Je, hili limekukuta kuachwa na bus kisha ukatumia bodaboda kulifukuza bus

Inaonesha wenye mabasi ni waswahili, mleta mada nae alifika dakika 15 mapema lakini basi lilishaondoka. Hawazingatii muda wanaondoka tu kwa mihemko.
maranyingi huwa hawazingatii ratiba huwa wanawahi au wanachekewa zaidi ukilinganisha na muda wa tiketi
 
Ndo ujanja huo??! Kudhulumu mwenzako unajisifia!!!!
Huoni kwamba Konda ndio alianza kudhulumu?

Walimwandikia muda wa kuondoka kwenye Tiketi, Abiria kafika stand dk kabla ya muda wa kuondoka lakini kakuta gari ishaondoka.

Hapo Abiria alikuwa na haki ya kurejeshewa nauli yake kwa kosa la gari kuondoka kabla ya muda waliomwambia
 
wazo lakununua tiketi mpya huwa halipo sababu unakua umevurugwa alfu wale maagent wanakushawishi uchukue bodaboda kwa kigezo cha bus halijafika mbali
Sababu wanajua ukishaondoka kufukuza Bus, wao washajivua moja kwa moja kwenye msala, inabaki juu yako.
 
Hao wasanii wanaondokaje kabla ya muda.

Wenzao Shabiby wakiona umechelewa wanakupigia simu.
 
Hao wasanii wanaondokaje kabla ya muda.

Wenzao Shabiby wakiona umechelewa wanakupigia simu.
Huu utaratibu nmewahi kuukuta gari za Tabora Dsm. Siku ya safari kutokana na dharura nkahairisha,nkaenda ofisini kwao nkabadilisha tiketi kusafiri siku inayofatia badala ya ile ya mwanzo.
Siku ya safari kwa tiketi ya mwanzo,kumi na mbili kasoro asubuhi nasikia simu inaita,kupokea jamaa ananiuliza ndugu uko wapi? Sisi tunakusubiri wewe hapa stand tuanze safari maana muda umekaribia,basi nkamjuza kuwa nilibadili tarehe ya safari na maongezi yetu yakaishia hapo.
Niliukubali sana ule utaratibu!
 
Kampuni ya bus gani hii?
 
Niliachwa na Super Feo Songea naelekea Dar. Dah usingizi huu. Niliamka hakuna kupiga mswaki, kunawa, shati kifua wazi yaani kama mwehu dah. Boda alimkimbia kama anapaa Mungu anatulinda aisee nashukuru Mizani haikuwa mbali hiyo ndiyo ilikuwa pona yangu, ila ndiyo siku pekee niliyoachwa na basic.
 
Mkifikia Walio achwa na Ndege Mnitag Nije nishushe Nondo.
 
Usingizi ni habari nyengine haukuweka alarm?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…