Naelewe hilo Mkuu....huyu wa kuja kaamua kuwatumia wasukuma kwa wingi wao kwa manufaa yake binafsi kisiasa na wengi wao wanajaa mkenge. Kwenye nchi yenye makabila zaidi ya 120 ni hatari kutukuza ukabila, hata kama mtu akiwa ndo mnufaika wa ukabila ni vema akaukataa ukabila kwani kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.
Kwanini kura yako iende kwa Halima na si kwa mwengine? Je sababu tu ni mgombea wa upinzani au ametekeleza ahadi zake alizowaahidi katika kipindi awamu yake iliyopita? au ni sababu ni sababu zipi zinazofanya umchague tena Halima?Halima Mimi siwezi kumlaumu maana serikali ndo inayokusanya Kodi(serikali kuu + Manispaa).Kwani watu wa kawe hatulipi Kodi ? Kama serikali haitaki kuleta maendelleo kawe ati kwa vile tumemchagua Mbunge wa upinzani,Basi hamna uhalali wa kukusanya Kodi huku kawe.KURA YANGU MI NAMPA DADA HALIMA.GWAJIMA AKACHUNGE KONDOO WA BWANA.
Paskali nisiwe mnafiki siwezi mchagua Gwajima kwakuwa alishasema anataka kuigeuza misikiti kuwa Sunday schools, nikiwa kama muislam nawaza huyu hakuwa na madaraka aliongea vile je nikimkabidhi madaraka itakuwaje? Mimi ni muislam na najivunia kuwa muislam
Mkuu Chakaza, hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Halima kupambana na serikali. Swali la uzi huu ni Halima ameifanyia nini Kawe kipindi chake cha miaka 10?.Kwa uwezo wa Halima kupambana na serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli, ninahakika atakuwa mbunge bora zaidi sio kwa Kawe tuu Bali Tanzania nzima katika serikali ya Tundu Lissu na Spika asiyetokana na CCM
Zungu ameifanyia Nini Ilala kwa Miaka 15 ?Mkuu Chakaza, hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Halima kupambana na serikali. Swali la uzi huu ni Halima ameifanyia nini Kawe kipindi chake cha miaka 10?.
Kwa vile pia ni ruksa mtu kuwa na dreams, na ndoto nyingine ni day dream za mchana kweupe, keep hopping for the best kuwa mtashinda, but get prepared for the worst ili usipate psychological depression.
P
Ambacho hakijafanya kazi ni dhana, ile ya maendeleo hayana, Yana chama.Ukweli upo wazi gwaji hana mpinzani , bi kidude hajafanya chochote cha maana jimboni kawe.
Paskali kuwa mkweli. Baada ya kupigwa chini na wajumbe na pia CC mlipewa maagizo kuwafagilia hao waliotoboa. Naona sasa upo kazini ila husemi ukweli. Kumbuka sijasema wewe ni muongo bali hujasema ukweli.Straight away, hii ni kampeni pia.
Ingawa umejaribu tu kuipamba kwa vijimaneno vya hapa na pale Kama kawaida ya wanasiasa mlivyo.
Ni kukosa mawazo sahihi kutazama Bunge lililoisha, lililomwita mleta mada ajieleze Kwa kuliita dhaifu, halafu kuamua linahitaji substitution atoke Mdee aingie Gwajima.Kwa uwezo wa Halima kupambana na serikali ya kibaguzi ya awamu ya tano chini ya Magufuli, ninahakika atakuwa mbunge bora zaidi sio kwa Kawe tuu Bali Tanzania nzima katika serikali ya Tundu Lissu na Spika asiyetokana na CCM