Je, huu ni ufuatiliaji wa uwajibikaji au udhalilishaji kwa bullying na intimidation?

Uwajibikaji Kwa Kosa gani?Kuna Wengine ni Wakuu wa Mikoa Wameshindwa Kutoa Vyeti ..Wamewajibishwa?
Kama Kuna Kosa awajibishwe kwa Namna inayofaa..Ni Mteule wake Huyo..anaweza kumuita Wakati Wowote ..
Wameshindwa kutoa vyeti wapi kwa nani na kwa sab gani?
 
Naomba kuuliza hivi katika mataifa ya watu walioendelea na kustaarabika, kiongozi unaweza kufanya maamuzi ya kuumiza hisia za wasaidizi wako hadharani na raia wakakushangilia?

Namba wenye majibu wanisaidie.

Hili swali la kichochezi...😵😵😵
 
Kujua idadi ya fedha iliyoletwa ofisini kwako sio kipaji cha kukariri ni umakini tu. Kumbuka aliyejibu swali lile lile kwa ufasaha ni diwani makini. Rais hawezi kuwachukia watendaji aliowateua mwenyewe.
 
Alichofanya Rais ni udhalilishaji he could've handled it way better ila pia huyu DED hakutimiza wajibu wake, haiwezekani Rais aje eneo lako la kazi ila usiwe na taarifa za miradi unayosimamia hata kwa kubeba notebook ili uweze kurejea.
 
The question is simple enough: hela za Road Fund ziko wapi?

Anajibu: Mimi ni mkubwa, nina Idara nyingi.

Rais kwani yeye hana idara nyingi? Nchi ilikuwa imeharibika, wacha ainyooshe kwanza. Wapinzani wanabariki uozo kupata sifa.
 
Wanabodi,
...
Is This Fair?, Huu Sio Udhalilishaji?.
This is not fair, hii sii haki, hii ni some sort of intimidation na udhalilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu. Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa.
....

Paskali
Paskali, kama ulivyoandika binadamu si mtimilifu, ni hivyo hivyo, Taasisi pia haiwezi kuwa timilifu kwa kuwa kanuni na taratibu za kuiendesha zimetungwa na binadamu ambaye si timilifu.

Paskali, kwamba B]Is This Fair?, Huu Sio Udhalilishaji?[/B], umeandika kwa hisia kali kwa kuwa unayedai kadhalilishwa ni mwanamke. Kwa msingi huo unajitabulisha kwamba una kasumba ya mfumo dume. Hakika wewe ndiye unamdhalilisha.

Kwamba Hizi intimidations niliwahi kuzizungumza hapa, ni mwendelezo wa kutetea waovu wasio na haya na hufanya hivyo kwa makusudi, panapokuwa na hombwe la uongozi (power vacuum). Kwa uhakika, majibu ya huyo Mkurugenzi (siyo kwa jinsi yake), ni ya udharilishaji wa kiongozi wa umma mbele ya public ya watu, nikirejea maneno yako.

Kajidharilisha mwenyewe, kama Mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi mkuu (accounting officer) wa bajeti (kupokea mapato na kuidhinisha malipo) na wakati ule ule kamdharilisha Rais, mamlaka ya uteuzi wake.

Moja ya misingi mikuu ya utawala bora ni kuchukua hatua papo kwa hapo. Na moja ya misingi ya ulezi bora wa mtoto ni kumpa adhabu wakati huo huo anapokosea.

UKIMCHEKEA NGEDERE UTAVUNA MABUA
 
Mtoa mada umeelezea kwa kina, our no 1 amekiuka kabisa protocol hapa huu ni udhalilishaji wa hali ya juu sio kazi ya Mkurugenzi kuwa na takwimu hizi na ninampongeza huyu mama pamoja na pressure from our no 1 alitulia na kujibu maswali kwa ukweli.

