Unadhani Watanzania ni wajinga kumwita baba haambiliki?
Aliharibu uchumi wa wananchi kwa kuwahamishia kwenye vijiji ya ujamaa vya mfano.
Watanzania wenye asili ya Tz hawakuruhusiwa kufanya biashara binafsi kila kitu duka la ushirika ila watu kutoka Asia waliachiwa matokeo yake Sasa wamekamata njia kuu zote za kiuchumi.
Kuna aina nyingi ya ulafi kwa baba haambiliki yeye ilikuwa power na sio Mali yaani ukionekana unakitaka kile kiti ujue kitakupata Cha mtema kuni mfano kamuulize Kambona.
Nchi kutokuwa na vipaumbele binafsi na kuamini kwenye umajumui wa Afrika hivyo kama Taifa kupoteza rasilimali muhimu ikiwemo fedha, watu na hakuna Cha maana tulichopata.
Unadhani kwa nini alikoswa kupinduliwa kama mara tatu, hii ya mwisho na kina bibi titi, captain maganga na kina Hans pope?
Kifupi nchi ilivurugwa kwa muda wake wote wa miaka 24 aliyokaa madarakani.
Hivyo maraisi wangu bora kiuchumi na kidemokrasia ni;
1.Benjamin William Mkapa
2.Jakaya Mrisho Kikwete
N.B Sasa Kuna wajinga wengi kuliko zamani