Je, Binadamu tulikuja duniani kimakosa au ni mipango ya Mungu?

Ndio maana nikasema humu kuna watu wa imani tofauti na misimamo tofauti,sasa wewe unajuaje kuwa mie nautafuta ukweli na si kwamba mie ndio nataka kukupa wewe ukweli?

Mie nimeekuuliza swali lenye kukuhusu wewe binafsi ila ajabu unataka nije kanisani.

Ila basi tukubali kutokukubaliana.
 
Mkuu sasa umeanza kujionyesha wewe ni nani nawajua ambao hutyumia hayo maandiko,nikuulize swali mwanjeshi anapokuwa vitani kuilinda nchi yake akiua ni dhambi au siyo dhambi kwa imani yako?Hilo andiko ulilotumia nipe nitashukuru najua lipo ila sikumbuki,nalihitaji ili nilisome ikiwezekana chapter yote,shida yako na ndugu zako huwa mnakuja na kamstari kamoja wakati ukisoma story yote inaweza ikakupa jibu.
Nimeupata 1samwel 15:3 ,nitausoma
 
Kwanza kabla ya kuendelea naona umeanza kwa kusema sasa nimejionesha mie ni nani.

Ningeomba kukuuliza kwanza ni kipi nilichofanya ambacho kimekufanya useme nimeanza kujionesha mie ni nani? Maana naona umeniweka kwenye kundi la watu ambao hata sijawajui ni akina nani.
 
Ndo mana mimi huwa mtu akijadili haya mambo kwa mujibu wa kitabu chake cha imani namuacha kwa sababu mimi siamini kitabu chake na yeye haamini kitabu changu hivyo itakuwa ni mabishano tu jambo ambalo hatuwezi kufikia muafaka.

Ila mtu akikubali kwamba kitabu anachokiamini fulani basi hakuna ubaya mkaanzisha majadiliano ya kielimu kwa sababu marejeo yanakiwa ni mamoja.

Mm siwezi kujadiliana na mtu kuhusu bibilia kwa sababu sina idea wala ujuzi nayo nawaachia wenyewe kitabu chao,
 
Mie nijuavyo kuamini inamaanisha hufahamu kuwa ni kweli au ni uongo mpaka pale utakapo dhibitisha..

Na kumbuka pia kuna kutokujua kitu,na kwavile sijui haimaanishi kuwa niamini coz sijui

Mm sijui kuwa Mungi yupo au hayupo hiyo sio sababu ya kufuanya mie niamini kuwa yupo au hayupo Mpk pale nitakapo kubaliana na fact ambazo zinaniconvive Niamini Na kisha amini haita maanisha kuwa ni kweli mungu yupo aui niongo

Sasa basi mie sijaona fact yeyote yakufanya niamini mungu yupo,NITAENDELEA KUT KUTOKUJUA mnaosema kweli natumai mtanidhibitishia
 
Kwa hadi sasa kutokuona sababu yeyote yenye kukushawishi kuamini kuwepo Mungu maana yake kwako ni sawa na kwamba haujaona lolote lenye kumuhitaji Mungu kiasi cha wewe ufikiri kuamini uwepo wake na hivyo kwako uwezokano wa kutokuwepo Mungu una make sense kwako.

Niseme tu kwamba watu hawasemi Mungu yupo kwa sababu wana uthibitisho bali kuna yaliyowafikirisha na kufikia kuamini uwepo wa Mungu,maana kama ingekuwa ni suala la uthibitisho tu basi nafikiri kusingekuwa na mabishano ya Mungu yupo au hayupo,kwa maana wote tungekuwa tunakubali uwepo wake maana isingeleta maana et watu hawajui uwepo wake kwa sababu hakuna uthibitisho,na ndiyo maana nikasema kama hujaona sababu ya uhitaji wa uwepo wa Mungu basi itakuwa kwako ina make sense uwezekano wa kutokuwepo Mungu.
 
Mimi sijui kama yupo,na sijakubaliana na fact zinazo sema yupo
.nadhan umenielewa hapo WATU WA DINI WANAAMINI ILA KUAMINIKWAO HAIMAANISHI KUWA KWELI MUNGU YUPO AU HAYUPO ila wanaamini tu kuwa yupo coz ya fact walizo zielewa
 


Nilichelewa kujibu kwa sababu nilikuwa natafakari huyu ninayejadiliana naye ni mtu aliye sawasawa au!!-- kwa sababu hajengi hoja bila kutukana ambapo ni kinyume kabisa na mafundisho ya Qur'an, katika (16:125) Allah anasema:-

"Ita katika njia ya mola wako kwa hekima na mawaidha yaliyomema--"

Hivyo Allah anatunasihi kutumia hekima na lugha nzuri ttunapofikisha ujumbe wake.

