Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Duh! kwa bahat mbaya ni kweli japo kuwa kwenye posts nyengine angalau kuna matumizi ya herufi kubwa baada ya full stop.

Uandishi wake wa leo unaweza kukataa kuwa ni mtu aliyemaliza chuo kikuu achilia mbali mtu anaegombea nafasi ya uraisi.



Nadhani aliandika kwa mkono mmoja,nimemuona anatumia mkono mmoja kuandika kwa kipindi hiki alichokuwa mgonjwa,embu tusubiri tuone,lakini je? is it the first time kuandika hapa JF?na kama no how was it
 
Kama umeelewa hili utaelewa maana ya constructive criticism, na kwa nini mtu aki criticize upinzani maana yake si lazima awe hapendi upinzani.

Na kama Nyerere alivyo blast CCM na baadaye kumkampainia Mkapa, ndivyo hivyo hata mimi na blast CHADEMA lakini bottom line nasema "VOTE SLAA"

Au na hili nalo hujaliona? Hizi criticism kutoka kwangu zinatakiwa kumuandaa Slaa na CHADEMA, na wala hazina lengo baya.

Tukikataa constructive criticism hatutajifunza, tusipojifunza hatutakua.
Kuona tatatizo kwa mtu unayempenda na kumkosoa kabla adui hajamuona na kumsema yaliyokuwa makubwa,mazito na mabaya huo ndo uungwana. Lakini pia kama upogo unaonekana kwa huyo umpendaye na wewe unauita jambo dogo na kuacha kusahihisha bila shaka unakuwa ukimuandaa kuwa kichekesho mbele ya wengi. Tuungane kusahihisha yaliyo tenge na wala kufanya hivyo kusitafsirike kuwa na 'beef' dhidi ya upinzani!........................a say....
 
..kama makala hii imetoka kwenye gazeti la RAIA MWEMA basi tumekwisha.

..mwandishi wa makala anajikanyaga-kanyaga kiasi hicho na mhariri bado anaruhusu iwe published.

..hii makala imejaa udini, na kitu cha kutisha zaidi ni kwamba imetolewa kwenye gazeti la mtu anayeheshimiwa sana na jamii ya wa-Tanzania, Jenerali Ulimwengu.

Binafsi nafikiri gazeti la Raia mwema lilitoa makala hii ili kukidhi uhuru wa mawazo kuliko kudhani vinginevyo kama ilivyo hapa Jamiiforums.
 
Weka pingamizi dhidi yake ili wewe ndio uonekane kilaza


Jamani hizi nembo za bendera za vyama vya siasa zinatafuta nini humu. JF halina dini, chama wala kabila. Kila mtu akiamua kuweka nembo ya bendera ya chama chake itakuwa virugu tupu. Ni mawazo yangu tu.
 
Slaa ni mtoto wa nyerere hana jipya :huyu ni ccm , akipata madaraka tutarudi zile enzi za nyerere kukaa foleni ya sigara . Hivi karibuni aliutembelea mzimu wa nyerere kule dodoma . Huyu mtu ni hatari sana .
.

Hata mimi niliwahi kulifikiria hilo. Ni wale wale tu kwa gamba jingine.
 
Siamini kama mhariri wa raia mwema anaweza kuruhusu upupu huu kuandikwa na gazeti makini kama hilo! Isijekuwa Rostam kesha nunua na raia mwema.
Mbona Gazeti la Tanzania Daima linaruhusu kuandika upupu huo huo katika makala ya Maswali magumu ya Ansbert Ngurumu. Upupu ni mbaya sana hata hapa JF umeanza kila mtu anamwaga kila jambo hata bila utafiti.
 
Pamoja na yote yaliosemwa lakini mimi bado na imani kubwa na dk slaa, tokea aliposimama bungeni nakuomba mishara ya wabunge ipunguzwe kwani mikubwa mno kulingana na wananchi wa kawawaida. Kitendo kile kimenifanya nione huyu kweli yupo pale kwa ajili ya wananchi na sikitu kingine,kwa hiyo hata akipewa nchi me poa tu!
.

Ni Propaganda za kisiasa tu, kama Dr Slaa aliona mshahara wa wabunge ni mkubwa mbona aliyendelea kuupokea? alikuwa anatafuta umaarufu bila shaka. Nina imani naye kuwa mbunge lakini sina imani naye kuwa Rais.
 
