blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,278
- 7,966
- Thread starter
-
- #221
Umeshindwa kutumia akili zako zote na nguvu zako kuijua kesho yako?Siijui, kwa sababu Mungu hayupo.
Angekuwepo ningeijua, maana Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, asingenibania nisiijue.
Mimi kutoijua kesho ni ushahidi kwamba Mungu huyo hayupo.
Si ushahidi kwamba Mungu yupo.
Unaamini Mungu hutoa laana?Tusimsingizie Mungu kwa majaribio tunayopitia…..siamini kama kweli mwenyezi Mungu alituletea kina Mwinyi, Mkapa na Kikwete, hili nitapinga mpaka mwisho. Ila naweza kukubali kuwa tuliletewa hao tajwa hapo juu na shetani kutokana na matendo waliyotufanyia kuwa ya kihuni. Nchi za wenzetu hawa wananyongwa, kwa kweli hii katiba LAZIMA ifumuliwe ili hawa marais washikishwe adabu kabla hawajafa na pressure, tunataka kuona wanavyonyongwa.
Mi naona yote ni mipango ya Mungu, we unaonaje?Vpi kuhusu watoto wanaouawa vitani ,wanaobakwa na kulawitiwa ?Mungu hana mpango nao?Wale wanaokufa kwa kukosa chakula? Watoto kwenye cancer?wakina Maria na consolata?Mungu hana na hakua na mpango wa kuwaokoa?
Kwanini hawawezi?Hawawezi.
Wasipoweza hilo linathibitisha Mungu yupo?
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kwa sababu Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote wa kuwawezesha hayupo.Kwanini hawawezi?
Mungu wako anapanga watoto wabakwe vitani?Mi naona yote ni mipango ya Mungu, we unaonaje?
Wewe unaijua kesho yako? Unaijua hata leo na jana yako?Umeshindwa kutumia akili zako zote na nguvu zako kuijua kesho yako?
Mkuu ipyax unaelewa nini kuhusu "wokovu"? Nani kakuambia kuwa hao watoto wanaokufa hawataokolewa? Au wewe unafikiri kupona magonjwa na kuendelea kuishi hapa duniani kwa maisha marefu ndiyo wokovu?? Kula na kushiba ndiyo wokovu??Vpi kuhusu watoto wanaouawa vitani ,wanaobakwa na kulawitiwa ?Mungu hana mpango nao?Wale wanaokufa kwa kukosa chakula? Watoto kwenye cancer?wakina Maria na consolata?Mungu hana na hakua na mpango wa kuwaokoa?
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo na si hadithi tu?Mkuu ipyax unaelewa nini kuhusu "wokovu"? Nani kakuambia kuwa hao watoto wanaokufa hawataokolewa? Au wewe unafikiri kupona magonjwa na kuendelea kuishi hapa duniani kwa maisha marefu ndiyo wokovu?? Kula na kushiba ndiyo wokovu??
Iko hivi; BWANA MUNGU anampango na hao watoto wote uliowataja na wote wataokolewa siku ikifika watafufuliwa na kupewa maisha mengine mapya kabisa, ambapo wataishi milele kwa raha mustarehe hapa hapa duniani. Fahamu kwamba sasa hivi MUNGU anaandaa kuuleta Ufalme wake hapa duniani, na siku aliyoipanga ikifika, basi MESSIAH atakuja tena duniani na kuitawala dunia yote na kuibadilisha kabisa, na dunia yote itakuwa paradiso!
Unamlaumu MUNGU kwa sababu hujui mpango wake aliouandaa kwa ajili ya binadamu wote. Na hii inatokana na watu kama wewe kutokusoma BIBLIA ambayo imeandika kila kitu atakachokifanya BWANA MUNGU kwa watu wake. Watu kama ninyi mnafikiri maisha ni haya haya na hakuna maisha mengine ndiyo maana mnakuwa wepesi kumlaumu MUNGU pale mnapoona maisha hayaendi vizuri.
