Je, hii ni Mikataba ya Kimangungo katika jina la Uwekezaji?

Je, hii ni Mikataba ya Kimangungo katika jina la Uwekezaji?

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1. Waarabu wa familia ya kifalme Dubai, (DP WORLD) wamepewa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kwa mikataba ya kiduanzi unaotajwa miaka thelathini

2. Waarabu wa familia ya kifalme ya Dubai (Blue Carbon LLC) wamepewa kusimamia na kuhifadhi misitu ya Tanzania. Hii ni hekta milioni 8.1 (8% ya ardhi yote)

3. Watu wa Korea Kusini wamekabidhiwa kipande cha bahari ya Hindi na ardhi wachimbe madini nadra. Ajabu, hawa na mkopo wametoa na TUTALIPA na riba

4. Watu wa Australia (URANEX) wamepewa ardhi nzuri wachimbe madini nadra ya kimkakati na graphite Mkoa wa Lindi. Kampuni zao tatu zitauza madini nje

5. Watu wa Canada (BARRICK GOLD) wanaondoka na dhahabu. Hawajajenga hata smelters moja. Wanaacha mashimo na watu wetu kupigwa risasi

6. Waarabu wa familia ya kifalme Dubai (OBC) wao wameongezewa 1,500km² kutoka 4,000km² zilizokuwa kwa Maasai ambao wamebaki na 2,500km²

7. Watu wa Netherlands (SHELL) na Norway (EQUINOR) wamepewa kuchimba gesi asilia eneo la bahari kuu kusini mwa Tanzania, eneo la Likong’o Lindi

8. Waarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wamepewa kuendesha huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART), Dar es Salaam.

9. Watu wa France, Maurel & Prom Exploration Production (T) Ltd. (MPEP) wamenunua hisa kitalu cha uzalishaji wa gesi asilia cha Mnazi Bay, Mtwara.

10. Kandarasi ujenzi Bwawa la Nyerere (JNHPP) kapewa Egypt. Kandarasi ya ujenzi wa SGR kapewa China na Turkey. Waswahili mtapewa Kanda Bongoman.

NB; Umepewa nini wewe? Unaendelea kuwa admin wa kundi la WhatsApp, kuwatishia watu na ‘remove button’ wanaokosoa serikali? Shensisana. Zoea hiyo sauti

Martin Maranja Masese, MMM.
 
Kiumbe ambae hakuwahi kuota kuwa Rais wa nchi anapata madaraka kwa mtindo wa bahati nasibu, anaingia ikulu akiwa hajui moja wala mbili kuhusu uongozi, matokeo yake anatoa sehemu ya ardhi ya nchi aliyopewa kuiongoza kwa wageni huku yeye kwa ujinga wake akiamini bado ana mamlaka kamili ya kiuongozi.

Kiongozi anayefikiria kwenda kwenye show ya msanii ndio maana hata sishangai akituhumiwa kwa kashfa za kipuuzi, namuona kabisa ana tabia zote za kufanana na kashfa anazohusishwa nazo, hatuwezi kuwa na kiongozi wa hovyo namna hiyo halafu tubaki salama kama taifa, lazima tuumizwe tu.

Akili yake ya ajabu kwa sasa inafikiria tu wawekezaji huku akiwa amewasahau kabisa wazalendo wa nchi hii na vizazi vyao, ameingia upofu wa akili anaongoza kama vile yeye ndie atakuwa kiongozi wa mwisho kutawala hili taifa, kichwani hana kitu akiulizwa maswali ya msingi anajibu taarabu zile zilizomkuza kule alipozaliwa, tuna hasara sana kama taifa.

Mbaya zaidi ya yote ni pale anapotuonesha hayupo tayari kujifunza kutokana na makosa, alianza kukosea kwa DPW, kabla ya hapo akakosea Ngorongoro kwa wamasai, akaenda kukosea kwa KIA, na sasa anakosea kwa Wakorea.

Yote hayo anafanya kwasababu anajua mikataba ya hovyo wanayoingia kuitoa sadaka Tanganyika yetu wataifanya siri, kwake anaamini walinzi wake ni chawa wataokuja na maelezo marefu kutetea ujinga wake yasiyo na mantiki huku mwisho wakiweka namba zao za simu watupiwe chochote, wako kama mbwa wanaozunguka nje ya jumba la tajiri ndimi zao zikiwa nje kwa njaa, walaaniwe.
 
