Je, ilikuwa ni kesi ya kisiasa kati ya CHADEMA dhidi ya Sabaya?

Je, ilikuwa ni kesi ya kisiasa kati ya CHADEMA dhidi ya Sabaya?

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,935
Je, ilikuwa ni kesi ya kisiasa kati ya chadema dhidi ya Sabaya?

Ilianzia jana huko Club House za Twitter ambapo kiongozi mwandamizi wa Chadema ndugu Godbless Lema alitoa povu la kutosha akiituhumu mahakama na mamlaka husika za Kitanzania kutotenda haki.

Pia wakili wa kujitegemea na kada mtiifu wa chadema, Fatuma Karume yeye alitoa povu lote kupitia DW-SWAHILI.

Ambapo alisema pamoja na ushindi huo, bado kuna nafasi ya kukata rufaa kwenye mahakama ya juu zaidi.

Baadae hali ikawa hivyohivyo kutoka kwa wafuasi mbalimbali wa chadema mpaka sasa.

Kuanzia Twitter,Facebook na hata humu Jamiiforums ni lawama kutoka kwa upande wa Chadema tu.

Tuhuma na kauli zinazoonekana kama vile kukatishwa tamaa kwa Chadema na wafuasi wao,kuhusiana na kushinda rufaa kwa Sabaya.

Je, kumbe ilikuwa ni kesi ya kisiasa kati ya Chadema dhidi ya Sabaya?

Ni kwa nini Chadema na waandamizi wake ndio wawe mbele zaidi kwenye malalamiko dhidi ya Sabaya?

Tuwekeni wazi kuhusiana na hili jambo.
View attachment 2216561
 
Wana haki ya kuumia maana vitendo vya ujambazi wa kutumia nguvu na uporaji nchini, huenda vikaongezeka badala ya kupungua.
Sio kuachiwa sabaya tu, chadema wanaumizwa hadi na wao kuendelea kuwa madarakani
 
Haikuwa uwazavyo. Chadema wanauwezo gani kushawishi mihimili ya serikali imtende mtu wao. Mwisho nikuulize ametimiz
 
Haikuwa uwazavyo.Chadema wanauwezo gani kushawishi mihimili ya serikali imtende mtu wao.Mwisho nikuulize ametimiz
Yule mwendesha mashtaka DPP Kweka.

Alituhumiwa awali kabisa kuwa na mahusiano ya kifamilia na Mbowe,lakini aliisimamia kesi mpaka hukumu ndio akaondoka kurudi Dodoma.

Kulikoni kwa hilo?
 
CCM wakitaka mtu ufungwe utafungwa tu, hakuna cha ushahidi Wala ubora wa mawakili,atatafutwa hakimu/jaji asiyejali kuharibu legacy yake provided amefanya watawala wanachotaka. Ni kupoteza muda kushangaa Sabaya ametokaje.
 
Ukiona hivyo ujue hiyo kesi umepigishwa kona kona nyingi mpaka kufikia jambazi kushinda rufaa. Jua tu CHADEMA ni watenda haki. Hapo wanawapigania wengi, hasa wananchi waliozurumiwa na huyo jambazi. Wanazurumiwa haki Yao pia. Hakuna mtetezi mwingine kwa wananchi wanyonge zaidi ya CHADEMA.
 
Ukiona hivyo ujue hiyo kesi umepigishwa kona kona nyingi mpaka kufikia jambazi kushinda rufaa. Jua tu CHADEMA ni watenda haki. Hapo wanawapigania wengi, hasa wananchi waliozurumiwa na huyo jambazi. Wanazurumiwa haki Yao pia. Hakuna mtetezi mwingine kwa wananchi wanyonge zaidi ya CHADEMA.
Wananchi walioporwa ardhi na Sabaya?

Wananchi waliochanganyiwa hela bandia na Sabaya?

Wananchi waliopandishiwa pato la halmashauri ya hai mpaka kuwa ya sita kitaifa?

Wananchi wa Hai waliobadilishiwa mbunge na Sabaya?

Au Wananchi wa kundi la Kweka waliopewa pesa kwenda kumzomea Sabaya mahakamani siku ya kwanza?
 
Back
Top Bottom