Mkuu habari ya wewe. Sijajua sana uzoefu wako katika mambo ya siasa, ufuatiliaji wa habari na pia kudadavua mambo. Na pia hujaona risk ya anayoyasema mama. Tatizo kubwa lilopo ni elimu kwa mlipa kodi. Watu wakiona TRA wanaona jini limekuja kunyonya kitu ambacho si kweli. TRA inaongozwa kwa mujibu wa sheria na kila sheria wanayoitumia imepitishwa na Bunge. Tatizo ni utumizi wa sheria. Mpaka viwango vya kodi vipo katika sheria za kodi. Makampuni makubwa hayana shida sana maana yanaweka wataalamu wa kodi kusimamia shughuli zote za kodi na wanachangia 40% ya kodi. Hayati Maguuli alilisema hili sana. Tena alienda mbali kusema wananchi wapewe elimu ya Mlipa Kodi waelewe mambo. Aligundua tatizo lipo wapi. Ushahidi wa aliyoyasema kuhusu TRA huu hapa. Naona Samia karudia mle mle. Sema watanzania tumesahau kwa sababu anasema mtu mwingine.
Chonde Chonde, tusirudi nyuma kwenye ukusanyaji wa kodi. Kodi zilizo kwa mujibu wa sheria, la sivyo nchi itapoteza mapato na hatutafika hata alipotuachia Hayati.
Kwa asili watu hatutaki kulipa kodi. Ni nature ya Binadamu. Tuanzishe masomo ya kodi Kuanzia Shule ya Msingi hata yakigusa maeneo kadhaaa ya kodi ili watu waanze keulewa wajibu wao. Nchi Fulani ambayo nilishawahi ishi, watu wanaona ni aibu kuto kulipa kodi. Ni ukikwepa kodi, ni sawa na kuitwa Fisadi.
Niwaombe Watanzania, tuipende nchi yetu. Hatuna wa kutujengea nchi yetu, bali sis ndio tutaijenga nchi yetu pendwa Tanzania.
HOTUBA YA HAYATI KUHUSU KODI HII HAPA