Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?

Je dini zitaeweza kuhimili maendeleo ya teknolojia?

Huyu jamaa ELI COHEN kashapoteza heshima jamvini kwa ajili ya ujinga wake na mambo yake ya hovyo nilitaka kuita utoto ila naona ni kukosea heshima watoto kwani hata watoto hawawezi kufanya upuuzi kama huu .

Mbona Mimi najadiliana sana mada za kidini ila huwezi kunikuta nafanya ligi ya matusi na mambo ya kijinga kama huyo jamaa na wapuuzi wenzake kutoka upande wa kikiristo na kwetu sisi Waislamu jinsi wanavyofanya hapa jukwaani.

Kuanzia mada zake , majadiliano na comments zake haipo kistaarabu na mizani ya watu wanaojielewa . Unaweza kukosoa Uilsamu na ukiristo kwa staha bila hata kuleta upuuzi kama wake na wenzake.

Muda sana mods tunawaambia kudili na watu kama hawa ambao wamevuka mipaka sio kwenye lugha za kejeli tu bali mpaka wanatukanana live na kutumia picha za hovyo . Anyway mods wakina Active Cookie Payge Boqin Moderator and Maxence Melo mmeridhia jukwaa liharibiwe na wapuuzi wachache kama hao
Snowflakes
 
Kwanza nakubaliana na wewe kabisa kwamba dini bila Sheria ni kweli haziwezi kusimama

Mimi naisha dar es salaam ambacho ni kitovu cha uislam lakin ikifika ijumaa ni ngumu kujua kwa sababu siku hiyo waislam wote wanakuwa wevaa mavazi ya Simba na yanga na siku hizi hata kuswali hawasali tena

Nawapongeza wakristo kwa sasa ikifika jumapili wanasali sana

Kwahiyo uislam bila kulindwa na Sheria unaenda kupotea kabisa tunaenda kubaki na waislam majina tu
 
Sijui kwa dini nyingine,lakini kwa upande wa uislamu hakuna namna utaleta janjajanja au au sijui tekinilojia itie pua yake pale

Chochote katika Uislamu lazima ufanye rejea kwenye qur'an au sunna sahihi za Mtume au kwa masahaba waongofu,kwahiyo si tekinolijia au nyakati ambazo zitaubadilisha uislamu
Kaka uislam bila kulindwa na Sheria unaenda kupotea kabisa tunaenda kubaki na waislam majina tu

Mfano ni dar hapa uislam umepotea kabisa
 
😁

Haziwezi mkuu kabisa

Unakuta mtu mzima imefika mwaka 2026 ila anaaamini eti akienda mbiguni atapata thawabu ya mito ya pombe na wanawake wa kumfariji

Sasa najiuliza hio mbigu au coco beach
Hahaha Bar
 
Hakuna haja ya yeye kurudi kwa hao watu ikiwa utofauti wa mapokeo ya Kati ya waislam upo wazi.
Sunni na shia utofauti wao upo kwenye Nini? Kwa nini watofautiane ikiwa wote ni waislam?
Utofauti wa shia na sunni si wa kificho, unahisi wao hawaijui Quran? Kama wanaijua kwa nn wanatofautiana?

TOFAUTI YA SUNNI NA SHIA KATIKA UISLAMU

Utangulizi

Uislamu ni dini moja iliyojengwa juu ya misingi mikuu ya Tauhid, kuamini Qur’an Tukufu, Mtume Muhammad ﷺ, Malaika, Vitabu vya Allah, Mitume, Siku ya Mwisho na Qadari. Hata hivyo, ndani ya Umma wa Kiislamu kuna makundi mawili makubwa yanayojulikana kama Sunni na Shia. Tofauti zao haziko katika msingi wa dini, bali zaidi zinatokana na masuala ya kihistoria, uongozi wa Umma baada ya kufariki kwa Mtume ﷺ, na baadhi ya misimamo ya kifiqhi na kiitikadi.
Makala hii inalenga kueleza tofauti hizi kwa lugha nyepesi, yenye uadilifu na bila chuki, ili kuongeza uelewa na kuimarisha umoja wa Waislamu

Asili ya mgawanyiko wa Sunni na Shia
Baada ya kufariki kwa Mtume Muhammad ﷺ mwaka 632 CE, Maswahaba walikabiliwa na swali muhimu: nani angeongoza Umma wa Kiislamu?

🔹 Sunni waliamini kuwa kiongozi achaguliwe kwa mashauriano (shura), ndipo Abu Bakr (RA) akawa Khalifa wa kwanza.

🔹 Shia waliona kuwa Ali bin Abi Talib (RA), ambaye alikuwa binamu na mkwe wa Mtume ﷺ, ndiye aliyekuwa na haki zaidi ya uongozi, na kwamba uongozi unapaswa kubaki ndani ya familia ya Mtume ﷺ (Ahlul Bayt).