Hata yeye mh. Rais ana wasaidizi wengi tu ambao wanamsaidia katika uendeshaji wa nchi, hivi yeye tukimuuliza ni kiasi gani cha fedha idara ya TISS imepata kwa mwaka huu sidhani kama atakuwa na jibu la hilo swali papo kwa papo.

CCM itabaki ila viongozi wake watakuja na kupita na kuna maisha baada ya siasa, ni vema our no 1 akatambua hilo na sio kwake binafsi pia kwa generations zake.

Tanzania ni yetu wote, tofauti za kiitikadi zisitufanye tuwe maadui na kuwageuza watanzania wengine kama wakimbizi ndani ya mother land yao.

Yes we need rais anayewajibika but kisheria ,elewa huyu mama ana familia ,ana watoto je wameathirika kiasi gani na tukio lile la kuona mama yao anaadhiriwa hadharani? Na mbaya zaidi viongozi wote hawa ni yeye aliyewateua ,na hii inatoa picha kuwa our no 1 anapofanya uteuzi wake he don't apply his mind,i feel so sorry kwa huyu mama na familia yake hasa watoto wake(kama anao).
 
Kusoma A haina uhusiano na cheti.
Ndivyo tulivyojibiwa na Mh.Rais..Kama Cheti kingewekwa Hadharani kusingekua na Sintofahamu..

Ila Serikali ya Awamu ya 5 imejipambanua Sifa ya Kuwa Mkuu wa Mkoa siyo Elimu ya juu..Hata ukijua kusoma A unaweza kuwa Mkuu wa Mkoa..

chikundi Usipo kubaliana na Mh.Rais kuhusu hili utakua na Vyeti feki ..Maana Wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki hawampendi Rais.
 
Chukua Tano.

Swali tu: Je, Rais anashaurika????.

Yaliyotokea kama yangefanyika nyuma ya Pazia yasingekuwa na hadhira iliyojitokeza.

Yes! Kama mkurungezi kuna baadhi ya Takwimu ni lazima uzijue.Maana hesabu zote zinafika mezani kwako.
 
wote ccm watajuana wenyewe ukiona shetan anamla shetan mwenzie jua kiama kimekaribia
 
"Kitu chochote anachouliza raisi ni kikubwa kinatakiwa kuchukuliwa kwa uzito wa juu kabisa, maana yeye ndiyo mwenye maono ya juu kuliko yeyote nchini." Haya ni maneno ya kipuuzi kuliko yote niliyowahi kuyasoma katika mtandao huu tangu nijiunge.
Hivi mtu anapokuwa rais ghafla anakuwa na akili zenye maono kuliko wote nchini?!!! Hivi Magufuli yule mwenye kukurupuka katika maamuzi akiwa Waziri, na ambaye mara nyingi aliwaumiza watu na nchi kwa maamuzi hayo, leo anaweza kuwa ni malaika Gabrieli wa kuwa na maono kuliko Watanzania wote. Hebu tuacheni mzaha. Tumweleze tu ukweli Rais kuwa anawadhalilisha watendaji walio chini ya yake mbele ya umma kama alivyofanya Pascal. Tusimpambe kwa eti yeye ni 'superior', la!!! Kuna vikao vya ndani vya majumuisho ya ziara. Ni mahali pazuri pa kusahihishana ili utendaji uende sawia.
 
Mama hakujikanyaga hata kidogo..ila aliyepewa majibu ndio hakupenda.
 
Huyo DED aliwaza sahihi kama wewe,ndiyo yakampata yaliyo mpata jana.Tumeshajua zamani tuna utawala wa namna gani.chukulia houseboy/boy wako unamuuliza swali mbele za watu halafu anakujibu kunya

 
mfano mtu anakupa jukumu la uangalizi wa Banda lake la kuku halafu baada ya muda anakuja kukuuliza wamezaliana kuku wangapi unamjibu kuwa hufahamu idadi yake wakati hilo ndilo jukumu lako la msingi; unafikiri mwenye Banda atachukua hatua gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…