Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?

Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?

Mwaka 2025 kulitokea vurumai nchini Israel pale kundi la wanazuoni wa Kiebrania wajulikanao kama Haredi lilipotakiwa kujiunga na jeshi la nchi hiyo kisheria.

Hoja kubwa iliyojengwa na Serikali dhidi ya kundi hilo ni kwamba hakuna sababu inayozuia wao kujifunza mambo ya dini yao wakiwa kwenye Kambi za jeshi kwani maendeleo ya teknolojia yaliyopo yanawawezesha wao kujifunza dini yao wakiwa mahali popote.

Dini hubebwa na tamaduni ambazo kudumu kwake kulitegemea mikazo ya kisheria na makatazo yaliyotolewa bila ya kuhojiwa.

Lakini maendeleo ya teknolojia yamefanya wanadamu kuwa na chaguao (option) kwenye kuutafakari ulimwengu na mahusiano yao na Mungu.

Teknolojia imeondoa umiliki wa maarifa ya dini toka kwa wabobevu wa dini husika na maarifa hayo kwa sasa yapo kwenye miliki ya watu wote tena bila mipaka hata kwa watu wasio wa dini husika.

Leo hii vitabu vya dini zote pamoja na theojia zake zimo mitandaoni na waunga mkono au wapingaji wa falsafa za dini hizo wana nafasi sawa za kutoa maoni yao juu ya dini husika.

Jee dini zitaweza kuhimili maendeleo ya teknolojia ya zama hizi na kuendelea kubaki imara?
Maendeleo ya Teknolojia yameanza Karne ya ngapi!?
 


Dalili kutoka Qur’an
1️⃣ Suratul Nisaa (4:3)
“…Basi oeni mnaowapenda katika wanawake wawili, watatu au wanne. Lakini mkihofia kuwa hamtaweza kufanya uadilifu, basi (oeni) mmoja tu…”

Hivi hapo palipoandikwa "Katika wanawake wawili, watatu au wanne" hilo neno halimaanishi sawa na "miongoni mwa wanawake wawili, watatu au wanne"?

Hiyo ndiyo unaona kama imeruhusu waislamu kuoa wake wanne?

Halafu nimeandika hapo juu kuwa siku hizi wapo baadhi ya waislamu wanakataa kutumia hadithi zozote kuisimamisha Quran. Wao wanasema Quran inajitegemea aihitaji Hadithi kuthibitisha.
 
View attachment 3534267
Huyu ni muislamu na anadai hapa kuwa uvaaji wa hijab haukuandikwa kwenye Quran.

Huyu kutokana na maendeleo ya teknolojia katao maoni yake bila ya kuhitaji hadhira maana hadhira yake iko kwenye mitandao ya kijamii.
Hijabu katika Uislamu si vazi tu, bali ni maadili yanayovaliwa kwa mwili na tabia 🌸🧕. Hapa kuna Sunna za Mtume ﷺ kuhusu hijabu, kwa dalili sahihi:
📖 Dalili kutoka Qur’an
1️⃣ Suratul Nur (24:31)
“…Na waambie wanawake Waumini waingize khimari zao juu ya vifua vyao…”
➡️ Khimari = kitambaa cha kichwa kinachoshuka hadi kifuani.
2️⃣ Suratul Ahzab (33:59)
“Ewe Nabii! Waambie wake zako, mabinti zako na wanawake wa Waumini wajisitiri kwa jilbab zao…”
➡️ Jilbab = vazi pana la nje linalofunika mwili.
📜 Sunna za Mtume ﷺ kuhusu hijabu
1️⃣ Wanawake wa Maswahaba walitekeleza haraka aya za hijabu
Aisha (RA) alisema:
“Allah awarehemu wanawake wa Answar. Ilipoteremshwa aya ya hijabu walichana vitambaa vyao wakajisitiri navyo.”
(Bukhari)
➡️ Inaonyesha utekelezaji wa haraka wa hijabu kwa kufuata Sunna.
2️⃣ Mtume ﷺ alimwambia Asmaa bint Abi Bakr (RA):
“Ewe Asmaa! Mwanamke akifika baleghe haifai kuonekana kwake isipokuwa haya na haya,”
akaashiria uso na mikono.
(Abu Dawud – baadhi ya wanachuoni wamesema hasan)
➡️ Dalili ya mipaka ya mwili unaoweza kuonekana.
3️⃣ Mtume ﷺ alisema:
“Wanawake waliovaa lakini wako uchi…”
(Muslim)
➡️ Onyo dhidi ya mavazi yanayobana, kuonyesha maumbo au kuvutia kwa makusudi.
🧭 Sifa za hijabu kwa mujibu wa Sunna
✅ Ifunike mwili mzima isipokuwa uso na mikono (kwa rai ya wengi)
✅ Isiwe nyembamba wala kubana
✅ Isiwe ya kuvutia macho kwa makusudi
✅ Isifanane na mavazi ya wanaume
✅ Isiwe kwa kujionesha (riyaa)
🌿 Hitimisho
Hijabu ni utiifu kwa Allah, heshima kwa mwanamke, na kinga ya heshima. Si mzigo, bali ni taji la heshima
 
Unakera mkuu. Huwezi kujadili mada yeyote bila kutoa baguzi za kiislamu? Mbaya zaidi unaandika matusi hovyo na kurusha picha zinazokera.

