Je, hii ni nchi au familia?

CWR2016

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
2,773
Reaction score
6,349
Moja kwa moja kwenye mada,

Kwa jinsi mambo yanavyoenda, najiuliza kweli hii tuliyomo ni "level" ya nchi kweli?

Au ni familia ya mtu kaamua ajinywee pombe zake na kuamua chochote?

Hebu tazama mifano michache hapa chini:-

Hebu soma mtiririko hapo juu,
Je, sisi wananchi ni "majuha"?!
Au hii nchi ni kama familia ya mtu, anaamua tu kusema lolote hata kama sio kweli?!

Tuendelee hapa chini..


Hebu soma tena mtiririko hapo juu,
Huyu ni Naibu Waziri, hapo alichokuwa anazungumza kipo wapi, kilichoandikwa kinaonekana kabisa, kuanzia 'heading' ya mkataba, hadi Appendix 1, phase2.

Nauliza hawa watu, are they jokers?! Is this a country really or just someone's family?!

Sisi ni "majuha?"

Tuendelee hapa chini tena..



Hebu tafakari.
Hiki ni kituko, these people are not serious!
Na hizo negotiations za DP WORLD na wakenya zilipigwa chini mwaka 2022.

Hivi najiuliza kweli huko CCM Kuna mtu ako serious kabisa?

Haya tazama tena hapa chini, si wanasema sio mkataba ooh bado hatuna mkataba..



Haya soma hapo juu, hiyo ni taarifa ya kamati ya Bunge, wanatamka kabisa "kwa kuwa MKATABA...",
Pia huyu anayeitwa Hamza Johari, anasema tumeweka kipengele katka mkataba kwamba hakuna mfanyakazi wa bandari....

Hicho kipengele wamekiweka wapi? Ktk MKATABA upi!?

Hivi ni maigizo au mazingaombwe?!

Hii nchi in TISS, JWTZ, PCCB, MAHAKAMA, BUNGE, MAWAZIRI, WABUNGE, TLS, LHRC, n.k
Hao wote wameshindwa kumsaidia mh. Rais Samia.?

Yani tamaa za CCM za uchaguzi ujao na za 10% za rushwa ktk hili, linayumbisha nchi kiasi hiki?!

Wote tumekuwa Taifa la ovyo kiasi hiki?!

Hii ni nchi au familia, ni akili au matope?!
 

Attachments

  • F0S-9CpX0AA8ieA.jpeg
    216.5 KB · Views: 5
  • Screenshot_20230716-000531.jpg
    225.7 KB · Views: 5
  • Screenshot_20230714-165246.jpg
    151.8 KB · Views: 3
Eti baada ya utafiti wa kina wakaichagua DPW ile iliyofunguliwa kesi karibia nchi zote walizoenda kuwekeza!

Huo utafiti utakuwa ulifanywa na vipofu wa macho na akili.
Hakuna cha utafiti wala kutumia akili. Ni waongo watupu.

Walaghai na wauza nchi.

Tuna bahati mbaya tumepata viongozi hata aibu hawana.
 
Wazee wa bahasha njoeni hapa mtudadavulie kwa facts... Lord denning, Faizafoxy mfia dini, covax, GUSSIE choiceVariable HIMARS!! NB; Msijeleta ngonjera hapa kila kitu kiko open. Jibuni hizi hoja ili mnachokikitetea raia wawaelewe!!
 
Nimescroll tu
 
Jamii forums kuna vichwa kuliko vichwa water vilivyojazana kwenye Baraza la mawaziri and co. God bless CWR2016. Hawa watu wangekuwa na aibu wangejifungia kupata mbinu mpya. System nzima umeiaibisha. CCM mlishakosa aibu
Tuna aibu nchi hii, acha tu.

Wanetu na wajukuu na vizazi vijavyo vitashangaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…