo kwa manabii wengine,kama ipo ilete hapa.
BaliBALI WEWE UNATUMIA UJUMLA WA AYA KUMTIA AAADAM KATIKA UJUMLA HUO.
AYA ZINAZOSEMA KILA UUMA ULITUMIWA MJUMBE BASI HAZIKUTAJA NABII MAULUM BALI ZIMEKUSANYA UJUMLA.
Jee aya ipi inamtoa adam katika ujumla huo?
KWANZA KABISA katika kutajiwa mitume na quran Adam ndiye nabii wa kwanza kisha baada ya mda kupita akatumwa Nuhu sasa na kuteremshiwa Wahyi ili awaonye watu wake waache shirki
Sasa hapa UKITAKA UNAWEZA KUNIPA NINI TAFSIRI YA WAHYI.
Asema Allah
إنا أوحينا إليك كما أوحينا إلى نوح والنبيين من بعده وأوحينا إلى إبراهيم وإسماعيل وإسحاق ويعقوب والأسباط وعيسى وأيوب ويونس وهارون وسليمان وآتينا داوود زبورا
[ AN-NISAAI - 163 ]
Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe(muhammad) kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi.
Aya inathibitisha kwamba hata nabii Adam hakupewa wahyi kama manabii waliokuja baada yake kwa sababu Kizazi cha Adam hakikuzama katika shirki bali ilifanyika kosa la kuuwana ambalo ilikuwa ni sababu ya ufisadi.
ALAFU UNATUAMBIA KWAMBA ALIKUWA WA KWANZA KUUMBWA KIROHO?
SASA TUAMBIE HIYO KIROHO NI VIPI SIO UNAVUNGA VUNGA TU ..
Aya ambazo zinathibitisha kuumbwa kwa Nabii adam kuwa mtu wa mwanzo zipo ila sasa tu nina mashaka isije kuwa utasema UNATAKA AYA AMBAYO INASEMA "nabii adam ndiyo mtu wa kwanza"
Aya hiyo ilosema moja kwa moja hivyo haipo kama vile ambavyo hakuna aya ya moja kwa moja ilosema kwamba nabii adam aliwakuta watu kabla yake.
BALI AYA zinaonyesha yeye ndo aliumbwA mwanzo kwa wenye akili ambao wameepukana na uwendawazimu
Allah asimulia
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ
(AL - BAQARA - 30)
Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua.
Duniani mwanzo walikuwako majini wakafanya ufisadi,hivyo malaika waliposema kwamba watamwagana damu walikuwa wanafananisha na yale matendo ya majini ila Allah akawajibu kwamba anajua wasoyajua.aya hapo imetaja kwamba Allah alikusudia kumuumba binadamu.
Kisha akasema baada ya kumuumba
وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَـٰؤُلَاءِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
(AL - BAQARA - 31)
Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli.
Kisha akasema katika aya ingine
وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ
[ AL - A'RAAF - 11 ]
Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.
Aya inaonyesha kwamba Adam aliumbwa akatiwa sura kisha ndipo akawaambia malaika wamsujudie adam
Japo imekuja lafdhi ya jam,u(jumla)kuonyesha na sisi kwamba alituumba na kututia sura lakini wa mwanzo ni Adam ndyo mana akasema kisha akawaambia malaika wamsujudie.
Sasa huyu nabii Adam sasa kuonyesha kwamba adam ndiye ambaye alitakiwa asujudiwe Allah anathibitisha
قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
[ AL - HIJR - 33 ]
Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura.
Kumbe unaona kwamba ibilisi alikataa kumsujudia yule aliyeumbwa kwa udongo,sasa huoni hapo ibilisi ndo alikataa kumsujudia Adam?
Kisha akasema tena Allah
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
[ AL - HIJR - 28 ]
Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
Bila shaka aya hizi anakusudiwa wa mwanzo kuumbwa aliumbwa kwa udongo.
SASA WEWE ULETE AYA ZINAZOSEMA KWAMBA HUYU HAKUWA WA KWANZA KUUMBWA WAPO WALOMTANGULIA...