Je, inawezekana Jakaya Kikwete ndiye Nyerere wa leo?

Asante kwa ufafanuzi mzuri,lakini nikwambie Waarabu walipendelea sehemu ambazo walikuwa wanachuma kitu fulani na ndiyo maana ukataja hizo sehemu zilizokuwa na vitu.Nakuuliza je,Musoma,Mwanza,Sumbawanga,Songea,Arusha,Iringa,Bukoba,Kigoma,Songea,Njombe,Tunduru na sehemu nyingine nilizozisahau Waarabu walijenga shule ngapi?
 
Kasome reference nilizikwambia majibu ya swali lako yamo. Hakuna mkoa ambao EAST AFRICA MUSLIM WELFARE SOCIETY Haikujenga shule . Kwa mfano Shule ya msingi KIGOMA pale mjini KIGOMA karibu na stesheni ilitaifishwa lkn ilikuwa shule iliyojengwa na waislamu kabla ya uhuru. Soma please kisha urudi hapa. Nyerere mwaka 1968 aliifuta hii taasisi ya waislamu na habari ikaisha na shule zake zikachukuluwa na serikali.
 
Mkapa alifanya nini wewe zaidi ya kuuza mashirika ya umma na kuuza migodi kwa Bei za kutupa akipata 10% zake!?..najua utasema alianzisha tra,tra ilianzishwa na mzee mwinyi,unadhani mkapa angekuta nchi aliyorithi mwinyi angefanya lolote la maana na sera zake za kulipa madeni!?
 
Mkapa ndiye Gwiji wa uchumi wa kisasa tulionao. Ila huwezi kuelewa kwa vile una akili za mipasho tu
 
Leo hii Wakenya ni maandamano kila kukicha, mishahara wanahangaika kulipa kwa miezi karibu sita sasa.

Tanzania inabadilika kiuchumi wakati majirani zetu wanaishi na hadithi nzuri za miaka iliyopita. Sawa sawa na zile story za wazee, zamani nilikuwa navaa sana, zamani nilikuwa napendwa sana na warembo zamani nyiiiingi na hazina msaada wowote kwa sasa.
 
Yaani watu ninyi wajinga sana Mkapa alifuta kodi ya kichwa na nchi ikasonga kuliko awamu zote.
 
Yaani watu ninyi wajinga sana Mkapa alifuta kodi ya kichwa na nchi ikasonga kuliko awamu zote.
Nchi ilisonga wapi babu!?..mkapa anaingia madarakani mpaka anatoka Nina akili zangu timamu,natoka dar-mwanza siku tatu,wenye hela wanapitia Kenya na Uganda kufika bukoba
 
Nchi ilisonga wapi babu!?..mkapa anaingia madarakani mpaka anatoka Nina akili zangu timamu,natoka dar-mwanza siku tatu,wenye hela wanapitia Kenya na Uganda kufika bukoba
Wewe uliyekuwa Dar es Salaam nchi haikusonga,lakini sisi wa Mikoani tuliiona kazi yake kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano.
 
Wewe uliyekuwa Dar es Salaam nchi haikusonga,lakini sisi wa Mikoani tuliiona kazi yake kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano.
Mimi kipindi Cha mkapa nikiisho dar na mikoani,sekta gani ilipiga hatua kipindi Cha mkapa!?..si kilimo si biashara,tukiita awamu ya ukapa sababu hapakua na hela,maafisa wa serikali mshahara elfu 60,mpaka anaondoka 2005 mshara hauzidu laki tatu kwa maafisa wa serikali
 
Pesa ilikuwa na thamani,kama ni sekta ni nyingi tu mfano.Kilimo,Elimu,Afya,Demokrasia,Siasa Safi,Utawala Bora,Miundo mbinu,Ajira,Ulinzi na Usalama pamoja na Diplomasia.
 
Pesa ilikuwa na thamani,kama ni sekta ni nyingi tu mfano.Kilimo,Elimu,Afya,Demokrasia,Siasa Safi,Utawala Bora,Miundo mbinu,Ajira,Ulinzi na Usalama pamoja na Diplomasia.
Hizo sekta zote zilikuwepo,ipi ilipiga hatua kipindi Cha mkapa!?..watu wa kilimo hulilia walau kitengewe bajeti 7%,mkapa aliweka ngapi?..maana huko nyuma ikiwekwa chini ya 3,%,jakaya nadhani aliweka juu kidogo,Kisha Samia ndiyo kavunja rekodi...sekta ipi mkapa aliinyanyua,mwinyi kaondoka kaacha Dola 1 ni 579,mkapa aliacha 1200,hayo Madai ya pesa kuwa na thamani yanatokea wapi!?
 
Acha dharau unawezaje kumfananisha Nyerere na kikwete

Nyerere alikuwa mbali Sana kuliko akina kikwete ,na maraisi wengine kiufupi sioni wa kufananisha na Nyerere
Ilikuaje akataka kupinduliwa mara tatu ?
 
Pesa ilikuwa na thamani,kama ni sekta ni nyingi tu mfano.Kilimo,Elimu,Afya,Demokrasia,Siasa Safi,Utawala Bora,Miundo mbinu,Ajira,Ulinzi na Usalama pamoja na Diplomasia.
Rekodi na maisha ya watu ni vitu viwili tofauti.Rejea utawala wa Awamu ya Tano tulitangaziwa kuwa Tanzania imekua kiuchumi na imefikia Uchumi wa Kati je hali ya maisha na huo uchumi wa kati viliendana?Rekodi za kwenye makaratasi sisi hatuzitaki hata sasa hivi utaambiwa umeme upo nchi nzima huku umeme ukikatika mara kwa mara bila aibu.
 
Tumia vizuri kichwa chako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…