Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kanisa au dhehebu ni jumuiko la watu wanao ongozwa na imani moja, ndani kuna sheria na taratibu za kuwa unganisha. Usipo kubaliana nazo, wewe si mmoja wao.Habari wadau..!
Kabla sijaanza mada yangu ni declare interest kwamba mm ni moja ya watu waliozaliwa katika familia za kikatoliki na kubatizwa na kupata mafundisho yote huko.Lakini kwa sasa nimechagua njia yangu baada ya kupoteza imani ya kikatoliki.
Ndani ya kanisa wameanzisha utaratibu wa kuwatenga watu wale ambao hawashiriki katika jumuia hata kama unaenda kanisani na kutoa sadaka lakini kama haupo kwenye jumuia unatengwa hata ukifa hawakuziki.Je hii wamepata wapi ?na je huyo papa ndio ameamuru hii kitu au ni utashi wa waumini wenyewe.?
Watoto wa dogo wamekuwa wakikataa kuwa batiza sababu mama au baba hashiriki jumuia,je mtoto anarithi makosa au dhambi ya babaye au mamaye?Kabla ya hapo miaka ya nyuma watoto walikuwa wanabatizwa pasipo kuangalia ushiriki wa wazazi katika jumuia wala kuangalia kama mtoto ni wa nje a ndoa au la.
Pia kumeanza utaratibu wa kuwatenga wale wanaoenda kwenye maombezi ya uponyaji hata kama ni wana jumuia lakini ukigundulika una sali pia maeneo mengine kama mfano kama kwa Mwamposa n.k unatengwa.I'm speaking from the experience wapo jirani waliotengwa pia wapo ndugu waliokataa kuwazika kwa hasira akaitwa shekhe akamwekea ubani mkristo watu wakazika.
Je kanisa katoliki halioni kama linavyofanya sio sahihi kwa waumini wake ?
Swali la kizushi hapa Tz kuna Kigogo inasemekana alikuwa hana dini lakini alipokufa alizikwa kwa heshima zote na padri ,what happened..?
Kanisa katoliki lina maji ya baraka (maji ya upako),pia lina wale wana maombi .
Waumini wengi wa katoliki wamekuwa wakikimbia kanisa na kuamia makanisa mengine ya kilokole kufuata mafuta,maji na chumvi,je kanisa Katoliki linakwama wapi?Badala ya kuweka sheria ngumu kuwazuia kondoo wasitoroke zizini alioni kama kuna ulazima wa kubadilika ili kuendana na speed?
uzi ulitakiwa uishie hapa.Ndugu, kwa upendo kabisa, nakushauri utafute kumjua Mungu zaidi kuliko kuwa na karibu na kanisa huku ukiishi kwa hofu.
Ukimfahamu Mungu kwa undani hizo hofu za kutengwa na hujui atakaekuzika zitaondoka. Unachotakiwa kuhofia ni kuishi sawa sawa na mapenzi ya Mungu sababu yeye ndio anafahamu kuhusu kuishi kwako na baada ya kufa kwako.
Yesu alizikwa na Yusufu wa Arithmataya na hakukuwepo na Ibada ya maziko. Sasa wewe ni nani unayeogopa kutengwa??
Muamini Mungu tu kwa kila jambo, hata wasipokuzika, Manispaa watakuzika. Sidhani kama Mungu ataangalia umezikwa vipi ila atahukumu matendo yako. Mpendeze Mungu na hayo mengine muachie yeye atakufanyia njia kwani Mungu anaweza yote.
😂😂😂😂😂,nilidhani nimeona yote dunianijirani waliotengwa pia wapo ndugu waliokataa kuwazika kwa hasira akaitwa shekhe akamwekea ubani mkristo watu wakazika.