Anasema eti,tutegemee wafasirina kufasiri Qur'an!!, wapi mtume (saw) alisema hivyo??. Qur'an yenyewe na hadithi za mtume (saw) zinatosha wala mtume (saw) hakusema popote tuwafuate wafasirina.

Elimu ya sheria ya Qur'an,eti inasema العموم و الخصوص yaani ujumla na umaalum unapatikana katika aya za Qur'an!!!🤔🤔-- wewe unaota (day dreams) ,hivi ni wapi mtume (saw) alifundisha jambo hilo??, tukufuate Wewe unayetaka kudanganya umma au Qur'an ??. Qur'an yenyewe inasema inazo aya za aina mbili:-
Muhkamat na Mutashabiat (محكمات و متشابهات) na muhkamat ni mama wa kitabu (هن ام الكتاب) yaani ni aya zenye maana za msingi zilizo wazi, hivyo basi aya niliyoitoa ya An nahl:36, ni miongoni mwa aya muhkamat kwa sababu ni aya iliyowazi kueleweka ila tu kwa sababu watu wanataka kushikilia upotevu wao "dogmatically" ndiyo maana wanalazimisha kuwa katika hiyo aya nabii Adam (as) huyumo hata uoga wa Allah hawana kwa kujaribu kumkosoa Allah. Aya ipo wazi inasema:-

Kwa hakika kwa KILA UMMA tuliutumia mtume kwamba, muabuduni Allah na mwepukeni shetani-----" (An nahl:36).

👆🏻Hapo maana yake kila mtume alikuwa na umma wake ambao kwao alitumwa hivyo basi kwa mujibu wa hiyo aya umma unakuwepo ndipo nabii anatumwa na tunakuliana kuwa Adam (as) alikuwa nabii.

👆🏻Hapo hakuna mtu atapinga labda aliyekuwa na kibri na ujeuri kumkosoa Allah, mtu yule aliyetunga sheria zake za kuhukumu aya za Allah eti, (ujumla na makhsusi) eti, Allah ni kipofu asijue kuwa hiyo aya Adam (as) hausiki na ashindwe kumtaja kwamba hahusiki !!??.

Eti,anataka nilete aya inayosema Nabii Adam (as) alitanguliwa na watu!!, huioni hiyo (An nahl:36)??.

Nashukuru umekiri wewe mwenyewe kuwa:- "aya inayosema moja kwa moja nabii Adam ndiyo mtu wa kwanza haipo"

Na mimi ninaongezea hata inayosema kwa mbali kuwa nabii Adam (as) ni mtu wa kwanza kuumbwa haipo.

Umetoa aya (2:30) kutetea hoja yako kwamba nabii Adam (as) alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa, ni kichekesho kikubwa, aya inasema:-

"Na kumbuka mola wako alipowaambia Malaika; mimi nitamuweka katika ardhi khalifa----"

Hapo bila shaka neno khalifa ndiyo limekuchanganya, khalifa ni neno lenye maana kadha kama, kiongozi,mtawala,muwakilishi nk, sasa kama ni kiongozi ni lazima kwanza wawepo wale watakaoongozwa, kama ni mtawala hawi mtawala hadi watawaliwa wawepo kwanza na kama ni mwakilishi ni lazima amwakilishe muhusika kwa watu ambao wapo kwa sababu mwakilishi anatumwa kumwakilisha mtu (mfano) kwenye mkutano uliokuwepo na anakwenda kumuwakilisha hivyo nabii Adam (as) alikuwa anamuwakilisha Allah kwa qaumu yake, katika Qur'an nabii Daudi (as) kaitwa khalifa pia kwa sababu alikuta umma upo na akawa mtawala juu yao kwa sababu pia alikuwa mfalme.

Umetoa aya; Al aaraf:11 na Al hijr: 26.

Hizo aya zinazungumzia uumbaji wetu sisi sote na jinsi Ibilisi alipokataa kumsujudia (kumsaidia) Adam (as) wala haziainishi kwamba Adam (as) alikuwa mtu wa kwanza kuumbwa.

Yeye Adam (as) alikuwa ni nabii wa kwanza lakini kamwe hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa na aliishi takriban miaka 6,000 na ushee iliyopita na kabla yake watu wameishi mamilioni ya miaka kabla yake ambao hawakuwa na miongozo ya Allah.

Ukikadiria miaka iliyopita kwa baadhi ya manabii (as) utakuta kwamba:-

Adamu-----miaka 6,000 na ushee
Nuhu---
Ibrahim---
Ismael---
Ishaaq--
Yakuub----
Yusuf----
Mussa-----miaka 4,000 na ushee
Issa-----miaka 2,000 na ushee
Muhammad (saw)-----1,400 na ushee.


Hujaleta aya inayoonyesha kuwa Adam (as) ni mtu wa kwanza kuumbwa.

Angalizo:- mtukufu mtume (saw) alisema tulinde ndimi zetu. Yaani tuepuke maneno machafu na hiyo ndiyo taswira ya muislamu safi.
 