-kama zile hadithi nilizozoea za hapo zamani za kale....
-umwkubali kutumika kisiasa na ccm na umekubali kutumika kidini na kikwete na uislamu..................pole sana
-unazungumzia sokoine na nyerere wakati tunamzungumzia rais dhaifu kabisa kuwahi kutokea yaani kikwete
-mpaka sasa huamini kuwa kikwete aliweka dini ya kiislamu mbele kwa kuweka mambo ya mahakama ya kadhi kwenye ilani ya ccm na kuitetea, hili ni suala la wazi
-kuna swala ambalo halijawahi kujificha na wala kukanushwa na waislamu baada ya ule moto na fukuto waliloonesha juu ya kuondoia mambo yao ya kipuuzi ya oic na mahakama ya kadhi waliposema hawatampiogia kura kikwete na ccm lakini aliwaita wazee ambao wanasambaza habari kwa usiri mkubwa baada ya kuwaahidi kutumia mamlaka atakayokuwa nyo kwa namna yoyote kufanya hiyo mahakama ya kikafiri iwepo kikatiba....
-wanasubiri tu kikwete achaguliwe maana ndivyo walivyoambiwa wasubiri kwani mambo mazuri hayataki haraka kwa mujibu wa kikwete
-mwandishi anajaribu kutumia mgongo wa kuwa alikuwa padre...hiyo ni kitu tofauti ila kwa kikwete ameonesha kwa vitendo...rais wa nchi huwezi kukaa kimya katiba ya nchi inachezewa na wajinga eti kuweka mambo ya dini...ndiyo maana waasisi wa taifa hili baada ya kuwa na mtazamo wa mbali waliamua kuondoa upumbavu huo maana mtu kama mimi siko tayari kodi yangu itumike kumlipa kafiri mshahara eti kwa kuwa mahakama ya kadhi...
-slaa na wakristo kwa ujumla ni watu wa kutafuta amani kwanza hata akichaguliwa kwanza hawezi kuruhusu bunge kuamua kupoteza muda kujadili upuuzi wa kadhi na kuacha mambo ya msingi ya kuwainua watu kiuchumi naamimini hatakaa kimya kwani ni upumbavu kujadili na kupoteza mudfs ikiwemo kuwapa posho wabunge kwa kujadili mambo ya dini
-NAAMINI TUMEELEWANA
.

Naamini makala hiyo haijatumika kidini (uislamu kuushambulia ukristo) dhidi ya Dr Slaa kama ambavyo Ansbert Ngurumo hatumiki kidini (ukristo kuushambilia Uislamu) kumshambulia Kikwete katika gazeti la Tanzania Daima

Ndugu, sio kikwete aliyeweka mahakama ya kadhi katika ilani ya uchaguzi. Mgombea hashirikishwi katika kuandaa ilani ya chama bali ni chama chenyewe chini ya secretarieti ya chama. Muundo wa secretarieti unawashirikisha wakristo na waislamu. Ilani ya uchaguzi sio ya mgombea ni ya chama.

Kikwete hawezi kama kikwete pekee kuwaahidi waislamu Mahakama ya kadhi au OIC. Masuala hayo yapo muda mrefu tangu enzi za marais Wakristo na Waislamu (Nyerere, Mwinyi na Mkapa). Hili ni suala tata kikatiba lakini pia ni suala la imani kwa Waislamu linazungumzika badala ya kutufarakanisha. Hili suala ni la watanzania wote bila kujali dini kwa maana kwamba nchi hii ni ya dini zote.

Wakristo na Waislamu ni ndugu moja kwa baba yao Ibrahimu na mama tofauti Sarah na Hajira. Kumbuka kwa baba huyo uzao wa Sarah ndio Ukristo na uzao wa Hajira ni ndio Uislamu. Bila kuvunja katiba ndio maana serikali imepeleka hoja kwa Waislam kwamba mahakama hiyo ikiundwa ndani ya taasisi zao waislamu inaweza kupunguza mgogoro wa kikatiba. Ni vyema tuvute subira huku tukitoa michango itakatusaidia kuishi kama ndugu wa baba mmoja Ibrahim ambaye ukoo wake kwa Yesu na Ismael ulileta dini hizi mbili.

kama ambavyo katiba inatambua kuwepo kwa madhehebu ya dini ndivyo ndugu zetu waislamu nao wanaomba suala hilo kupitiwa upya. mahakama ya kadhi ipo katika kitabu kitakatifu cha Kuran hivyo ni jambo la imani kama ilivyo kwa sheria na kanuni mbalimbali katika kitabu kitakatifu cha Bibilia. Sio jambo jepesi hivyo kushughulikia jambo la kidini na hasa kama limeandikwa katika moja ya vitabu hivyo. bila jaziba tushirkiane kuishauri serikali kwa manufaa yetu wote.
 
