Je, huu ni wakati sahihi kwa kanisa Katoliki kubadilika na kuendana na kasi ya makanisa ya Kilokole?

Bila michango kanisa litaendaje sasa litalipaje umeme,maji,na bill zingine
 
Swali la kizushi hapa Tz kuna Kigogo inasemekana alikuwa hana dini lakini alipokufa alizikwa kwa heshima zote na padri ,what happened..?

"Kingunge ngombale mwiru"
 
Kanisa au dhehebu ni jumuiko la watu wanao ongozwa na imani moja, ndani kuna sheria na taratibu za kuwa unganisha. Usipo kubaliana nazo, wewe si mmoja wao.
 
uzi ulitakiwa uishie hapa.
 
Unajua wengi hapa mnamkosoa mtoa hoja kwa mihemko ama kwa kuwa ninyi nisehemu ya ..au BADO hamjamuelewa..mfano kule lutheran Kuna sadaka ya jengo..ipo miaka na miaka ..ikaja sadaka ya ujenzi..kabisa likajengwa ..hii sadaka ya jengo BADO ipo tu..unakaa unajiuliza hii ya Kazi Gani sasa..unajua ni kheri ikawa specified kwamba Kuna sadaka ya kutunisha mfuko wa kanisa..na watu wanaelewa hivyo..kuliko kuendelea kudanganya miaka chungu laki..kingine waumin mnachangishwa sijui kujenga shule..shule inajengwa..inakamilika..inaanza kufanya Kazi..BADO tena wanakuja kukusanya sadaka za kuendesha hio shule..unakaa unajiuliza Hawa walikuwa wanalengo Gani sasa..!?

Kanisa linamamiradi chungu kibao..lakni BADO wameendela kukamua mifuko ya waumini...kwa kigezo eti cha kumtolea mungu sadaka..ambazo ibada ikishaisha watu wachache wanajifungia chemba wanafanya wajuavyo...

Hoja ya mtoa mada iko clear..haya makkanisa mawili..katoliki na lutheran wameanzisha vijitabia ujinga ambavyo naona kabisa kabisa ipo siku watu haswa vijana wataacha kwenda kusali huko.na kuyapinguzia waumini..sheria za kutengana tengana kisa huna kadi ya kanisa..kisa sijui jumuia n.k.. sidhan Kama ni nzuri..

Na hizo jumuiya nazo ni uozo mtupu..na kuendekeza Umungu Mtu ..
 
Kweli mtupu huu
 
Uliona wapi mgonjwa anakunywa dawa za kienyeji na wakati huohuo anakunywa hizi dawa za kizungu. Aidha utulie kwenye dawa ya asili ama ya kizungu.

Umekosa Nini huku mpaka uende kule? Chagua moja ukishindwa wanakuchagulia.

Nyie ndio mnaenda tuition makanisa mengine....
 
Padre ana mshahara, bado michango ya kumwezesha inatakiwa. Jioni unamkuta bar anakunywa bia na totos pembeni. Ujinga, mchango kanisani sitowi.
 
Padre ana mshahara, bado michango ya kumwezesha inatakiwa. Jioni unamkuta bar anakunywa bia na totos pembeni. Ujinga, mchango kanisani sitowi.
Heheee..hao majamaa wanaonaga waumini kama makondoo flani hivi..na ndio ukweli waumini wengi ni makondoo wazee wa ndio mzee ukihoji unaonekana huna imani unataka kuvuruga amani kanisani..kumbe ni kujitambua..waumini wengi wa hizi imani hawajitambui.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Padre ana mshahara, bado michango ya kumwezesha inatakiwa. Jioni unamkuta bar anakunywa bia na totos pembeni. Ujinga, mchango kanisani sitowi.
Na wewe si ungekuwa padri! Kila mtu alipewa equal chance ya kuwa anavyotaka!
 
Issue ni wingi wa michango na matumizi yake. Kuna siku unaweza ombwa michango zaidi ya tano. Sadaka, shukrani, zaka, ujenzi, redio, miundombinu, sijui tunamuaga Nani, kumuwezesha kateksta.
Pili, Je michango inatumika sahihi. Hakuna kuhoji!
 
