Nadhani hujaelewa hoja ya mhusika.
Hoja ya mchangiaji ipo katika kufananisha, " Alichokuwa anafanya Nyerere kwa RAIS aliyekuwepo madarakani kipindi yupo hai" ni sawa na anachofanya Kikwete kwa RAIS ambaye yupo madarakani kipindi hiki.( Hoja ya ulinganisho ndio ilikuwa hapo).
NB
URAISI ni kazi ngumu sana, katika uongozi huwezi kuwa unakubali kila kitu, ukifanya hivyo ukakaruhusu mambo ya ajabu sana kwa kigezo cha demokrasia( Hivyo, Udikteta katika baadhi ya mambo ni MUHIMU. Hasa yale yanayolinda maslahi ya nchi).
Kashfa za rushwa, wizi, matumizi mabaya ya madaraka, uuzaji wa rasilimali za nchi, nk. Nyerere hakuwa nazo, Hivyo aliondoka na mikono safi( Hii inaonesha kuwa alikuwa ana nia njema).
Hao waliokuwa wanamshauri walikuwa wana mtazamo wa chini na walikuwa wanatumika na maadui wa nchi. Ndio maana Nyerere alikataa ushauri wao.