Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Siyo wote mkuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Naelewe hilo Mkuu....huyu wa kuja kaamua kuwatumia wasukuma kwa wingi wao kwa manufaa yake binafsi kisiasa na wengi wao wanajaa mkenge. Kwenye nchi yenye makabila zaidi ya 120 ni hatari kutukuza ukabila, hata kama mtu akiwa ndo mnufaika wa ukabila ni vema akaukataa ukabila kwani kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.
 
Wasukuma wa awamu hii ni wakabila mno, hata bandiko hili lina mrengo wa ukabila kwa mbaali. Hapo msukuma anapigiwa kampeni.
 
Wewe boya kweli. Yani unapiga kampeni huku ukijihami. Kama ulikuwa unauliza kuhusu Mdee, na lengo ni kuepuka ukada, usingemnadi Gwajima.

Mimi sina pande, hata wote wakose sijali. Ila tu , sipendi kugeuzwa boya. Acha unaa
 
Sijawahi vutiwa na siasa za CHADEMA ila kwa hili la Kawe Bora arudi Halima Gwaji boy ana zile siasa za kizamani Kama ule wimbo Ndio Mzee ya proffjize...Imagine eti anawadanganya wananchi atafanya exchange program ya wananchi na Marekani kha!
 
Ni bahati nzuri kuwa wanaccm wenzako walishakataa kukusikiliza kw a lolote lile. Gwajima hauziki kwa namna yoyote ile, karne hii mtu wa aina yake hawezi kujitokeza kuomba kura za kisiasa. Halima Mdee unamwelewa, na wewe mwenyewe utampigia kura
 
Halima Mimi siwezi kumlaumu maana serikali ndo inayokusanya Kodi(serikali kuu + Manispaa).Kwani watu wa kawe hatulipi Kodi ? Kama serikali haitaki kuleta maendelleo kawe ati kwa vile tumemchagua Mbunge wa upinzani,Basi hamna uhalali wa kukusanya Kodi huku kawe.KURA YANGU MI NAMPA DADA HALIMA.GWAJIMA AKACHUNGE KONDOO WA BWANA.
Kwanini kura yako iende kwa Halima na si kwa mwengine? Je sababu tu ni mgombea wa upinzani au ametekeleza ahadi zake alizowaahidi katika kipindi awamu yake iliyopita? au ni sababu ni sababu zipi zinazofanya umchague tena Halima?
 
Ni bora mara elfu moja jimbo liwe na Gwajima kama mbunge kuliko hiyo mama wa swaga za kitaa.

Miaka kumi imemtosha huyo mama, hana kipya zaidi ya kushinda kisutu akipambana kumaliza kesi zake.

Kawe ni jimbo lenye watu very influential hapa TZ hivyo sio haki kuongozwa na mbunge mwanaharakati.
 
Kwa uwezo wa Halima kupambana na serikali ya kibaguzi ya awamu ya tano chini ya Magufuli, ninahakika atakuwa mbunge bora zaidi sio kwa Kawe tuu Bali Tanzania nzima katika serikali ya Tundu Lissu na Spika asiyetokana na CCM
 
Paskali nisiwe mnafiki siwezi mchagua Gwajima kwakuwa alishasema anataka kuigeuza misikiti kuwa Sunday schools, nikiwa kama muislam nawaza huyu hakuwa na madaraka aliongea vile je nikimkabidhi madaraka itakuwaje? Mimi ni muislam na najivunia kuwa muislam

Na mimi n mkristo siwezi kubali waislam wanyanyapaliwe na watengwe hta ktk teuzi siwez mchagua gwajima na hta familia yngu tuliojindikisha n wanne hatuwezi pigia kura hyu mcheza porno, eti askofu mla kondoo
 
Kwa uwezo wa Halima kupambana na serikali ya awamu ya tano chini ya Magufuli, ninahakika atakuwa mbunge bora zaidi sio kwa Kawe tuu Bali Tanzania nzima katika serikali ya Tundu Lissu na Spika asiyetokana na CCM
Mkuu Chakaza, hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Halima kupambana na serikali. Swali la uzi huu ni Halima ameifanyia nini Kawe kipindi chake cha miaka 10?.

