Je, hii ni nchi au familia?

Lugha ya malikia imekupiga chenga.Mtafute mtu akutafsirie.
 
Wazee wa bahasha njoeni hapa mtudadavulie kwa facts... Lord denning, Faizafoxy mfia dini, covax, GUSSIE choiceVariable HIMARS!! NB; Msijeleta ngonjera hapa kila kitu kiko open. Jibuni hizi hoja ili mnachokikitetea raia wawaelewe!!
Lugha ya malikia ,mleta uzi,imempiga chenga
 
Jamii forums kuna vichwa kuliko vichwa water vilivyojazana kwenye Baraza la mawaziri and co. God bless CWR2016. Hawa watu wangekuwa na aibu wangejifungia kupata mbinu mpya. System nzima umeiaibisha. CCM mlishakosa aibu
Lugha ya malikia mleta uzi,imempiga chenga.
 
Ukishakuwa na Waswahili wa Pwani kama viongozi wa juu kabisa nchini wawe huru kufanya maamuzi mambo kamwe hayawezi kunyooka. Ndivyo walivyo hao!!
Tatizo lugha ya Malikia inawapiga chenga.Mleta uzi Engish ya sheria ,ni tofauti na ya broken English.Makubaliano(MoA) na Mkataba(contract) ni vitu viwili tofauti.
 
😀😀...hongera aisee,
yani umekusanya evidences zote.Umepita mule mule, washajichanganya hata hawajui wanaongea nini sasa kuanzia juu mpaka watendaji wote
 
[emoji3][emoji3]...hongera aisee,
yani umekusanya evidences zote.Umepita mule mule, washajichanganya hata hawajui wanaongea nini sasa kuanzia juu mpaka watendaji wote
Tatizo lugha ya malikia,inampiga chenga mleta uzi,na wengineo.
An MOU is Used when companies plan to
work together or partner on a project or similar venture.
A memorandum of understanding (MOU) is a formal agreement that OUTLINES(makubaliano) plans for a common(Ya Pamoja) line of action between TWO or MORE PARTIES.
MOA(Makubaliono) ni tofauti na CONTRACT(
!mkataba wa sheria) .
Contract :That is intended to be enforceable by LAW.
 
Umeieleza vizuri,
Ila moja ya hoja ya msingi katika hii mada hapo juu ni mkanganyiko uliopo katika kuleta ufafanuzi juu ya huo mkataka au makubaliano as you have termed it..
Don't you see something is wrong there?
 
Hii ya kusema kwamba walishindanisha makampuni 7 na DPW akapatikana ni kutaka kujitoa kwenye kashfa ya kuvunja sheria ya manunuzi ya umma, wakati inavyoonekana hii ngoma imetolewa kama sandakalawe kwa wajomba.....watu tuna akili zetu bhanaa.
 
CCM inanuka haitufai na chadema na demokrasia yao tukiipa nafasi watapitisha LGBT mchana kweupe... tunahitaji chama kipya kabisa cha vijana tukafanye mabadiliko tunayoyataka na wanayoyataka baba na mama zetu katika nchi hii bila uoga wowote
Nimekusoma vizuri sana na kukuelewa ulichoandika hapa.

Sina mawazo ya kupingana na chochote ulichoandika hapa, lakini naomba nawe unisome kwa uangalifu unielewe vyema.

Ni hivi mkuu 'Mtu Mweusi':

Kama unavyojionea wewe mwenyewe juu ya jambo hili wanalong'ang'ania CCM; swala la Bandari, waTanzania tutake au tusitake mradi huo, CCM imekwishaamua, kwa hiyo waTanzania hawana chochote cha kufanya juu ya hilo.
Lakini nikukumbushe, kama hukumbuki, CCM walishajiapiza kwamba "watatawala milele"; maana yake ni kwamba hawawezi kuachia madaraka kwa njia yoyote ile bila ya kuwaondoa kwa nguvu.

Kwa hiyo, CCM ipo, na itaendelea kuwepo waTanzania watake au wasitake; na wataendelea kufanya lolote watakalo wao bila kuhojiwa na yeyote.
Wakitaka huo ushoga unaokutisha sana wewe leo hii, hao jamaa utawakuta wakijitangaza hadi mlangoni kwako, na hutakuwa na lolote la kufanya.
Tafadhali, usidhani CCM haiwezi kuruhusu ushoga Tanzania, hawajapata ushawishi tu wa kuwafanya wafanye hivyo. Bila shaka unajua "ushawishi" ninaouzungumzia hapa.

Sasa geukia kwa hao CHADEMA.
Wewe umetaja hofu yao kuwa juu ya kuruhusu ushoga. Mimi pamoja na kuwa na hofu nao juu ya hilo, na wala halinipi shida kubwa sana kwao, ninazo sababu kubwa zaidi ya hiyo kuwatilia mashaka, kwa sababu sera wanazozisimamia sizielewi vizuri. Hawajawa bayana sana juu ya hilo.

Pamoja na hofu hizo juu ya CHADEMA kuwepo, sina hofu kubwa juu yao kwamba wakiingia madarakani watajitangazia uwepo wao hapo daima, waTanzania watake au wasitake. Maana yake ni kwamba, bado waTanzania watakuwa na uamzi wa kuwaondoa wakivuruga na kuwaweka wengine kutuongoza.

Sasa basi, kama baada ya kusoma yote haya yanayotofautisha vyama hivi viwili, na bado huelewi, itakuwa kwamba wewe husemi kweli juu ya sababu zako za kuwabakisha CCM madarakani. Wewe utakuwa ni CCM mwenyewe kindakindaki, ila hapa unazuga tu uonekane hupendezwi na yanayofanywa na chama chako.

Haya, kama huwataki CHADEMA, na wala huwataki CCM, mbona hujawataja ACT-Wazalendo, na vyama vingine vilivyopo Tanzania; lakini unasubiri chama kisichokuwepo?
 
Alionesha kivuli chake, umemuweka wazi.
 
Haya onesha, kwenye hicho kipengele, lugha niliyopotoka..
Dah!

Wakati mwingine inabidi kubaki mtu ukicheka tu, pamoja na unyeti wa swala linalojadiliwa hapa.

Kuna nyakati hushawishika niwaandike majina watu, kama huyo uliyemjibu hapo, ili niwe kila mara nikijikumbusha kutopoteza muda na wanayoandika humu kwa sababu hayana lengo lolote la kuchangia ili kuongeza uzito wa upande wanakosimamia wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…