Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Duh! kwa bahat mbaya ni kweli japo kuwa kwenye posts nyengine angalau kuna matumizi ya herufi kubwa baada ya full stop.

Uandishi wake wa leo unaweza kukataa kuwa ni mtu aliyemaliza chuo kikuu achilia mbali mtu anaegombea nafasi ya uraisi.



Nadhani aliandika kwa mkono mmoja,nimemuona anatumia mkono mmoja kuandika kwa kipindi hiki alichokuwa mgonjwa,embu tusubiri tuone,lakini je? is it the first time kuandika hapa JF?na kama no how was it
 
Kuona tatatizo kwa mtu unayempenda na kumkosoa kabla adui hajamuona na kumsema yaliyokuwa makubwa,mazito na mabaya huo ndo uungwana. Lakini pia kama upogo unaonekana kwa huyo umpendaye na wewe unauita jambo dogo na kuacha kusahihisha bila shaka unakuwa ukimuandaa kuwa kichekesho mbele ya wengi. Tuungane kusahihisha yaliyo tenge na wala kufanya hivyo kusitafsirike kuwa na 'beef' dhidi ya upinzani!........................a say....
 

Binafsi nafikiri gazeti la Raia mwema lilitoa makala hii ili kukidhi uhuru wa mawazo kuliko kudhani vinginevyo kama ilivyo hapa Jamiiforums.
 
Weka pingamizi dhidi yake ili wewe ndio uonekane kilaza


Jamani hizi nembo za bendera za vyama vya siasa zinatafuta nini humu. JF halina dini, chama wala kabila. Kila mtu akiamua kuweka nembo ya bendera ya chama chake itakuwa virugu tupu. Ni mawazo yangu tu.
 
Slaa ni mtoto wa nyerere hana jipya :huyu ni ccm , akipata madaraka tutarudi zile enzi za nyerere kukaa foleni ya sigara . Hivi karibuni aliutembelea mzimu wa nyerere kule dodoma . Huyu mtu ni hatari sana .
.

Hata mimi niliwahi kulifikiria hilo. Ni wale wale tu kwa gamba jingine.
 
Siamini kama mhariri wa raia mwema anaweza kuruhusu upupu huu kuandikwa na gazeti makini kama hilo! Isijekuwa Rostam kesha nunua na raia mwema.
Mbona Gazeti la Tanzania Daima linaruhusu kuandika upupu huo huo katika makala ya Maswali magumu ya Ansbert Ngurumu. Upupu ni mbaya sana hata hapa JF umeanza kila mtu anamwaga kila jambo hata bila utafiti.
 
.

Ni Propaganda za kisiasa tu, kama Dr Slaa aliona mshahara wa wabunge ni mkubwa mbona aliyendelea kuupokea? alikuwa anatafuta umaarufu bila shaka. Nina imani naye kuwa mbunge lakini sina imani naye kuwa Rais.
 
.

Naamini makala hiyo haijatumika kidini (uislamu kuushambulia ukristo) dhidi ya Dr Slaa kama ambavyo Ansbert Ngurumo hatumiki kidini (ukristo kuushambilia Uislamu) kumshambulia Kikwete katika gazeti la Tanzania Daima

Ndugu, sio kikwete aliyeweka mahakama ya kadhi katika ilani ya uchaguzi. Mgombea hashirikishwi katika kuandaa ilani ya chama bali ni chama chenyewe chini ya secretarieti ya chama. Muundo wa secretarieti unawashirikisha wakristo na waislamu. Ilani ya uchaguzi sio ya mgombea ni ya chama.

Kikwete hawezi kama kikwete pekee kuwaahidi waislamu Mahakama ya kadhi au OIC. Masuala hayo yapo muda mrefu tangu enzi za marais Wakristo na Waislamu (Nyerere, Mwinyi na Mkapa). Hili ni suala tata kikatiba lakini pia ni suala la imani kwa Waislamu linazungumzika badala ya kutufarakanisha. Hili suala ni la watanzania wote bila kujali dini kwa maana kwamba nchi hii ni ya dini zote.

