Update ya Utumbuaji
Hata Utumbuaji wa Wazuri wa mambo ya ndani, Mhe. Kangi Lugora, umefanywa kistaarabu.
Rais Magufuli aliishapokea taarifa ya madudu yao kitambo kupitia njia za kiserikali, waziri, katibu Mkuu na kamishna wa jeshi la zimamoto na uokoaji wote walijua kuwa hili rais ameisha lipata, Katibu Katibu Mkuu is the only one who did the right thing kwa kuandika barua ya kujiuzulu. Waziri na Kamisha waling'ang'ana kwenye nafasi zao.
Mpaka jana asubuhi rais Magufuli alipoyasena madudu yao, na kuwashangaa bado wapo, walikuwa bado hawajatumbuliwa, ni madudu yao tuu yamewekwa hadharani lakini wao hawakutumbuliwa. Enzi za tumbua za mwanzo, ilikuwa Lugora na kamisha watumbuliwe siku ile ile rais amepokea ripoti ya madudu yao,
Kwa vile kwa sisi huku nje ya serikali, no one knows rais Magufuli alipokea lini ripoti ya madudu hayo, ila ile asubuhi anazindua zile nyumba ndipo akautangazia umma madudu yale huku Waziri bado ni Waziri na hajatumbuliwa.
Halafu rais Magufuli akalalamikia madudu hayo publically huku Waziri bado ni Waziri, na baadae jioni ndipo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Kijazi akatoa taarifa ya uteuzi na kutumbuliwa kwa Waziri Kangi Lugora, haya ni mabadiliko chanya. Utumbuaji huu sio wa papara, na haukutangazwa kwa hamasa kwenye ile live!.
Tukisema this man is changing for the better, we are very right and truthful this man is changing for better. Siku hizi hakuna tena Utumbuaji wa papara
P