Je hapa Nina mke kweli?atumia laki tatu ndani ya wiki3 akiwa ugenini katika harus

Je hapa Nina mke kweli?atumia laki tatu ndani ya wiki3 akiwa ugenini katika harus

Wiki 3 mkuu na watoto 2??? Huyo Ni wife material kabisa na kajua kujibana kweli kweli
In fact 350,000 ni hela ndogo tu,
Chukua 350,000/ gawanya Kwa 21 ni sawa na 16,600/- tu
 
Habar wanajamiiforum mke Yuko safar ,Yuko ugenini.. ktk harus yandugu zake ana wiki 3 Sasa,alikwenda na watoto 2,nje usafiri nilimpa laki350 kama akiba yamatumiz yake madogo madogo Cha ajabu, Sasa mtoto hata mtoto apate mafua anataka atumiwe Hela ya dawa tu ya 3000 nimebaki nashangaa,hapa nna mke kweli
Hahaha! Hapo umechemka brother!

Utafiti au kipimo cha money management kwa mke wako hauwezi kupima au kuhitimisha kupitia safari ya harusi au msiba.

Iko hivi, harusi na msiba zinakula sana pesa. Sasa hapo inategemea na mke wako huko harusini ana status gani! Kama ndiyo tajiri wa familia, kila shida lazima afikishiwe, na yeye ni ngumu kukataa kwa sababu mbalimbali ikiwemo kulinda status na tabia ya wanawake kupenda kwao! Asipotoa fedha atafedheheka ikiwa ndugu wanajua kabisa nyie mna pesa angalau!

Kama huwa hamuwasapiti huko kwa ndugu, sasa hapo ndiyo wamemnasa, hawamwachi lazima atoboke. Je, unahisi atavumilia kuambiwa maneno ya fedheha na ndugu zake akikataa kutoa pesa. Mfano, ndugu yake mwenyeji analialia anamwambia mkeo amuongezee pesa akakomboe nguo kwa fundi watakazovaa harusini unafikiri atakataa? ili anuniwe? Mwache mkeo amalize harusi kwa furaha!

Pima uwezo wa money management wa mke wako akiwa nyumbani na siyo kwenye matukio yanayohitaji pesa mfano harusi na msiba!
 
Picha yake tumuone.....
kabla ya picha tumwambie, mke kaenda kwao (kijjn i bet). sasa wa kjjn watajuaje kama katoka mjn kama asipochukua majukumu yote ya kwao,

350k kwa wiki 3 mwanaume mwenzetu anafungua uzi? umetudhalilisha sana wanaume wenzako mkuu,
 
Wiki tatu laki 3 ugenini let other thing zi remain constant awe anatumia 5000 per day

5000*30 days =150,000

At least angetumia hata ndani ya miezi miwili.

Ila kama anakula hotelini kwa wastani wa 10,000 per day angalau atumie ndani ya mwezi MZIMA na siku kadhaaa.

Naomba kuwasilishaaa.
Mkuu laki 3 ni hela ya kawaida sana kama kaenda nyumbani,huwezi kufika kwenu halafu uachie wazazi wako wakuhudumie!.Sasa hiyo hela tena uchanganye na hekaheka za harusi aisee, hapo una mke tena muongezee hata laki 2
 
nilimpa laki350 kama akiba yamatumiz yake madogo madogo Cha ajabu, Sasa mtoto hata mtoto apate mafua anataka atumiwe Hela ya dawa tu ya 3000 nimebaki nashangaa,hapa nna
Ni sawa tu, wewe umempa hela yake ya watoto hujampa kwa mujibu wa maelezo yako,
So mtumie tu
 
Uyo ni chaguo lakooo
Ni chaguo lakoooo *2

Ata kama anatingisa bhobhobhooo
Utadumu naeee *2

Sasa acha ujinga akirudi mfungulie biashara ili akipata dharura atumie ela yake, apo ndo ataona uchungu wa fwezaa.

Wanaume wengi mmewageuza wanawake omba omba ndo maana wanawanyoosha, mpe mtaji atafuteza kwake uone kama atazichezea kirais rais😀😀😀😀😀
 
Mkuu laki 3 ni hela ya kawaida sana kama kaenda nyumbani,huwezi kufika kwenu halafu uachie wazazi wako wakuhudumie!.Sasa hiyo hela tena uchanganye na hekaheka za harusi aisee, hapo una mke tena muongezee hata laki 2
Sawaaaa
 
Back
Top Bottom