Moderators Cookie Active Paw celix YinYang Moderator 255Fixer BlackBold Boqin Bridger Fang Innovator NightCrawler Payge hebu someni post za huyu anavunja engagement rules kila siku.

Nashangaa sana kwanini hadhibitiwi. Moderators hili jukwaa mnaliharibu. Sasa imeanza kuwa kawaida kuandika matusi ovyo na wengine wanaiga.
Kiukweli kabisa jukwaa halina nidhamu kabisa,halafu ni mtandao wa kitanzania huu,hakika ni aibu kubwa sana
 
Huu upumbavu wa dini umebaki kwa waafrika na kwa baadhi ya wazungu.

Dini ni outdated lies. Zinazopigiwa promo ziendane na usasa.

Dini zitakuja kuondoka tu.

Watu hawauziwi uoga tena na stori uchwara za motoni. Wanahoji kwa kasi sana zama hizi.

Wadau wengi sana, wanaleta nyuzi za namna gani wao wenyewe au wapendwa wao wamekuwa wakimtumainia Mungu, Lakini mwisho wa siku mambo yakaenda drama.

Polepole imani kwa Mungu ina pungua. Watu wanaamka.

Watu Wanaanza kuona hizi habari za Mungu ni hadithi za danganya toto, kula kande mbichi!!
 
Teknolojia ya sasa na ya kipindi Cha nyuma ina utofauti Gani!? Teknolojia ni teknolojia tu haijalishi ya sasa au ya zamani. Labda kama unaongelea kitu kingine tofauti kabisa na teknolojia.
Kwa ivo jinsi watu wanavyowasiliana Sasa kwa teknolojia iliyopo inafanana na teknolojia iliyokuwepo kwa miaka ya 1990?
 
Huu upumbavu wa dini umebaki kwa waafrika na kwa baadhi ya wazungu.

Dini ni outdated lies. Zinazopigiwa promo ziendane na usasa.

Dini zitakuja kuondoka tu.

Watu hawauziwi uoga tena na stori uchwara za motoni. Wanahoji kwa kasi sana zama hizi.

Wadau wengi sana, wanaleta nyuzi za namna gani wao wenyewe au wapendwa wao wamekuwa wakimtumainia Mungu, Lakini mwisho wa siku mambo yakaenda drama.

Polepole imani kwa Mungu ina pungua. Watu wanaamka.

Watu Wanaanza kuona hizi habari za Mungu ni hadithi za danganya toto, kula kande mbichi!!
Zitaondoka sababu maasi yatazidi.
Ila UKWELI UTABAKI pale pale dini ndo muongozo sahihi wa binadamu KUTOKA Kwa Mungu wake.acha hyo sayansi ya juzi juzi unayoiamini wewe
 
Kiukweli kabisa jukwaa halina nidhamu kabisa,halafu ni mtandao wa kitanzania huu,hakika ni aibu kubwa sana
Hii mada mlipaswa muijadili katika kapu moja kihekima kabisa , ukiipasua katika mregwa wa upande mmoja ,utakinzana na hisia za ambao hawapo upande wako na hapo utazalisha kejeli , matusi na kila aina ya dhahma .

Hivyo haya yanayotokea ni mbegu ya mnacho kipanda tu , iwe kwa uzuri ama kwa ubaya .
 
Kwa ivo jinsi watu wanavyowasiliana Sasa kwa teknolojia iliyopo inafanana na teknolojia iliyokuwepo kwa miaka ya 1990?
Hapa Kuna kitu unachanganya.

Dini ni nini!? Na Teknolojia ni nini!?

Dini zilianza lini na Teknolojia ilianza lini!?

Je, kwa karne zote za nyuma kulikuwa na Maendeleo ya Teknolojia!? Ndio au hapana!? Mbona hayakuathiri uwepo wa Dini!? Kwanini sasa!?

Je, kama Maendeleo yalikuwepo kwanini Bado Dini zipo mpaka sasa!?

Je, Maendeleo ya Teknolojia yamefikia tamati!? Je, kwa Maendeleo hayo Dini zipo au hazipo?
 
Hivi hapo palipoandikwa "Katika wanawake wawili, watatu au wanne" hilo neno halimaanishi sawa na "miongoni mwa wanawake wawili, watatu au wanne"?

Hiyo ndiyo unaona kama imeruhusu waislamu kuoa wake wanne?

Halafu nimeandika hapo juu kuwa siku hizi wapo baadhi ya waislamu wanakataa kutumia hadithi zozote kuisimamisha Quran. Wao wanasema Quran inajitegemea aihitaji Hadithi kuthibitisha.
Huwezi kuilewa qur'an peke yake pasina hadith za Mtume,kuna mambo yameelezwa kwenye qur'an lakini ufafanuzi wake umeelezwa na Mtume Muhammad swala aallahu alaih wassalamu

mfano huyo muislamu anayesema qur'an inajitegemea muulize ALLAH kasema tuswali swala tano,je qur'an imeonyesha namna ya kuswali?

Muulize tena qur'an imesema enyi waja wa Allah mkitaka kuswali osheni nyuso zenu na vichwa vyenu,muulize je namna ya kuosha viungo vyengine je tumeelekezwa na nani?

kisha wakikujibu njoo hapa tena tujadiliane
 
Back
Top Bottom