Kweli mtupu huuUnajua wengi hapa mnamkosoa mtoa hoja kwa mihemko ama kwa kuwa ninyi nisehemu ya ..au BADO hamjamuelewa..mfano kule lutheran Kuna sadaka ya jengo..ipo miaka na miaka ..ikaja sadaka ya ujenzi..kabisa likajengwa ..hii sadaka ya jengo BADO ipo tu..unakaa unajiuliza hii ya Kazi Gani sasa..unajua ni kheri ikawa specified kwamba Kuna sadaka ya kutunisha mfuko wa kanisa..na watu wanaelewa hivyo..kuliko kuendelea kudanganya miaka chungu laki..kingine waumin mnachangishwa sijui kujenga shule..shule inajengwa..inakamilika..inaanza kufanya Kazi..BADO tena wanakuja kukusanya sadaka za kuendesha hio shule..unakaa unajiuliza Hawa walikuwa wanalengo Gani sasa..!?
Kanisa linamamiradi chungu kibao..lakni BADO wameendela kukamua mifuko ya waumini...kwa kigezo eti cha kumtolea mungu sadaka..ambazo ibada ikishaisha watu wachache wanajifungia chemba wanafanya wajuavyo...
Hoja ya mtoa mada iko clear..haya makkanisa mawili..katoliki na lutheran wameanzisha vijitabia ujinga ambavyo naona kabisa kabisa ipo siku watu haswa vijana wataacha kwenda kusali huko.na kuyapinguzia waumini..sheria za kutengana tengana kisa huna kadi ya kanisa..kisa sijui jumuia n.k.. sidhan Kama ni nzuri..
Na hizo jumuiya nazo ni uozo mtupu..na kuendekeza Umungu Mtu ..
Uliona wapi mgonjwa anakunywa dawa za kienyeji na wakati huohuo anakunywa hizi dawa za kizungu. Aidha utulie kwenye dawa ya asili ama ya kizungu.Elewa kiswahili mtu hajajitenga anaenda kanisani kama kawaida na kutoa sadaka ila hayupo kwenye jumuia.Au anaenda kanisani kila jumapili na yupo kwenye jumuia ila akitoka kanisani anaenda kwenye uponyaji kwa Lusekelo au Mwamposa n.k .Mtu huyo anatengwa.
Kasome acha stori za vijiweni kila kitu kiko wazi.Dah kweli mnauwezo mdogo wa kupambanua mambo!
Heheee..hao majamaa wanaonaga waumini kama makondoo flani hivi..na ndio ukweli waumini wengi ni makondoo wazee wa ndio mzee ukihoji unaonekana huna imani unataka kuvuruga amani kanisani..kumbe ni kujitambua..waumini wengi wa hizi imani hawajitambui.Padre ana mshahara, bado michango ya kumwezesha inatakiwa. Jioni unamkuta bar anakunywa bia na totos pembeni. Ujinga, mchango kanisani sitowi.
Na wewe si ungekuwa padri! Kila mtu alipewa equal chance ya kuwa anavyotaka!Padre ana mshahara, bado michango ya kumwezesha inatakiwa. Jioni unamkuta bar anakunywa bia na totos pembeni. Ujinga, mchango kanisani sitowi.
Ujalazimishwa kama haunaIssue ni wingi wa michango na matumizi yake. Kuna siku unaweza ombwa michango zaidi ya tano. Sadaka, shukrani, zaka, ujenzi, redio, miundombinu, sijui tunamuaga Nani, kumuwezesha kateksta.
Pili, Je michango inatumika sahihi. Hakuna kuhoji!
Kwa kuwa watoto wadogo hawana uelewa kamili; hubatizwa kwa imani ya wazazi na walezi wao. Kama wazazi na walezi wao hawaiishi vema imani Katoliki basi hakuna haja ya kuwabatiza.Watoto wa dogo wamekuwa wakikataa kuwa batiza sababu mama au baba hashiriki jumuia,je mtoto anarithi makosa au dhambi ya babaye au mamaye?Kabla ya hapo miaka ya nyuma watoto walikuwa wanabatizwa pasipo kuangalia ushiriki wa wazazi katika jumuia wala kuangalia kama mtoto ni wa nje a ndoa au la.