Hapo ndipo ulipoanza mgawanyiko wa kihistoria ambao baadaye ulijikita pia katika masuala ya elimu ya dini, fiqhi na itikadi.

Maana ya Sunni na Shia

🔹 Sunni linatokana na neno Ahlus-Sunnah wal-Jama’ah, yaani watu wanaofuata Sunna ya Mtume ﷺ na umoja wa Waislamu.

🔹 Shia ni kifupi cha Shiat Ali, yaani wafuasi wa Ali bin Abi Talib (RA).
Majina haya yanabeba historia, siyo uadui, bali mitazamo tofauti juu ya uongozi wa Umma.

Vyanzo vya dini na elimu

Sunni
Wanategemea: ✔ Qur’an Tukufu
✔ Sunna ya Mtume ﷺ kupitia Hadithi zilizopokelewa na Maswahaba wengi
✔ Ijma’ (makubaliano ya wanazuoni)
✔ Qiyas (kulinganisha)

Shia
Wanategemea: ✔ Qur’an Tukufu
✔ Hadithi nyingi kupitia Ahlul Bayt wa Mtume ﷺ
✔ Mafundisho ya Maimamu wa kizazi cha Mtume ﷺ

Tofauti hii imezaa madhehebu tofauti ya fiqhi na mitazamo ya kiitikadi.

Mtazamo kwa Maswahaba na Ahlul Bayt
🔹 Sunni: Wanawaheshimu Maswahaba wote kwa ujumla, wakiamini walikuwa watu bora waliobeba Uislamu hadi kwa vizazi vilivyofuata.

🔹 Shia: Wanawaheshimu sana Ahlul Bayt wa Mtume ﷺ, na wana mtazamo wa tofauti kwa baadhi ya Maswahaba, hasa kuhusu masuala ya uongozi baada ya Mtume ﷺ.

Hata hivyo, pande zote mbili zinawakubali Ahlul Bayt kuwa watu watukufu na wa karibu sana na Mtume ﷺ
Tofauti za kiitikadi

🔹 Sunni: Wanaamini uongozi wa Umma ni wa kibinadamu na kisiasa, siyo sehemu ya msingi wa itikadi ya dini.

🔹 Shia (hasa Ithna Ashari): Wanaamini Imamah (uongozi wa Maimamu) ni sehemu ya msingi wa dini, na Maimamu hawa wanahifadhiwa na makosa katika masuala ya dini.

Hii ndiyo tofauti kubwa zaidi ya kiitikadi kati ya makundi haya mawili.

Tofauti za kifiqhi na kiibada

Zipo tofauti ndogo katika baadhi ya ibada, mfano: ✔ Namna ya kushika mikono wakati wa Swala
✔ Kuunganisha baadhi ya Swala
✔ Baadhi ya hukumu za ndoa na ibada
Lakini Swala, Saumu, Zaka na Hija ni wajibu kwa wote

Maeneo wanakopatikana kwa wingi
🔹 Sunni: Wengi duniani (takribani 85–90% ya Waislamu), hupatikana kwa wingi Afrika, Asia ya Kusini, Mashariki ya Kati na Asia ya Kusini Mashariki.

🔹 Shia: Wengi hupatikana Iran, Iraq, Azerbaijan, Bahrain na sehemu za Yemen.

Msingi wa umoja kati ya Sunni na Shia
Licha ya tofauti zao, wote: ✔ Wanamwamini Allah Mmoja
✔ Wanamfuata Mtume Muhammad ﷺ
✔ Wanaiamini Qur’an Tukufu
✔ Wanakabili Qibla kimoja
✔ Wanaswali Swala tano
✔ Wanahiji Makka

Hivyo, tofauti zao hazipaswi kuwa sababu ya chuki, bali fursa ya kujifunza, kuheshimiana na kuimarisha umoja wa Uislamu

Hitimisho
Tofauti ya Sunni na Shia ilianza kama suala la uongozi wa Umma baada ya Mtume ﷺ, kisha ikaenea katika maeneo ya fiqhi na itikadi. Hata hivyo, misingi mikuu ya Uislamu inabaki kuwa mmoja. Kilicho muhimu zaidi kwa Waislamu leo ni kushikamana na Qur’an, Sunna, maadili ya udugu na amani, na kuepuka migawanyiko inayodhoofisha Umma.
“Hakika Waumini ni ndugu.” (Qur’an 49:10)
 
Dini ingekuwa ndio muongozo sahihi wa binadamu, Kusingekuwa na haja ya kuanzishwa mahakama, Magereza, sheria na haki za kuongoza na kulinda maisha ya mwanadamu.

