Je inachukua muda gani hadi account kua banned?

Sawa mkuu
Una uwezo wa kupokea kiwango chochote cha pesa hata billion ila inategemea na declaration yako uliyotoa wakati wa kufungua account kwamba una uwezo wa kuingiza kiasi gani kwa mwezi na kwa mwaka kama ni mfanyabiashara au kama ni mshahara ni kiasi gani. Kikizidi kiwango chako ulichojaza wakati wa kufungua akaunti lazima ilete hoja. Uliandika una uwezo wa kuingiza 10M kwa mwaka halafu wanakuta imeingia 100M kwa mkupuo lazima uhojiwe.
 
Wanakuchunguza vp mkuu sijaelewa hapo
Umepokea pesa kutoka AEY Inc.

Unasema AEY Inc hauifahamu.

Amount 100K dollars ni ngumu kuingia kwa mtu huku hamjuani.

So uchunguzi ni kuconfirm ikiwa hauifahamu AEY Inc.

Mfano unaifahamu na hata transaction unaijua.

Uchunguzi ni kuconfirm hiyo transaction siyo kwaajili ya kufund uhalifu au shughuli zingine za kinyume na sheria.
 
Nitawajib siifaham mwenyew nimeshangaa kuingiziwa pesa kama hizi😁
 
Ni kweli na hasa kama sins maelezo ya wapi ilikotokans kwa madhumuni gani. Hii inaitwa kutakatisha fedha, kosa ambalo halina dhamana. Utaswekwa lupango hadi hapo uchunguzi utakaponesha vinginevyo.
Nasweka vp na nimeenda kureport mwenyew kua nimeingiziwa pesa kimakosa??
 
Pesa ya kutoka nje haiingiii kimakosa kama vile umetumia mpesa.

Kule pesa inapotoka kuna fomu inajazwa ikieleza hiyo pesa inaenda kufanya nini? Au lengo la kuituma pesa nini?

Pili. Pesa itaingia kwenye acc yako lakini accnt yako inauwezo wa kupokea kiasi hicho? Kama sio maana yake pesa utaina ila hutoweza kuitoa.

Hapo ndipo itabidi uwaone wahusika uwapatie maelezo pesa imetoka wapi na inakuja kufanya nini?

Usije kuwa unafadhili vikundi vya kigaidi.

NB. 100m ni pesa ndogo sana hata mkulima anaweza kuipata kwa msimu 1.


Nimetoka zangu kupokea dolla 500.
 
Kwahiyo milion 100 acc haiwifungi?
 
Kwahiyo milion 100 acc haiwifungi?
Ni pesa ndogo ila itategemea imeingia acc ya nani.

Mf. Acc yako hsijawahi kupokea hata zaidi ya 5M. Unategemea nini? Hapo lazima waipaune acc yako iweze kupokea kiasi hicho cha pesa.

Katika kuipanua hapo ndipo itabidi uitolee maelezo.
Tofauti na hivyo pesa itaingia ila hutoi ng'ooo
 
Utatakiwa uwaambie huifahau au wairudish ilikotoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…