Je, inawezekana Jakaya Kikwete ndiye Nyerere wa leo?

Je, inawezekana Jakaya Kikwete ndiye Nyerere wa leo?

Meli ya serikali iliyouzwa kipindi chake siyo ufisadi?.
Halafu kumpa sifa mtu aliyeshindwa kukuza uchumi wa watu kati ya milioni 9 na 15,ni upuuzi ukimlinganisha na aliyekuza uchumi wa watu kati ya milioni 40 na 50.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Babu yako kipindi nyerere anapigania nchi alikuwa wapi wewe zwazwa
 
Kwenda kinyume ni presha za wahisani zinazokuwa ni sababu tusizozifahamu za nyuma ya pazia.

Kwenda kinyume pengine ni ile roho ya wasaidizi wa marais wanaotaka kutajirika wakijua kuwa kipindi cha kupata neema ni ile miaka kumi ya kuwa pamoja na rais.

Kuongoza nchi sio kazi ya rais peke yake, anakuwa na timu nzima ya wasaidizi nyuma yake.
Hakuna kitu kama hicho
 
Wakuu kwanza nianze kwa kujihami mimi ni layman kwenye upande wa political science! Pia si mkereketwa kbs wa siasa lakini kwa kuwa maisha ya binadamu wa leo ni ngumu sana kuyatenga na politics by default najikuta tu niko uwanjani.

Nimejaribu kufuatilia safari ya maisha ya JK ya kisiasa influence yake ndani na nje ya nchi, namna viongozi wanavyokimbilia kwake kuomba ushauri, inanipa nafasi ya kufikiri kwa uchache wake.

Je, inawezekana yeye ndo Nyerere wa Tanzania ya leo?! (Remote from Msoga).
Acha kumlinganisha Nyerere na vitu vya kipuuzi
 
Hata huo muda wa kuandika kejeli zako ukiwa huru na amani tele chumbani kwako ni matunda ya Julius. Aliiunganisha nchi na kujenge msingi tunaouishi hata sasa.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Watanganyika walikua wamoja tangu kabla ya Nyerere kufundisha pugu,ndiyo maana alipoingia siasa, waswahili wa dar walimpa nyumba magomeni Aishi Bure huku wakiilea familia yake,Kama unazungumzia muungano basi zbar na Tanganyika walikua wamoja, ndiyo maana mzee mwinyi alihamia zbar akiwa na wazazi akiwa na umri wa miaka mitano,uhuru ni kazi ya waswahili wa pwani
 
Jk ana kipi cha maana zaidi ya kusifiwa na nyinyi wavaa makobadhi?
Alijenga barabara za lami 6000km wakati awamu tatu za mwanzo hazikujenga zaidi ya 4000km,alijenga shule za kata ili watu wasome wakati awamu zilizopita zilirithi shule za mkoloni na hazikujenga sekondari hata moja,alifungua fursa za elimu ya juu nchi ikawa inatoa wahitimu mpaka 50k wakati kabla ilikua 10k,aliongea zaidi ya $30d kwenye GDP ya nchi,aliajiri,Jenga hospitali kubwa na kuboresha,aliinua kilimo nk
 
Alijenga barabara za lami 6000km wakati awamu tatu za mwanzo hazikujenga zaidi ya 4000km,alijenga shule za kata ili watu wasome wakati awamu zilizopita zilirithi shule za mkoloni na hazikujenga sekondari hata moja,alifungua fursa za elimu ya juu nchi ikawa inatoa wahitimu mpaka 50k wakati kabla ilikua 10k,aliongea zaidi ya $30d kwenye GDP ya nchi,aliajiri,Jenga hospitali kubwa na kuboresha,aliinua kilimo nk
Hata mimi nakubali kuwa JK alifanya makubwa mengi wakati wake. Lakini naomba usi discount yaliyofanywa na watangulizi wake ukadhani ni madogo.

Kazi ya BW Mkapa peke yake ni kubwa pengine kuliko marais wote waliomfuata yaani JK, JPM na Samia. Ila inabidi uwe mbobezi kwenye uchumi na analysis katika issues.

Misingi yote ya uchumi tulionao leo iliwekwa na BWM, hawa wengine wanapita tu kusafiria nyota yake
 
Unalinganisha Nyerere na JK wewe kweli barvicha

USSR
Nyerere huyu aliekuwa anaambiwa na Kenyatta anaongoza Maiti??? Walikuwa na kipindi Kenya kama kile cha klab la leo walikuwa wakiuliza masuali ni nchi gani wanavaa mipira ya gari kama viatu??? Jibu Tanzaniaaaa Heeeee wanashangilia walitudharau sana wakenya kipindi cha babayenu wa Taifa.
 
Soma reference zenye akili kisha ndo uje kuandika. Wajerumani walipofika tanganyika walikuta wasomi wakiwa waislamu ambao waliandika kila kitu kwa hati ya kiarabu.
Taasisi ya EAST AFRICA MUSLIM WELFARE SOCIETY iliyojenga mashule kibao Tanganyika kwa ajili ya waislamu Nyerere aliipiga ban mwaka 1968.
Kama ni mtu wa usawa kwa nini hakupiga marufuku mashirika ya kikristo yaliyomiliki shule mbalimbali ili kufanya usawa?
Sasa nakusaidia. Kasome Kitabu cha Padre Dr John Sivalon na Kitabu cha Mohamed Said humo utapata kumjua Nyerere ni nani hasa na utaacha porojo zako ulizodesa kutoka magazeti ya uhuru na mzalendo. Utaelewa kwa nini wakati wa kuandika historia ya Tanganyika na uhuru wake walipewa hiyo kazi watu 2 :
1. Dr Wilbert Kleruu
2. Abdulwaheed Sykes
Baadaye Abdulwaheed akaondolewa na akaandika Dr Kleruu peke yake.
SOMA KIJANA ACHA POVU.
Yaani wewe unafikiri tuko zama za giza unamdanganya nani ni shule zipi Tanzania ambazo Waislam walijenga kabla ya uhuru?
 
Yaani wewe unafikiri tuko zama za giza unamdanganya nani ni shule zipi Tanzania ambazo Waislam walijenga kabla ya uhuru?
Shule ya msingi lumumba pale karibu na magazeti ya ccm, Kinondoni muslim, kibohehe sec kule moshi.
Yaani kwa ufupi ni nyingi sana.
Wewe soma kitabu cha UNTOLD STORY OF MUSLIM STRUGGLE AGAINST BRITISH COLONIALISM IN TANGANYIKA by MOHAMED SAID kisha ukimaliza urudi hapa kutema pivu lako tuone.
Ukiongeza na kusoma kitabu cha mkatoliki Dr John Sivalon aliykuwa padre utambua kuwa waislamu waliminywa tena maksudi.
 
Back
Top Bottom