Wakati huu tutasikia na kuona mengi! Kwa makala hii inanifanya nianze kuwa na mtazamo tofauti na nilivyomdhania Jenerali Ulimwengu! Hofu mojawapo ya mwandishi ni eti nchi itatawaliwa na kanisa kana kwamba hii ni mara ya kwanza kuchagua Rais Mkristo! Cha ajabu zaidi nii pale Rais mwema wanaposhindwa kutofautisha taasisi na mtu binafsi. Urais ni taasisi inayoongozwa na katiba na sheria, Unachokisema wewe ni kama kwamba Dr Slaa atasimama barabarani na rungu kubwa kuwawinda wasitii mamlaka ya kanisa!
Tunacholilia Tanzania ni kujenga demokrasia ya kuwakataa wote wababaishaji, Wala watz sio marobott ya kugeuzwa geuzwa kwa remote Dr Slaa atapimwa kwa mizani ile ile iliyompimia Kikwete na ikiwa haenendi sawa sawa tutamtapika pia!
Mwanzoni wa utawala wa kikwete Cartoon moja ilionekana kwenye magazeti ya Kenya waandishi wa Tz wanamlamba miguu Mhe! Leo hii hakuna kitu kitu kama hicho labda wachache wanaojipendekeza kama Raia mwema na magazeti ya serikali. Why? Kwa sababu mwanaume hasifiwi kwa sura!
.

Gazeti la Raia mwema limekuwa na kawaida ya kuandika makala mbalimbali dhidi ya Kikwete hakuna aliyelalamika lakini gazeti hilo linapoweka mizania sawa ya kuandika kwa wagombea wote imekuwa nongwa. Dr Slaa asiguswe lakini Kikwete ni halali kumsema kwa kila jambo hata ambalo halina utafiti wa kutosha. Binafsi naona tupeane uhuru wa kutoa mawazo yetu kwa wagombea wote
 
Mwafrika,
Inawezekana Jenerali ameacha ichapishwe kwa sababu ni maoni ya mwandishi.(column) Haikuandikwa kama news item. Lakini kosa walilofanya ni kuondoa jina la mwandishi na kutoonyesha kuwa ni op-ed (opinionated editorial which it is) I would have done the same but would have made sure my readers understand this is an op-ed.
.

makala hiyo ilikuwa ni maoni ya mwandishi na ndio maana ni makala huru na mwandishi wake ni Chovenye Kipunde wenye email kchovenye@yahoo.com. mwandishi huyo amejitambulisha kuwa ni msomaji wa muda mrefu wa gazeti la raia mwema. Gazeti la Raia mwema wanadai wameyachapisha maoni hayo kwa sababu, pamoja na mambo mengine, ndani ya toleo hilo kuna mahojiano maalum ya Dr Wilbraod Slaa ambayo mengine yanagusia maoni ya msomaji huyo. Naamini hawakuwa na makusudi nyingine ila kumjua Dk Slaa kwa undani zaidi kama atatufaa kwa nafasi kubwa ya Urais.
 
Mozze,

Waogopeni sana watu wa aina ya Anti-sijui nini!

Hawa ni wa kuja na kuondoka hawa!...Amekuja kikazi hapa na ni pandikizi la watu au mabwana wanaomlipa nusu-na-robo ya unga!..
Anamtumikia kafiri apate mradi wake!...
Hapa anachotaka ni kuchokonoa ili tuweke wazi baadhi ya mbinu tunazotumia, then acopy na ku-paste kwenye genge lao...
Hatudanganyiki ati broda!.

Akamwambie mume wake kwamba amegonga mwamba!..Mambo yote aliyosema hapo kwenye post yake ni kama liquid inayopatikana katika shimo la choo!..huh!

Tukizungumzia kwamba wengine wametumwa hapa basi hakuna atakayesalimika. kila mmoja wetu ana mtu wake katika uchaguzi ujao hivyo acha kila mtu awe huru kuchangia. Hapa wapo wa CCM na Chadema. Hakuna aliyetumwa au pandikizi wote ni watanzania tunajenga nyumba moja kila mtu abebe tofali moja kukamilisha ujenzi huo.
 