Msingi wa Kanisa Katoliki upo katika familia na Jumuiya ndogondogo. Kama hauwezi kuwa na ushiriki hai katika hatua ya familia na Jumuiya ndogondogo basi hauwezi kuwa na uhai katika hatua ya Kigango au Parokia.Ndani ya kanisa wameanzisha utaratibu wa kuwatenga watu wale ambao hawashiriki katika jumuia hata kama unaenda kanisani na kutoa sadaka lakini kama haupo kwenye jumuia unatengwa hata ukifa hawakuziki.Je hii wamepata wapi ?na je huyo papa ndio ameamuru hii kitu au ni utashi wa waumini wenyewe.?
Kwa mujibu wa Sheria za Kanisa (Cannon Law); unaposhirikiana na mtu aliyejitenga na Kanisa Katoliki maana yake na wewe unajitenga na Mama Kanisa. Unakosa haki na favours zote unazopaswa kuzipata kama Mkatoliki.Pia kumeanza utaratibu wa kuwatenga wale wanaoenda kwenye maombezi ya uponyaji hata kama ni wana jumuia lakini ukigundulika una sali pia maeneo mengine kama mfano kama kwa Mwamposa n.k unatengwa.I'm speaking from the experience wapo jirani waliotengwa pia wapo ndugu waliokataa kuwazika kwa hasira akaitwa shekhe akamwekea ubani mkristo watu wakazika.
Kwa kuwa umeshindwa kumtaja huyo kigogo, hizi zinabaki kuwa hearsay na majungu tu.Swali la kizushi hapa Tz kuna Kigogo inasemekana alikuwa hana dini lakini alipokufa alizikwa kwa heshima zote na padri ,what happened..?
Hakuna imani ya kulazimishwa. Mungu ametuumba viumbe hai, hatulazimishi kumfuata. Sasa inawezekanaje Kanisa Katoliki likulazimishe? Haiwezekani.Kanisa katoliki lina maji ya baraka (maji ya upako),pia lina wale wana maombi .
Waumini wengi wa katoliki wamekuwa wakikimbia kanisa na kuamia makanisa mengine ya kilokole kufuata mafuta,maji na chumvi,je kanisa Katoliki linakwama wapi?Badala ya kuweka sheria ngumu kuwazuia kondoo wasitoroke zizini alioni kama kuna ulazima wa kubadilika ili kuendana na speed?
Hakuna shule binafsi zenye gharama nafuu kama Seminari na shule nyingine nyingi za Kanisa. I am speaking this from my own experience.Mchange kujenga hospitali ikikamilika gharama za matibabu ziko juu waumini hamuwezi kumudu na wala hamuwezi kutibiwa bure. Pamoja na kutoza gharama za matibabu za juu, ukarabati unarudi kwa waumini hata kama hawatibiwi hapo.
Unapotosha.Kuna michango ya kijinga, waumini mumchangie padri awe na bima ya afya lakini waumini mkiugua mnaenda awaombee, wakati pado waumini mmechanga kujenga zahanati ama hospitali ambayo huyo padri anaweza kutibiwa bure.
Ilipaswa usikitike na unasikitisha katika hili.I am glad kwamba jamii inaanza kustuka na huu utapeli wa makanisa na kuanza kuhoji uwepo wa Mungu. Miaka 50 ijayo dini itakua haina influence kubwa kwenye maisha tena.
Bahati mbaya Kanisa linafuata Theocracy (Uongozi wa Mungu) siyo Democracy (Uongozi wa raia). Haliangalii wangapi wanapenda nini ila linaangalia kipi ni sahihi mbele za Mungu.Kiukweli hili la kumtenga mtu kisa hashiriki jumuiya lina chukiza watu wengi ...na aliye wapa hii idea kawapoteza yaan wanahukumu wao wakati kazi ya kuhukumu ni Mungu....
Yesu alisema atakaye ni kana bac na yy atamkana mbele ya baba yake ....hakusema atamkana duniani....
Matendo yako ndiyo yana determine excommunication.Elewa kiswahili mtu hajajitenga anaenda kanisani kama kawaida na kutoa sadaka ila hayupo kwenye jumuia.Au anaenda kanisani kila jumapili na yupo kwenye jumuia ila akitoka kanisani anaenda kwenye uponyaji kwa Lusekelo au Mwamposa n.k .Mtu huyo anatengwa.