Dini zilifeli toka kitambo, ndio maana ikaonekana ipo haja ya kutungwa sheria na haki za binadamu kuleta MUONGOZO sahihi wa maisha ya mwanadamu duniani.

Hakuna Mungu.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo.
Mbona sharia za kiislam zipo ila mnazikataa ushasahau?
Sheria za mungu zipo ila mnazikataa ushasahau?
 
Vipi kwa wale waliokufa kabla ya dini kuwafikia? Wao muongozo sahihi kwao ulikia ni upi?
Kila mtu ataulizwa na kuhukumiwa KUTOKA na KUFIKIWA AU KUTOKUFIKIWA NA UJUMBE WA ALLAH.
umma wowote haukuangamizwa mpaka ulipopelekewa mjumbe.kwa hyo watajibu kama hawajafikiwa na watasamehewa.vipi wewe haujafikiwa na ujumbe wa mungu
Vipi kwa wale waliokufa kabla ya dini kuwafikia? Wao muongozo sahihi kwao ulikia ni upi?
 
Kila mtu ataulizwa na kuhukumiwa KUTOKA na KUFIKIWA AU KUTOKUFIKIWA NA UJUMBE WA ALLAH.
umma wowote haukuangamizwa mpaka ulipopelekewa mjumbe.kwa hyo watajibu kama hawajafikiwa na watasamehewa.vipi wewe haujafikiwa na ujumbe wa mungu
Hoja yangu ni kwamba Mungu hawezi kuhukumu sababu ya dini yako. Kwa kuwa kuna mamilion waliokufa kabla ya dini
 
Castle_Lite njoo uone huku hivi tunavyoshinda makanisani tunasema "napokeeaaa” wakati wajapan wanakesha wakitengeneza magari si ni sawa tu?

Anyways tunapokea kwa imani..

Shem Seran za ww.
Sorry siku 2 hizi i was busy busy sana. Ndio naingia JF muda huu.

Hope weekend yako ilikuwa poa.
 
Watu wanaangamia sana na kuwa brainwashed, ata kama unaamini hakuna haja ya kuwa hivyo🙆🏽‍♀️

Imani hubadilisha akili yako, tabia zako, na maamuzi yako.

Wanaoenda kwa hawa apostles . Mara zote wanaenda ili kupata nguvu ya imani kwasababu atakuwa ameambiwa na rafik au jamaa ake kuwa kwa apostle flan kuna upako. Na ushuhuda wa waliofanikiwa.

Kama huna imani. Hata ungeenda kwa TB Joshua kipind kile. Haufanikiwi.

Kwahiyo ni namna Iman yako inavyojengeka kupitia Kiongoz flan wa dini. Ambaye unamuamini na anayeaminika na watu wako wa karibu.
 
Imani hubadilisha akili yako, tabia zako, na maamuzi yako.

Wanaoenda kwa hawa apostles . Mara zote wanaenda ili kupata nguvu ya imani kwasababu atakuwa ameambiwa na rafik au jamaa ake kuwa kwa apostle flan kuna upako. Na ushuhuda wa waliofanikiwa.

Kama huna imani. Hata ungeenda kwa TB Joshua kipind kile. Haufanikiwi.

Kwahiyo ni namna Iman yako inavyojengeka kupitia Kiongoz flan wa dini. Ambaye unamuamini na anayeaminika na watu wako wa karibu.
Hahaa umenikumbusha mchungaji mmoja aliwahi kusema ata kama mchungaji wako aombe huku anawaka moto ni kazi bure pasipo imani..
 
Hoja yangu ni kwamba Mungu hawezi kuhukumu sababu ya dini yako. Kwa kuwa kuna mamilion waliokufa kabla ya dini
Sawa hao watalipwa pia.
Ndo maana mungu alileta mitume na manabii kuwa wajumbe wake.sasa kama hawakufikiwa na huo ujumbe sio kosa lao.hawana Cha kujibu .ila kama mjumbe aliwafikia wakambishia wanalo.la kujibu
 
Sijui kwa dini nyingine,lakini kwa upande wa uislamu hakuna namna utaleta janjajanja au au sijui tekinilojia itie pua yake pale

Chochote katika Uislamu lazima ufanye rejea kwenye qur'an au sunna sahihi za Mtume au kwa masahaba waongofu,kwahiyo si tekinolijia au nyakati ambazo zitaubadilisha uislamu
Nipe rejea ya wewe kutumia jamii forum
 
Neil deGrasse Tyson’s quote, "God is an ever-receding pocket of scientific ignorance." As science and technology advance, umuhimu wa Mungu na dini unazidi kupungua.
 
Hizi ndio maada za msingi kuzizungumzia..
Buti Dini ya kweli ya mungu itabaki imara, haidhuru nini kitakuja.
 
Back
Top Bottom