Issue ni wingi wa michango na matumizi yake. Kuna siku unaweza ombwa michango zaidi ya tano. Sadaka, shukrani, zaka, ujenzi, redio, miundombinu, sijui tunamuaga Nani, kumuwezesha kateksta.
Pili, Je michango inatumika sahihi. Hakuna kuhoji!
Ujalazimishwa kama hauna
 
Kanisa katoliki halihitaji kusifiwa au kumwogopa yoyote! kama unataka kutoka toka wala huna athari japo hata 0.000000000000000001%
Wewe nenda tu kajifie mbere kwa mbere
waliondoka akina martin luther na bado kanisa ni imara kuliko hata walipokuwepo ndio itakuwa wewe kinyamkera?
 
Kwa kuwa watoto wadogo hawana uelewa kamili; hubatizwa kwa imani ya wazazi na walezi wao. Kama wazazi na walezi wao hawaiishi vema imani Katoliki basi hakuna haja ya kuwabatiza.

Msingi wa Kanisa Katoliki upo katika familia na Jumuiya ndogondogo. Kama hauwezi kuwa na ushiriki hai katika hatua ya familia na Jumuiya ndogondogo basi hauwezi kuwa na uhai katika hatua ya Kigango au Parokia.

Kwa mujibu wa Sheria za Kanisa (Cannon Law); unaposhirikiana na mtu aliyejitenga na Kanisa Katoliki maana yake na wewe unajitenga na Mama Kanisa. Unakosa haki na favours zote unazopaswa kuzipata kama Mkatoliki.

Swali la kizushi hapa Tz kuna Kigogo inasemekana alikuwa hana dini lakini alipokufa alizikwa kwa heshima zote na padri ,what happened..?
Kwa kuwa umeshindwa kumtaja huyo kigogo, hizi zinabaki kuwa hearsay na majungu tu.

Hakuna imani ya kulazimishwa. Mungu ametuumba viumbe hai, hatulazimishi kumfuata. Sasa inawezekanaje Kanisa Katoliki likulazimishe? Haiwezekani.
 
Mchange kujenga hospitali ikikamilika gharama za matibabu ziko juu waumini hamuwezi kumudu na wala hamuwezi kutibiwa bure. Pamoja na kutoza gharama za matibabu za juu, ukarabati unarudi kwa waumini hata kama hawatibiwi hapo.
Hakuna shule binafsi zenye gharama nafuu kama Seminari na shule nyingine nyingi za Kanisa. I am speaking this from my own experience.

Kuna michango ya kijinga, waumini mumchangie padri awe na bima ya afya lakini waumini mkiugua mnaenda awaombee, wakati pado waumini mmechanga kujenga zahanati ama hospitali ambayo huyo padri anaweza kutibiwa bure.
Unapotosha.

Kanisa Katoliki linaamini kuwa sayansi ni matokeo ya uumbaji wa Mungu. Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa akili na utashi ili vimsaidie kufikia wokovu wake.

Wamisionari walipofika eneo fulani kueneza Injili walijenga vitu vitatu: Kanisa, Hospitali na shule. Kanisa linaamini katika sayansi. Hivyo kama una matatizo ya kiafya utapewa huduma za Kiroho (Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa) na utaambiwa uende Hospitali.

Mapdri pia hupewa huduma za kiroho (Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa) lakini pia hupaswa kupelekwa Hospitali. Hivyo wanapaswa kuwa na Bima.

Na kwa kuwa hawana ajira, hivyo ni jukumu la Kanisa Mahalia kumchangia na kuhakikisha anapata mahitaji yote ya kimwili ili aweze kutoa huduma za kiroho vizuri na kwa ufanisi.

I am glad kwamba jamii inaanza kustuka na huu utapeli wa makanisa na kuanza kuhoji uwepo wa Mungu. Miaka 50 ijayo dini itakua haina influence kubwa kwenye maisha tena.
Ilipaswa usikitike na unasikitisha katika hili.
 
Bahati mbaya Kanisa linafuata Theocracy (Uongozi wa Mungu) siyo Democracy (Uongozi wa raia). Haliangalii wangapi wanapenda nini ila linaangalia kipi ni sahihi mbele za Mungu.
 
Matendo yako ndiyo yana determine excommunication.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…