Kwa vile pia ni ruksa mtu kuwa na dreams, na ndoto nyingine ni day dream za mchana kweupe, keep hopping for the best kuwa mtashinda, but get prepared for the worst ili usipate psychological depression.
P
 
Mkuu Chakaza, hakuna ubishi kuhusu uwezo wa Halima kupambana na serikali. Swali la uzi huu ni Halima ameifanyia nini Kawe kipindi chake cha miaka 10?.

Kwa vile pia ni ruksa mtu kuwa na dreams, na ndoto nyingine ni day dream za mchana kweupe, keep hopping for the best kuwa mtashinda, but get prepared for the worst ili usipate psychological depression.
P
Zungu ameifanyia Nini Ilala kwa Miaka 15 ?

Mtulia ameifanyia Nini kinondoni baada miaka 4 ya kuwa CCM

Ritha mlaki alikuwa mbunge kawe kwa Miaka mingi aliifanyia Nini kawe?

Wewe ulikuwa JF kwa Miaka mingi umeifanyia Nini JF zaidi ya hizi post zako?
 
Siwezi kuchagua gwajima kwasababu anadanganya vijana wetu kuwa atawapeleka Birmingham kusoma na ataleta boti za kuvulia samaki. Isitoshe na anasahau kuwa hapo nyegezi mwanza kuna chuo cha uvuvi vijana wetu wanasoma hapo. Anadanganya kuwa ataleta tren pia amekuwa akitoa ahadi za uongo hiyo ni dalili ya wazi kuwa hafai kuwa kiongozi kwa njia yeyote ile. Akatimize kwanza ahadi alizozitoa kanisan kwake mbele ya madhabahu ya mungu.
 
Paschal kumbe na wewe umo? Mungu anakuona ndugu yangu, weka pembeni siasa chafu za gwajima.
 
wana Jf mmemnyoosha babu pasko mpaka presha imempanda,
mimi wala sina cha kuchangia zaidi ya kumwambia kuwa awe mbunifu, ajiajiri hata kilimo kinalipa, asisubiri huruma za waajiri wake ndo apate chakula cha kulea wajukuu.


hizi hoja dhaifu zinamvunjia heshima yake sana.
 
Paschal naomba nikuulize maswali haya yafuatayo.
1. Serikali ya Tanzania inaongozwa na chama gan?
2. Kazi ya serikali kwa wananchi wake ni ipi?
3. Kazi ya mbunge akiwa bungeni ni ipi?
4. Je unadhan mbunge anaweza kuleta maendeleo katika jimbo lake pasipo msaada kutoka kwa serikali inayoongoza?
5. Je mbunge mpinzan anawezo gan wa kuleta maendeleo katika jimbo lake kama hasikilizwi na hapati msaada kutoka serikali inayoongoza?
6. Tunaambiwa maendeleo hayana chama lakin dhahiri shahiri inaonekana maendeleo katika majimbo yanapelekwa kwa kuangalia umetoka chama gan, asilimia kubwa wanaopata ni kutoka chama tawala kwanini na wapinzani hawapati chochote?
7. Hata ukiangalia kwa ndani zaidi hata wabunge wa chama tawala hakuna maendeleo yeyote wanapeleka kwa wananchi kwa hiyo usishangae halima mdee kutopata maendeleo kwenye jimbo lake. Je unaweza kuniambia kwanini majimbo ya chama tawala nayo hayana maendeleo??
 
Straight away, hii ni kampeni pia.

Ingawa umejaribu tu kuipamba kwa vijimaneno vya hapa na pale Kama kawaida ya wanasiasa mlivyo.
Paskali kuwa mkweli. Baada ya kupigwa chini na wajumbe na pia CC mlipewa maagizo kuwafagilia hao waliotoboa. Naona sasa upo kazini ila husemi ukweli. Kumbuka sijasema wewe ni muongo bali hujasema ukweli.
 
Kwa uwezo wa Halima kupambana na serikali ya kibaguzi ya awamu ya tano chini ya Magufuli, ninahakika atakuwa mbunge bora zaidi sio kwa Kawe tuu Bali Tanzania nzima katika serikali ya Tundu Lissu na Spika asiyetokana na CCM
Ni kukosa mawazo sahihi kutazama Bunge lililoisha, lililomwita mleta mada ajieleze Kwa kuliita dhaifu, halafu kuamua linahitaji substitution atoke Mdee aingie Gwajima.
Ili akaongeze nini ambacho Bunge la Ndugai lilikosa?
 
Back
Top Bottom