Wakristo na Waislamu ni ndugu moja kwa baba yao Ibrahimu na mama tofauti Sarah na Hajira. Kumbuka kwa baba huyo uzao wa Sarah ndio Ukristo na uzao wa Hajira ni ndio Uislamu. Bila kuvunja katiba ndio maana serikali imepeleka hoja kwa Waislam kwamba mahakama hiyo ikiundwa ndani ya taasisi zao waislamu inaweza kupunguza mgogoro wa kikatiba. Ni vyema tuvute subira huku tukitoa michango itakatusaidia kuishi kama ndugu wa baba mmoja Ibrahim ambaye ukoo wake kwa Yesu na Ismael ulileta dini hizi mbili.

kama ambavyo katiba inatambua kuwepo kwa madhehebu ya dini ndivyo ndugu zetu waislamu nao wanaomba suala hilo kupitiwa upya. mahakama ya kadhi ipo katika kitabu kitakatifu cha Kuran hivyo ni jambo la imani kama ilivyo kwa sheria na kanuni mbalimbali katika kitabu kitakatifu cha Bibilia. Sio jambo jepesi hivyo kushughulikia jambo la kidini na hasa kama limeandikwa katika moja ya vitabu hivyo. bila jaziba tushirkiane kuishauri serikali kwa manufaa yetu wote.
 
.

Gazeti la Raia mwema limekuwa na kawaida ya kuandika makala mbalimbali dhidi ya Kikwete hakuna aliyelalamika lakini gazeti hilo linapoweka mizania sawa ya kuandika kwa wagombea wote imekuwa nongwa. Dr Slaa asiguswe lakini Kikwete ni halali kumsema kwa kila jambo hata ambalo halina utafiti wa kutosha. Binafsi naona tupeane uhuru wa kutoa mawazo yetu kwa wagombea wote
 
.

makala hiyo ilikuwa ni maoni ya mwandishi na ndio maana ni makala huru na mwandishi wake ni Chovenye Kipunde wenye email kchovenye@yahoo.com. mwandishi huyo amejitambulisha kuwa ni msomaji wa muda mrefu wa gazeti la raia mwema. Gazeti la Raia mwema wanadai wameyachapisha maoni hayo kwa sababu, pamoja na mambo mengine, ndani ya toleo hilo kuna mahojiano maalum ya Dr Wilbraod Slaa ambayo mengine yanagusia maoni ya msomaji huyo. Naamini hawakuwa na makusudi nyingine ila kumjua Dk Slaa kwa undani zaidi kama atatufaa kwa nafasi kubwa ya Urais.
 

Tukizungumzia kwamba wengine wametumwa hapa basi hakuna atakayesalimika. kila mmoja wetu ana mtu wake katika uchaguzi ujao hivyo acha kila mtu awe huru kuchangia. Hapa wapo wa CCM na Chadema. Hakuna aliyetumwa au pandikizi wote ni watanzania tunajenga nyumba moja kila mtu abebe tofali moja kukamilisha ujenzi huo.
 
Humu ndani kuna watu wapo kwa ajili ya kudivert hoja sasa ukishajua huyo ni mmoja wao, hata akiku-quote unamshit! Au unautumia uhuru wako vema una update ignore list kwa kumuongeza, nalohili lahitaji wawekezaji au uhisani wa watu wa marekani! Mbona rahisi! Mjue wenzenu wanafurahi kuona mnavyohangaika kuumiza vichwa kuwajibu wakati wao hata hawajui wanaandika nini mradi wamebinya keyboard!
Chukua hatua hakuna aliyetumwa humu kila mtu kajituma ila tunatofautiana uwezo wa kufikiri, wengine uwezo wao wa kutumwa na wengine wa kutuma, wa kutumwa hata asipotumwa ni sawa kuwa katumwa tu unampotezea kwani hata umri na elimu yake hujui vinaweza vikawa vinamruhusu kufikiria anavyofikiri! Na ungejua hata usingethubutu kumjibu ila ungemcheka!
 
Jamani hizi nembo za bendera za vyama vya siasa zinatafuta nini humu. JF halina dini, chama wala kabila. Kila mtu akiamua kuweka nembo ya bendera ya chama chake itakuwa virugu tupu. Ni mawazo yangu tu.
Na wewe weka ya chama chako hakuna shida. Hapa tunaruhusiwa kuandika hata majina yetu halisi. Hatukatazwi.

