Alijenga kanisa la parokia ipi?, Au alimsomesha padre yupi?, Au alijenga seminari gani?
Tatizo la kutumia maneno ya vijiwe bila kuwa na fikra tunduizi( critical thinking) ndio haya.
Nyerere katika maisha yake ya siasa na elimu alisaidiwa na kanisa ndio sababu ya ukaribu na hao jamaa.
Issue ya wakristo wengi kuwa viongozi ilitengenezwa na suala la elimu. Waislamu wengi hawakusoma elimu ya kikoloni ambayo ilikuwa ndilo hitaji la uongozi.
SASA utampaje mtu uongozi wa Katibu mkuu wa wizara au mkurugenzi wa idara fulani na wakati ameishia darasa la nne na hajui chochote kuhusiana na hiyo wizara au idara?
KIFUPI: Hakukuwepo upendeleo ila upande wa pili walikuwa hawana elimu iliyohitajika.
Waislamu walikuwa wana elimu ya dini ambayo inasisitiza uongozi apewe muislamu mwenzao na siyo vinginevyo ( Nyerere alifanya kazi ya kuondoa mawazo ya aina hii, Ndio maana anachukiwa na upande huo).
Angekuwa mdini uongozi wa URAISI angemkabidhi MKRISTO mwenzake lakini hakufanya hivyo. Kwahiyo, Nyerere analaumiwa kwa kutengeneza jamii yenye usawa ( Kwasababu, wale waliotarajia kupendelewa, hawakupendelewa).