Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?

Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?

[
Hapa Kuna kitu unachanganya.

Dini ni nini!? Na Teknolojia ni nini!?

Dini zilianza lini na Teknolojia ilianza lini!?

Je, kwa karne zote za nyuma kulikuwa na Maendeleo ya Teknolojia!? Ndio au hapana!? Mbona hayakuathiri uwepo wa Dini!? Kwanini sasa!?

Je, kama Maendeleo yalikuwepo kwanini Bado Dini zipo mpaka sasa!?

Je, Maendeleo ya Teknolojia yamefikia tamati!? Je, kwa Maendeleo hayo Dini zipo au hazipo?
Aisee!!

Hivi maendeleo ya teknolojia yanafanana kwa nyakati zote? Jee kabla ya kuvumbuliwa Kwa Spika Adhana misikitini zilikuwa zinapigwa kama siku hizi?

Kabla ya kutengenezwa Kwa kengele wakristo walikuwa wanajulishana muda wa ibada kama Sasa?

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yamewezesha watu kuwasiliana kubadilishana maarifa kirahisi zaidi kuliko ilivyokuwa zamani.

Sasa historia inaonesha vitabu vya dini vilikuwa vipo kwa baadhi tu ya watu, lakini Sasa hakuna kitabu Cha dini yoyote kisichoko kwenye mitandao ya kijamii.

Sasa hizo teknolojia za zama hizo ambazo Bado dini ziliweza kizistahimili zinafanana na zilizopo sasa?
 
Hii mada mlipaswa muijadili katika kapu moja kihekima kabisa , ukiipasua katika mregwa wa upande mmoja ,utakinzana na hisia za ambao hawapo upande wako na hapo utazalisha kejeli , matusi na kila aina ya dhahma .

Hivyo haya yanayotokea ni mbegu ya mnacho kipanda tu , iwe kwa uzuri ama kwa ubaya .
Bwashee sio mada hii tu,hili jukwaa kwa asilimia kubwa halina muangalizi,kuna nyuzi nyingi sana watu wanatukana lakini hioni hatua zozote zinachukuliwa,mbona sisi wengine hata tukitofautiana na watu kimtazamo huwa hatutukani


Uongozi umeshindwa kusimamia nidhamu ya jukwaa
 
Huwezi kuilewa qur'an peke yake pasina hadith za Mtume,kuna mambo yameelezwa kwenye qur'an lakini ufafanuzi wake umeelezwa na Mtume Muhammad swala aallahu alaih wassalamu

mfano huyo muislamu anayesema qur'an inajitegemea muulize ALLAH kasema tuswali swala tano,je qur'an imeonyesha namna ya kuswali?

Muulize tena qur'an imesema enyi waja wa Allah mkitaka kuswali osheni nyuso zenu na vichwa vyenu,muulize je namna ya kuosha viungo vyengine je tumeelekezwa na nani?

kisha wakikujibu njoo hapa tena tujadiliane
Haya maelezo yako yanathibitisha ninachokisema. Wao wanasema kama kitu hakikuandikwa kwenye Quran basi hakipaswi kufuatwa.

Maana kwa mtizamo wao Quran ni timilifu aihitaji kuthibitishwa na Hadithi.
 
Mwaka 2025 kulitokea vurumai nchini Israel pale kundi la wanazuoni wa Kiebrania wajulikanao kama Haredi lilipotakiwa kujiunga na jeshi la nchi hiyo kisheria.

Hoja kubwa iliyojengwa na Serikali dhidi ya kundi hilo ni kwamba hakuna sababu inayozuia wao kujifunza mambo ya dini yao wakiwa kwenye Kambi za jeshi kwani maendeleo ya teknolojia yaliyopo yanawawezesha wao kujifunza dini yao wakiwa mahali popote.

Dini hubebwa na tamaduni ambazo kudumu kwake kulitegemea mikazo ya kisheria na makatazo yaliyotolewa bila ya kuhojiwa.

Lakini maendeleo ya teknolojia yamefanya wanadamu kuwa na chaguao (option) kwenye kuutafakari ulimwengu na mahusiano yao na Mungu.