Humu ndani kuna watu wapo kwa ajili ya kudivert hoja sasa ukishajua huyo ni mmoja wao, hata akiku-quote unamshit! Au unautumia uhuru wako vema una update ignore list kwa kumuongeza, nalohili lahitaji wawekezaji au uhisani wa watu wa marekani! Mbona rahisi! Mjue wenzenu wanafurahi kuona mnavyohangaika kuumiza vichwa kuwajibu wakati wao hata hawajui wanaandika nini mradi wamebinya keyboard!
Chukua hatua hakuna aliyetumwa humu kila mtu kajituma ila tunatofautiana uwezo wa kufikiri, wengine uwezo wao wa kutumwa na wengine wa kutuma, wa kutumwa hata asipotumwa ni sawa kuwa katumwa tu unampotezea kwani hata umri na elimu yake hujui vinaweza vikawa vinamruhusu kufikiria anavyofikiri! Na ungejua hata usingethubutu kumjibu ila ungemcheka!
 
Jamani hizi nembo za bendera za vyama vya siasa zinatafuta nini humu. JF halina dini, chama wala kabila. Kila mtu akiamua kuweka nembo ya bendera ya chama chake itakuwa virugu tupu. Ni mawazo yangu tu.
Na wewe weka ya chama chako hakuna shida. Hapa tunaruhusiwa kuandika hata majina yetu halisi. Hatukatazwi.

Hii isikupe shida hii ndiyo avtar yangu
 
Ukweli ni kwamba:

1. Kweli makala ilitoka ... lakini kwenye toleo hilo hilo ilikuweko makala nyingine nzuri sana. Na jambo la msingi ni kuwa mhariri alitoa dokezo kwa nini ameitoa hii makala tunayoisoma hapa. Alisema ameitoa ili iende sambamba na makala niyingine ndefu iliyokuwa katikati ya gazeti hilo....bahati mbaya siipati kwnye mtandao..

2. Lakini makala yenyewe ni very positive .... ianyondeana na mtizamo halisi wa wahariri wa Rai Mwema.

3. Nilimuelwa kuwa kama angekataa kuitoa makala tunayosoma hapa alafu akaitoa ile nyingine.... angeonekana kuwa amekaa upande mmoja ...hivyo kwa kujiamini...azkazitoa zote.... LAZIMA KUZISOMA ZOTE PAMOJA ILI KUPATA MAANA KAMILI!!!!
 
Dr. Slaa wewe ni public figure hivi sasa na sidhani kama unatumia muda wako vyema kumjibu mtu anayesema 'umetumwa na kanisa kugombea urais' this is too low..Hivi ndivyo nionavyo.

Ungefanya la busara kuelezea mikakati yako na kuelezea kinagaubaga jinsi utavyoshape sera zako za kiuchumi ziadi. Haya mambo ya uswazi waachie akina Malaria Sugu.


malaria sugu yuko wapi?
 
Dr unaandika bila hata ya paragraph watu watashindwa kusoma.

Halafu "the onus of proove' ndiyo kitu gani mkuu? Kama Kiingereza mambo fulani tuandike Kiswahili tu tutaelewana, hii mikogo ya Kiingereza cha kuunga unga inakuaibisha tu.

Kiswahili cha first person na third person kinachanganywa humo humo wakati mtu (Dr.) anajiongelea mwenyewe !

Na inakuwaje CHADEMA mkawaachia CCM kuchukua majimbo 10 bila kupingwa, mengine wagombea hawarudishi fomu, mengine wanarudisha fomu lakini wagombea dhaifu kama kina Regia Mtema, hivi mkipeleka wabunge dhaifu kama hawa mnatuambia nini kuhusu uimara wa chama?

Zaidi ya hapo, je ukweli kwamba hamna wagombea madhubuti unachangia CHADEMA kuchukua mapandikizi ya watu walioshindwa kupata nafasi kugombea ubunge kwa tiketi za CCM ?

Regina mtema yuko makao makuu ya chadema. Bila kuzingatia ushawishi wake kisiasa wameona akagombee tu na matokeo yake kumbe ni mgombea dhaifu. Kufanya kazi kwake makao makuu ya chama ndio imekuwa kigezo cha kumpa kugombea. Wagombea kama hawa wakishindwa utakuta anatafutwa mchawi na mchawi huyo atakuwa CCM. kwa sasa CCM ina wabunge 21 waliopita bila kupingwa na madiwani 236 waliopita bila kupingwa. katika soka tunaita ushindi wa mapema ambapo mabeki wa timu pinzani hawakuweka ngome ya kutosha kuzuia kufungwa mapema mapema.
 