Wawekezaji wanasaidia tunapatapo ajira za udere. "kidding"
 
Naomba kujuzwa, hayo yote ni awamu hii isiyo na awamu?
 
Kiumbe ambae hakuwahi kuota kuwa Rais wa nchi anapata madaraka kwa mtindo wa bahati nasibu, anaingia ikulu akiwa hajui moja wala mbili kuhusu uongozi, matokeo yake anatoa sehemu ya ardhi ya nchi aliyopewa kuiongoza kwa wageni huku yeye kwa ujinga wake akiamini bado ana mamlaka kamili ya kiuongozi....
Usijali mkuu kuna siku hizo mali zote zitarudi kwa wananchi/ watz
 
Duh! Huyu muuzaji wa maliasili zetu ipo siku tutamfunga na kumchalaza fimbo mbele ya umma.haiwezekani auze za kwetu tu halafu za nyumbani kwao hauzi.
 
Usijali mkuu kuna siku hizo mali zote zitarudi kwa wananchi/ watz
Siku hizi kila nikilala nikiamka naskia katoa bandari, mara tena katoa misitu, katoa madini, katoa na bahari, hizi ni tabia za mwanamke asiyejitambua anayetuonesha kwa vitendo kabisa enzi za ujana wake alikuwa na tabia za aina gani.
 
Hili jambo limenikumbusha mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Mkataba huu ulisainiwa mwaka 2013 kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya China Merchants Holdings International.

Mkataba huo ulikosolewa sana kwa masharti yake yasiyofaa kwa Tanzania, ikiwemo kipindi kirefu cha mkataba (miaka 99) na kiwango cha chini cha kodi ambacho kampuni ya China ingelipa.

Huu pia naona una makando kando mengi sana. Mungu ilinde Tanzania
 
Ndiyo maana wanauana kwasababu ya vyeo wanajua madudu wanayofanya, ifike mahali chaguzi ziwaengue wanafamilia ili kuinusuru nchi
 
Wazee kwani ni nani anawashauri viongozi Wa Afrika.!?
Embu fikirieni Rais anapanda ndege na Cabinet yake... Naposema Cabinet simaanishi baraza la Mawaziri ..namaanisha wale anaohisi waende nae kula maisha.
Only...Only.. to put a signature in a paper..
KOREA!? WHAT DO THEY HAVE TO GIVE!? TO US.

Alafu unaweza fikiri tuko wenyewe..
Ruto nae Kaenda.

Is Black a CURSE...or Our Leaders ..!?
 
Ingekuwepo sheria ya kuwawajibisha viongozi kwa utendaji wao ingesaidia sana kuondokana na mambo kama haya.

Bado tuna safari ndefu sana kama taifa, kila kiongozi anakuja na kufanya atakachoamua kufanya, aharibu/asiharibu anajua fika muda wake ukiisha atajiondokea zake na hakuna kitu mtaeza mfanya.
 
Ingekuwepo sheria ya kuwawajibisha viongozi kwa utendaji wao ingekuwepo ingesaidia sana kuondokana na mambo kama haya.

Bado tuna safari ndefu sana kama taifa, kila kiongozi anakuja na kufanya atakachoamua kufanya, aharibu/asiharibu anajua fika muda wake ukiisha atajiondokea zake na hakuna kitu mtaeza mfanya.
Hatuwezi kuendelea na usng huu...
Haiwezekani.
 
Imagine Ruto...
Ambao tunaamini Wakenya wanajielewa anajustify uamuzi wake wa kijinga kabisa...

Hivi kama kweli kuna mbingu na roho hazifi.. mbona machifu wanalia sana huko waliko.

They fought battles against white's domination..
Saizi mijitu misomi na akili zao. Inapanda ndege kuwafuata.
 
Wazee kwani ni nani anawashauri viongozi Wa Afrika.!?
Embu fikirieni Rais anapanda ndege na Cabinet yake... Naposema Cabinet simaanishi baraza la Mawaziri ..namaanisha wale anaohisi waende nae kula maisha.
Only...Only.. to put a signature in a paper..
KOREA!? WHAT DO THEY HAVE TO GIVE!? TO US.

Alafu unaweza fikiri tuko wenyewe..
Ruto nae Kaenda.

Is Black a CURSE...or Our Leaders ..!?
Nasikiliza wasafi fm hapa namsikia msemaji wa serikali matinyi

Anatupanga mpaka AUTO yaan anaongea utazani anaongea na familia yake 😊

R.i.p John Pombe Joseph Magufuli
 
Back
Top Bottom