Teknolojia imeondoa umiliki wa maarifa ya dini toka kwa wabobevu wa dini husika na maarifa hayo kwa sasa yapo kwenye miliki ya watu wote tena bila mipaka hata kwa watu wasio wa dini husika.

Leo hii vitabu vya dini zote pamoja na theojia zake zimo mitandaoni na waunga mkono au wapingaji wa falsafa za dini hizo wana nafasi sawa za kutoa maoni yao juu ya dini husika.

Jee dini zitaweza kuhimili maendeleo ya teknolojia ya zama hizi na kuendelea kubaki imara?
HAIWEZEKANI. Tena hizi dinimbili ndo kabisaa, Upande mmoja wanakwambia dogo Mudy alienda jelusalem na farasi anaepaa, upande wa pili blasa Ima alikufa akafufuka na akapaa mwenyewe mpaka mbinguni.
Sayansi inakataa vyote hivyo na haviwezi kuthibitishwa (ushahidi upo kwenye vitabu vyao na katuni tu).

Walivokua wanatunga dini zao hawakujua kua teknolojia itakua hivi.
 
Bwashee sio mada hii tu,hili jukwaa kwa asilimia kubwa halina muangalizi,kuna nyuzi nyingi sana watu wanatukana lakini hioni hatua zozote zinachukuliwa,mbona sisi wengine hata tukitofautiana na watu kimtazamo huwa hatutukani


Uongozi umeshindwa kusimamia nidhamu ya jukwaa
Bahati mbaya sana ndio leo umenifahamisha kuwa huku kuna uongozi bwashee, binafsi mimi ndio kiongozi wa serikali yangu nikitaka kukwepa kuona takataka yoyote huyu na tia ignore tu.
 
Sijui kwa dini nyingine,lakini kwa upande wa uislamu hakuna namna utaleta janjajanja au au sijui tekinilojia itie pua yake pale

Chochote katika Uislamu lazima ufanye rejea kwenye qur'an au sunna sahihi za Mtume au kwa masahaba waongofu,kwahiyo si tekinolijia au nyakati ambazo zitaubadilisha uislamu
ila inatokana na matumizi au mapokezi ya teknolojia, kuna watu wamekuwa waislamu na wengine imani imeongezeka kutokana na ugunduzi uliofanywa na nasa au maabara za kisayansi, mfano kuna aya inaelezea nyota inayogonga au inayongaa kama mapigo ya moyo na baadae nasa wakagundua puslar yenye sifa kama hizo, sasa hivi kuna app inayosoma quraan huku ukipewa na tafsiri na visa vya kwenye aya fulani hivyo inaonyesha faida ya teknolojia
 
[
Aisee!!

Hivi maendeleo ya teknolojia yanafanana kwa nyakati zote? Jee kabla ya kuvumbuliwa Kwa Spika Adhana misikitini zilikuwa zinapigwa kama siku hizi?

Kabla ya kutengenezwa Kwa kengele wakristo walikuwa wanajulishana muda wa ibada kama Sasa?

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yamewezesha watu kuwasiliana kubadilishana maarifa kirahisi zaidi kuliko ilivyokuwa zamani.

Sasa historia inaonesha vitabu vya dini vilikuwa vipo kwa baadhi tu ya watu, lakini Sasa hakuna kitabu Cha dini yoyote kisichoko kwenye mitandao ya kijamii.

Sasa hizo teknolojia za zama hizo ambazo Bado dini ziliweza kizistahimili zinafanana na zilizopo sasa?
Kwanza kabisa jiulize "essence(kiini)" ya Dini na Teknolojia ni nini!?

Dini ni nini!? Adhana, kengele n.k ni physical attributes za Dini na sio Dini.

Kwanini zimeishi pamoja kwa maelfu ya miaka!?

What makes it now 'special'!?

Je, tupo kwenye apex/ climax ya Maendeleo ya Teknolojia!?

Je, unaweza kutudhibitishia kwamba Maendeleo ya Teknolojia in the future hayawezi kuleta revelations zaidi ambazo hatuzifahamu kwa sasa na kuzaliwa kwa Dini mpya au kuimarika kwa Dini kongwe!?
 