Mbona unaandika na kujijibu mwenyewe kama vile unapiga p... Acha kujidhalilisha, inaelekea usivyokuwa na akili kwa kuanzisha thread ambayo haina viwango, yaani umeonyesha chuki na kutumwa. Halafu mwanaume kutumwa bwana, yaani unakuwa ka nyoka, kutumwa, kama vile kukatuma katoto sigara dukani, lol aibu sana mtu mzima, eti antibayotiki, lol. Haya maneno hayana tofauti na Makamba hivi, manake ndio anaongea bila kufikiri

Hajatumwa anatoa mawazo na mtazamo wake katika hoja iliyo mbele yetu na hiyo ndio demokrasia yenyewe. Demokrasia ina pande mbili, utamu na uchungu. Ukitaka demokarsia hiyo iwe chungu kwa kikwete na tamu kwa Dk. Slaa ni bora ujiondoe mwenyewe kwenye jukwaa hili huru.....acha watu wakosoane kwa pande zote za utamu na uchungu kwa wagombea wote. Hii ndio gharama ya kushabikia kampeni za kihuni bila hoja za msingi.
 
Kiranga,
Wewe usijione kwamba haki ya mtu kueleza jambo kwa kiingereza ni YAKO WEWE BINAFSI(kIRANGA)!
Wewe ndiye namba 1 kwa kuandika andika vitu visivyoeleweka hapa jamvini kwa lugha hiyohiyo unayomlaumu nayo Dr Slaa...what a mess!:eyeroll2: .



Umembiwa kwamba mwandishi anatakiwa kufanya utafiti kidogo ili kuyajua hayo!..Hata wewe ukifanya utafiti kidogo tu utajua maana ya "the onus of proof"!...huh!

Kiranga hajagombea Urais hata akiandika kiingereza kibovu inakubarika kwa kiwango chake cha elimu lakini pia hana PHD kama Dk. Slaa. Tusilinganishe vitu visivyofanana wakati tunatafakari namna ya kupata Rais bora kwa nchi yetu.
 
1. Mostly naandika vitu vinavyoeleweka, kama huelewi niulize.

2. Hata ikitokea kwa nadra nimekosea, sijawahi kukosea kuandika "the onus of proove" instead of 'the onus of proof"

3. Hata ningekosea hivyo, sijaomba urais na standard ya kunibana mimi ni tofauti na standard ya kumbana Dr. Slaa

Dr. Slaa anataka kuwa colloquial sasa, na anatutia shaka kuhusu uwezo wake. Kiingereza hajui, kuandika kwa paragraph hajui, kutochanganya kiswahili na kiingereza hajui, kuwapa proofreaders wamsomee mambo hajui.

Anaweza kuwa rais akafanya vituko kama mambo yenyewe ndiyo haya.

Watanzania twafwa, Kikwete kilaza, Dr. Slaa mwenyewe watu wanaomtegemea awe kiongozi mbadala ndiye huyu au mtu tu kaja kuchukua hilo jina ?

kuna siku niliwaambia kwamba hapa JF kila mtu na fani yake kama ambavyo ACID anatamba hapa JF na fani ya sayansi hasa chemistry somo ambalo sikuwahi kufanya vizuri. Kiranga ni mtaala wa lugha kaona mapungufu ya kiingereza cha mgombea Urais wetu Dk Slaa kwa nini hatumpi fursa akatoa dukuduku lake. Fani zina wenyewe na ukizichezea wenye fani hizo hawawezi kukaa kimya. Ni bora tukubaliane tu kwamba Dk Slaa akaongeze uelewa katika somo la kiingereza kuliko kujidanganya kwamba mgombea huyo anajua kila kitu kwa ufasaha.
 
no group thinking and haitakaa itokee... fuatilia mada utaona where i stand, lakini lazima uambiwe ukweli, kuchamba kwingi kutoka na m@vi

excellence in vigezo vingi na si english au lugha, and that's where we differ

narudia tena... kuchamba kwingi kutoka na ------

That is you bro

Acidic

Kama umemuelewa kiranga anasema wembe ni ule ule kama unavyomvyoa kikwete hauna budi kumnyoa pia na Dk. Slaa. Angekuwa ni kikwete kaambiwa hajui kiingereza hakuna ambaye angejitokeza kumtetea na kama angejitokeza basi angeambiwa katumwa. Acheni group thinking kila mtu ajitegemee kwa hisia zake dhidi ya wagombea.

nisingependa kutaja watu kwa majina kwa vile hata kabla sijawataja na wao wanajijua. Ili ukubarike kwenye kundi la watu hawa hapa JF basi mkosoe sana kikwete huku ukimsifia mgombea yoyote wa upinzani na hasa Dk. Slaa. mtindo huu wa fikra mgando umejaa kuvunja kanuni za haki na uhuru wa binadamu kujieleza.
 
Back
Top Bottom