Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Mwaka 2025 kulitokea vurumai nchini Israel pale kundi la wanazuoni wa Kiebrania wajulikanao kama Haredi lilipotakiwa kujiunga na jeshi la nchi hiyo kisheria.
Hoja kubwa iliyojengwa na Serikali dhidi ya kundi hilo ni kwamba hakuna sababu inayozuia wao kujifunza mambo ya dini yao wakiwa kwenye Kambi za jeshi kwani maendeleo ya teknolojia yaliyopo yanawawezesha wao kujifunza dini yao wakiwa mahali popote.
Dini hubebwa na tamaduni ambazo kudumu kwake kulitegemea mikazo ya kisheria na makatazo yaliyotolewa bila ya kuhojiwa.
Lakini maendeleo ya teknolojia yamefanya wanadamu kuwa na chaguao (option) kwenye kuutafakari ulimwengu na mahusiano yao na Mungu.
Teknolojia imeondoa umiliki wa maarifa ya dini toka kwa wabobevu wa dini husika na maarifa hayo kwa sasa yapo kwenye miliki ya watu wote tena bila mipaka hata kwa watu wasio wa dini husika.
Leo hii vitabu vya dini zote pamoja na theojia zake zimo mitandaoni na waunga mkono au wapingaji wa falsafa za dini hizo wana nafasi sawa za kutoa maoni yao juu ya dini husika.
Jee dini zitaweza kuhimili maendeleo ya teknolojia ya zama hizi na kuendelea kubaki imara?