Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Bila ya kupata hitilafu chuma ungeikuta babati hiyo, nazile cruiser zinapakia mizigo mpaka kwa mbele zinanyanyuka hivi hamuogopi
 
Nilikuwa naenda Arusha nimekata kilimanjaro express Enzi hizo zipo moto
Nmefika mapema kabisa nikapanda kwenye gari nikatulia gari ikaanza safari
Tunafika mbezi wanakagua ticket naambiwa nmekosea gari Ile niliyopanda inaenda Tunduma
Wakanishusha nirudi pale shekilango nikapande ya arusha ya saa kumi na mbili maana nilikuwa nmekata ya saa 11 alfajiri na ilishaondoka ilikuwa inapita njia ya bagamoyo.. nikachukua boda hadi shekilango tena
Ikabidi nipande ya saa 12 nilikuta nayo ndyo inatoka wakanipa siti
Tangu hapo nikajifunza kusoma namba ya gari kabla sijapanda.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
ndio uzuri wa kusafiri na kampuni yenye mabus mengi
 
Mbona kama chai mkuu🤣
Mkuu napata faida gani kuleta chai humu?.... Kama huamini basi ni wewe ila habari ndio hiyo, tena inaendana na mada hii.
 
Mkuu, Ubungo kuna mabasi yalikuwa yanaruhusiwa kuondoka saa 10:00 asubuhi? Nakumbuka mabasi yalianza safari saa 12:00 asubuhi.
Yeye kaandika saa 4:00 wewe unaandika saa 10:00 ?
 
Yeye kaandika saa 4:00 wewe unaandika saa 10:00 ?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] wewe kweli pacha wangu nilitaka kuandika sentensi hii kama ilivyo ila nikaona uzi tayari una komenti nyingi itakuwa tayari wameshamwambia wengi nikaona niache tu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] wewe kweli pacha wangu nilitaka kuandika sentensi hii kama ilivyo ila nikaona uzi tayari una komenti nyingi itakuwa tayari wameshamwambia wengi nikaona niache tu
Nimegundua mleta mada ali-edit, aliandika 10:00
 
Inaonesha wenye mabasi ni waswahili, mleta mada nae alifika dakika 15 mapema lakini basi lilishaondoka. Hawazingatii muda wanaondoka tu kwa mihemko.
 
Mkuu napata faida gani kuleta chai humu?.... Kama huamini basi ni wewe ila habari ndio hiyo, tena inaendana na mada hii.
HAkuna shida mkuu, ila nauli ya basi ilikua ngapi kipindi hiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…