😁

Haziwezi mkuu kabisa

Unakuta mtu mzima imefika mwaka 2026 ila anaaamini eti akienda mbiguni atapata thawabu ya mito ya pombe na wanawake wa kumfariji

Sasa najiuliza hio mbigu au coco beach
Kama mbinguni kuna mito ya pombe kwanini huku duniani wanakatazwa kuzitumia! Si waanze kutumia tokea huku ili wakifika kule ni muendelezo.
 
Kama mbinguni kuna mito ya pombe kwanini huku duniani wanakatazwa kuzitumia! Si waanze kutumia tokea huku ili wakifika kule ni muendelezo.
Ndio hapa unaona kuwa hizi dini ni mindgames na zinacheza katika vichwa vya wapumbavu kama ERTUGRUL BEY,

Atakupa vifungu vingi vilivyoandikwa na mwanaume mwenzake ila yeye anakuja kuviamini asilimia mia nne na vinaendssha mustakabali wa maisha yake hadi kusahau utashi wake

Akiambiwa hua huyu aanaua kweli, akiambiwa oa mtoto wa miak 10 anaoa kweli

UTAHIRA
 
Maendeleo ya technology ni MUNGU anasema: SI NILIWAAMBIA?

Wewe unaona yamekuja kupindua imani, sisi huku tunaona merging of prophecy on all fronts, yamekuja kuimarisha imani.

MUNGU WETU ALISEMA, JE HAYATOKEI KAMA ALIVYOSEMA? ? ?

TUMIA AKILI.

1)
"Basi, huyu mnyama wa pili akafanya miujiza mikubwa hata akasababisha moto kutoka mbinguni ushuke duniani mbele ya watu.

Aliwapotosha wakazi wa dunia kwa miujiza hiyo aliyojaliwa kutenda mbele ya mnyama wa kwanza. Aliwaambia wakazi wa dunia watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi tena.

Kisha alijaliwa kuipulizia uhai hiyo sanamu ya yule mnyama wa kwanza, hata ikaweza kuongea na kuwaua watu wote ambao hawakuiabudu.

Aliwalazimisha wote, wadogo na wakubwa, matajiri na maskini, watu huru na watumwa, watiwe alama juu ya mikono yao ya kulia au juu ya paji za nyuso zao.

Akapiga marufuku mtu yeyote kununua au kuuza kitu isipokuwa tu mtu aliyetiwa alama hiyo, yaani jina la yule mnyama au tarakimu ya jina hilo.

Hapa panatakiwa hekima! Mwenye akili anaweza kufafanua maana ya tarakimu ya mnyama huyo, maana ni tarakimu yenye maana ya mtu fulani. Tarakimu hiyo ni 666."

Ufunuo13.13-18.BHN


2) "
Ila sasa, Danieli, weka siri mambo hayo; kifunge kitabu na kukitia mhuri mpaka wakati wa mwisho utakapofika. Wengi watakimbilia huko na huko, na maarifa yataongezeka."
Danieli.12.4.BHN

3) Hata nyie mlioiacha imani na kujiona mna akili sana na kukumbatia dini yenu mpya ya scientism inayoamini sayansi ndo itawapa majibu ya kila kitu maishani, na kukumbatia kutafuta utajiri kama lengo la maisha yenu, hata nyie ni utimizo wa unabii. Sisi tuaminio tukiwaona tunafarijika kwani SI MUNGU WETU ALISEMA? ? JE HAYAWI?

"Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu.

Watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu.... na waovu..."

2Timothy.3.1-2.BHN


"Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana."
Mathayo.24.10.BHN



BTW hizo nchi mnazozihusudu zimeendelea sana zimejengwa na kina nani? ?


Wangekuwa washika mauzauza tangu mwanzo mnafikiri wangefika hapo? ?

Ukitaka kujua faida za mauzauza ona hali zilivyo sasa hivi huko. We have a mentally disturbed, drug consuming generation who dont even know what gender they are! ! !

Are these the people who could have built those nations? ? ?