Hiyo nayo ni imani mkuu.
Kwa maana unaamini kutokuwepo kw mungu,au hauamini hivyo?
Kwa hvyo kama hiyo nayo ni imani basi mtu Naweza akawa na haki ya kukudai uthibiitisho w imani yako.

Unajitoaje katika kundi ya waumini wanaokanusha uwepo wa Mungu kwa mfano?
 
Wacha tuende na swali moja moja kwanza mana nilichogundiua hapa tunapiga mbuzi gitaa.

Unaposema ukikadiria miaka ya manabii naomba uniambie unakadiria kupitia nini au kifaa gani ?

Na wapi katika quran panazungumzia kwamba adam aliishi miaka 6000 ushahidi huo umeutoa wapi?
 
Mie sipo ktk kundi la wanao amini mungu hayupp

Wewe ukisema mungu yupo si sawa na asemaye anamini mungu yupo

We ukinambia yupo inamaana ulidhibitisha kweli yupo

Sasa mie sijui kwamba yupo ila nasikia watu wanaamini kwamba yupo kwa fact zao na wangine wanasema yupo
.SASA HAO WANAO SEM YUPP WANADHIBITISHIE KAMA KWELI YUPO ILI NAMI NIPATE KUJUA

SIPO Ktk kundi la wanao amini kuwa Mungu hayupo na pia sipo ktkkundi la wanao sema mungu yupo

Usinipangie mkuu
 
Nani kakupangia mkuu.

We tulia na imani yako ya kutokuwepo kwa Mungu ama kuwepo kwake wala hakuna alokupangia mku
 


(Counter question) ni jibu lako.

Wapi katika Qur'an unapata nabii Mussa (as) aliishi takriban miaka 4,000 iliyopita au Nabii isa (as) aliishi takriban miaka 2000 iliyopita?

Tahadhari: usitoe lugha chafu na uwe kama muislamu safi.
 
(Counter question) ni jibu lako.

Wapi katika Qur'an unapata nabii Mussa (as) aliishi takriban miaka 4,000 iliyopita au Nabii isa (as) aliishi takriban miaka 2000 iliyopita?

Tahadhari: usitoe lugha chafu na uwe kama muislamu safi.
Sielewi kiingereza hivyo nakuomba utumie kiswahili ikiwa hutojali.

Pili sijapata kuona kwenye quran kama nabii Mussa aliishi miaka 4000

Na sijapata kuona kama nabii issa aliishi miaka 2000 iliyopita

Mimi sijaona hayo katika qurani
Ukitazama quran utaona inasema nabii Nuhu aliishi na watu wake miaka 950 .

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُونَ

[ AL - A'NKABUT - 14 ]
Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka khamsini. Basi tufani liliwachukua, nao ni madhaalimu.

Quran ikibainisha idadi ya miaka tunaichukua kama ilivyobainishwa,na sio kujitia ujuzi kuanza kutia makorokoro mengine.

Sasa hapo tunasema alikaa miaka hiyo tajwa,haya wewe una Mbavu za kupiiga hesabu tokea mda wa Nabii nuhu mpaka leo ni miaka mingapi KUPITIA QURAN?

Swala linarudi pale pale kwamba mimi sijapata kuona kwenye quran kwamba manabii ulowataja hasa huyo adam kwamba Aliishi miaka 6000 ilopita ndo mana siamini hayo maneno.

Wewe umepata wapi katika qurani??????
 
Imani gan??
Imani ya kutoamini kundi la wanaokubali uwepo wa mungu na imani ya kutoamini kundi la wanaokataa uwepo wa Mungu.

Wewe upo katika imani hiyo.
Mimi naipa jina ni imani ya ukati na kati.

Wewe unaweza kujiona haupo katika imani yoyote lakini ni kwa namna unavojitafsiri wewe mwenyewe na una uhiari ya kujitafsiri utakavyo pasi na kukulazimisha yeyote
 



Wewe unadhani mtukufu mtume (saw) aliposema tutafute elimu hadi China,ulidhani ni elimu ya dini??.

Wewe unadhani Pia aliposema "kutafuta elimu ni faradhi kwa kila muislamu mwanamme na mwanammke" ilikuwa ni elimu ya dini pekee??

We unadhani Qur'an tukufu ni kitabu cha kumbukumbu za miaka ya maisha ya manabii hadi tukute humo kwamba Mtume fulani na fulani waliishi miaka kadhaa!!

Hayo yanapatikana katika vitabu vya historia (taarikh) na hizo ndizo elimu alizotuagiza mtukufu mtume Muhammad (saw) tukajifunze hata ikibidi tuende China.

Baadaye nitatoa reference (rejea) ya kitabu/vitabu vya historia juu ya miaka (makadirio) aliyoishi Adam (as) hadi hii leo (zama zetu).

Angalizo:- usitukane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…