Hii isikupe shida hii ndiyo avtar yangu
 
Ukweli ni kwamba:

1. Kweli makala ilitoka ... lakini kwenye toleo hilo hilo ilikuweko makala nyingine nzuri sana. Na jambo la msingi ni kuwa mhariri alitoa dokezo kwa nini ameitoa hii makala tunayoisoma hapa. Alisema ameitoa ili iende sambamba na makala niyingine ndefu iliyokuwa katikati ya gazeti hilo....bahati mbaya siipati kwnye mtandao..

2. Lakini makala yenyewe ni very positive .... ianyondeana na mtizamo halisi wa wahariri wa Rai Mwema.

3. Nilimuelwa kuwa kama angekataa kuitoa makala tunayosoma hapa alafu akaitoa ile nyingine.... angeonekana kuwa amekaa upande mmoja ...hivyo kwa kujiamini...azkazitoa zote.... LAZIMA KUZISOMA ZOTE PAMOJA ILI KUPATA MAANA KAMILI!!!!
 


malaria sugu yuko wapi?
 

Regina mtema yuko makao makuu ya chadema. Bila kuzingatia ushawishi wake kisiasa wameona akagombee tu na matokeo yake kumbe ni mgombea dhaifu. Kufanya kazi kwake makao makuu ya chama ndio imekuwa kigezo cha kumpa kugombea. Wagombea kama hawa wakishindwa utakuta anatafutwa mchawi na mchawi huyo atakuwa CCM. kwa sasa CCM ina wabunge 21 waliopita bila kupingwa na madiwani 236 waliopita bila kupingwa. katika soka tunaita ushindi wa mapema ambapo mabeki wa timu pinzani hawakuweka ngome ya kutosha kuzuia kufungwa mapema mapema.
 

Hajatumwa anatoa mawazo na mtazamo wake katika hoja iliyo mbele yetu na hiyo ndio demokrasia yenyewe. Demokrasia ina pande mbili, utamu na uchungu. Ukitaka demokarsia hiyo iwe chungu kwa kikwete na tamu kwa Dk. Slaa ni bora ujiondoe mwenyewe kwenye jukwaa hili huru.....acha watu wakosoane kwa pande zote za utamu na uchungu kwa wagombea wote. Hii ndio gharama ya kushabikia kampeni za kihuni bila hoja za msingi.
 

Kiranga hajagombea Urais hata akiandika kiingereza kibovu inakubarika kwa kiwango chake cha elimu lakini pia hana PHD kama Dk. Slaa. Tusilinganishe vitu visivyofanana wakati tunatafakari namna ya kupata Rais bora kwa nchi yetu.
 

kuna siku niliwaambia kwamba hapa JF kila mtu na fani yake kama ambavyo ACID anatamba hapa JF na fani ya sayansi hasa chemistry somo ambalo sikuwahi kufanya vizuri. Kiranga ni mtaala wa lugha kaona mapungufu ya kiingereza cha mgombea Urais wetu Dk Slaa kwa nini hatumpi fursa akatoa dukuduku lake. Fani zina wenyewe na ukizichezea wenye fani hizo hawawezi kukaa kimya. Ni bora tukubaliane tu kwamba Dk Slaa akaongeze uelewa katika somo la kiingereza kuliko kujidanganya kwamba mgombea huyo anajua kila kitu kwa ufasaha.
 

Kama umemuelewa kiranga anasema wembe ni ule ule kama unavyomvyoa kikwete hauna budi kumnyoa pia na Dk. Slaa. Angekuwa ni kikwete kaambiwa hajui kiingereza hakuna ambaye angejitokeza kumtetea na kama angejitokeza basi angeambiwa katumwa. Acheni group thinking kila mtu ajitegemee kwa hisia zake dhidi ya wagombea.

nisingependa kutaja watu kwa majina kwa vile hata kabla sijawataja na wao wanajijua. Ili ukubarike kwenye kundi la watu hawa hapa JF basi mkosoe sana kikwete huku ukimsifia mgombea yoyote wa upinzani na hasa Dk. Slaa. mtindo huu wa fikra mgando umejaa kuvunja kanuni za haki na uhuru wa binadamu kujieleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…