Most seem to only get meaning in life from fighting people with meaning in life: peole with faith.

The paradox. You dont believe in something then spend your whole life consumed by it. Speaking of being mentally disturbed.


Let's hear from the founding fathers of America:

i) George Washington, Rais wa kwanza wa Marekani, alisema:

ā€œUnafanya vyema kutamani kujifunza sanaa zetu na njia zetu za maisha, na zaidi ya yote, dini ya Yesu Kristo. Mambo haya yatakufanya muwe taifa kubwa zaidi na lenye furaha kuliko mlivyo sasa.ā€

ii) John Adams, Rais wa pili wa Marekani, alisema:

ā€œKanuni za jumla ambazo mababa wa taifa walitumia kufikia uhuru zilikuwa kanuni za jumla za Ukristo Ninakiri kwamba niliamini wakati huo, na ninaamini hata sasa, kwamba kanuni hizo za jumla za Ukristo ni za milele na zisizobadilika kama vile uwepo na sifa za Mungu.ā€

iii) John Quincy Adams, Rais wa sita wa Marekani, alisema:

ā€œKatika mfululizo wa matukio ya kibinadamu, siku ya kuzaliwa kwa taifa letu imefungamanishwa bila kutenganishwa na siku ya kuzaliwa kwa Mwokozi. Azimio la Uhuru liliweka jiwe la msingi la serikali ya wanadamu juu ya kanuni za kwanza za Ukristo.ā€

iv) Maneno kutoka Azimio la Uhuru wa Marekani (Declaration of Independence):

ā€œTunashikilia ukweli huu kuwa ni wa wazi wenyewe, kwamba watu wote wameumbwa wakiwa sawa, kwamba wamepewa na Muumba wao haki fulani zisizoweza kunyang’anywa, na miongoni mwa haki hizo ni Uhai, Uhuru, na utafutaji wa Furaha... Na kwa ajili ya kuunga mkono Azimio hili, kwa kutegemea kwa uthabiti ulinzi wa Maongozi ya Kimungu (divine Providence), tunaahidiana sisi kwa sisi kutoa Maisha yetu, Mali zetu, na Heshima yetu takatifu.ā€

v) Na maneno kutoka rais wa mwisho wa Marekani, Donald Trump :2Head: (I don't believe I'm quoting this guy):

"I believe people can't be happy without religion, without that belief. Let's bring religion back. Let's bring God back into our lives".
 
Sijui kwa dini nyingine,lakini kwa upande wa uislamu hakuna namna utaleta janjajanja au au sijui tekinilojia itie pua yake pale

Chochote katika Uislamu lazima ufanye rejea kwenye qur'an au sunna sahihi za Mtume au kwa masahaba waongofu,kwahiyo si tekinolijia au nyakati ambazo zitaubadilisha uislamu
Tayari distortions zipo. Kutumia tu hii kalenda ya Gregorian ni kosa. Lakini kwa nini mnaitumia? Huoni tayari maendeleo ya teknolojia yameondoa uhalisia wenu?
Mnasheherekea maulid! birthday ha kuzaliwa mtume), hii nayo ishaondoa uhalisia
 
Lakini kwenye mitandao Sasa hivi wapo waislamu wanaokosoa mambo mbali mbali ya Uislamu ikiwa na pamoja na matumizi ya Hadithi kuisimamisha Quran.

Kwa mfano wapo wanaosema kuoa wake wengi si maamrisho ya Quran. Nadhani teknolojia iko siku itathibitisha huu mtizamo wako siyo sahihi.
Wanabisha vitu ambavyo vipo wazi. Anasema hawawezi kubadilishwa na teknolojia wakati bado wanatumia madawa ambayo yana uwezo wa kubadilisha hadi DNA.
 
Teknolojia ni upanga wenye pande mbili, upande mmoja imesaidia kuonyesha illogical , ujinga, uongo na utata wa dini, upande mwingine teknolojia hiyo hiyo imesaidia kuziremba(romanticize) dini na kuzipa muonekano mzuri wa kuvutia katika jamii.
 
Back
Top Bottom