Kaa ufahamu kwamba hapa duniani ni sehemu ya kupita tu, ni sehemu ya maandilizi kwa ajili ya maisha ya baadaye ya milele, lakini ili ufanikiwe kwenye hayo maisha ya milele ni lazima kwanza umtii MUNGU na kuzishika Amri zake na maagizo yake yote. Uwe maskini uwe tajiri, uwe kilema uwe mzima, uwe umeungana kama Maria na Consolata au uwe vyovyote uwavyo, jukumu lako ni KUTII na kutekeleza yote yale yaliyoagizwa na MUNGU. Ukifa, utapumzika kaburini kwako kwa muda, na siku ikifika, utafufuliwa na kulipwa kwa kadiri ya matendo yako.
Kama ulikuwa tajiri utahukumiwa kwa kadiri ya matendo yako, kama ulikuwa maskini pia utahukumiwa kwa kadiri ya matendo yako, kama ulikuwa kilema pia utahukumiwa kwa kadiri ya matendo yako, kama ulikuwa mzima kabisa pia utahukumiwa kwa kadiri ya matendo yako. Kama ulikuwa kipofu ama kiziwi ama bubu, kila mmoja atahukumiwa kwa kadiri ya matendo yake. Watoto wadogo hawatahukumiwa sababu watoto hawajui mema wala mabaya, na MUNGU ni mwenye haki na hukumu zake ni za haki.
Acha kabisa kumlaumu MUNGU, anza kubadilisha maisha yako na matendo yako, muda huu uliopewa wa kuishi hapa duniani ni wa kupita tu, maisha yawe mazuri au mabaya kwako, wewe tenda mema kwani baada ya maisha haya umeandaliwa neema ama zawadi ya uzima wa milele. Kama una akili utakuwa umenielewa ndugu yangu ipyax
Tamaa zako mwenyewe ndiyo zinakufanya uibe. Maamuzi yako mwenyewe ndiyo yanakufanya uibe.Sasa ni nani kani fanya niibe?
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna tamaa mbaya na tamaa zote ni nzuri tu?Tamaa zako mwenyewe ndiyo zinakufanya uibe. Maamuzi yako mwenyewe ndiyo yanakufanya uibe.
Unafanya kile unachoamua kufanya wewe mwenyewe, hakuna anayekulazimisha kufanya chochote kile, kila kitu ni hiari yako mwenyewe.
Mimi nikijitazama kwenye kioo, nikitoka nje na kuwatazama binadamu wenzangu, wanyama wafugwao na wale wa porini, ndege wa angani, wadudu warukao na watambaao, samaki wa baharini, ziwani, na mitoni, nyota za angani, jua na mwezi, mimea ya kila namna, milima, mabonde, tambarale, mito, maziwa na bahari; vyote hivyo na vile vyote ambavyo sijavitaja ni uthibitisho tosha kuwa yupo mmoja mwenye nguvu, maarifa na uwezo usiopimika aliyefanya yote haya kwa mkono wake, na huyo siyo mwingine bali ni BWANA MUNGU.Unaweza kuthibitisha Mungu yupo na si hadithi tu?
Hujathibitisha. Umelazimisha.Mimi nikijitazama kwenye kioo, nikitoka nje na kuwatazama binadamu wenzangu, wanyama wafugwao na wale wa porini, ndege wa angani, wadudu warukao na watambaao, samaki wa baharini, ziwani, na mitoni, nyota za angani, jua na mwezi, mimea ya kila namna, milima, mabonde, tambarale, mito, maziwa na bahari; vyote hivyo na vile vyote ambavyo sijavitaja ni uthibitisho tosha kuwa yupo mmoja mwenye nguvu, maarifa na uwezo usiopimika aliyefanya yote haya kwa mkono wake, na huyo siyo mwingine bali ni BWANA MUNGU.
Hakuna uthibitisho mwingine kuwa BWANA MUNGU yupo zaidi ya kazi aliyoifanya, kazi ya KUUMBA, UUMBAJI uliotukuka, kazi ya mikono yake inaonekana kwa macho, na Yeye ndiye aliyeyafanya macho, naam hata viungo vyote vya mwili na udongo alioufinyanga akaufanya kuwa nafsi hai, leo hii Kiranga udongo huo uliofinyangwa na kuwa nafsi hai umejaa kiburi hata unatamka hakuna MUNGU!
BWANA MUNGU yupo, alikuwepo na ataendelea kuwepo milele na milele!
Asili ya tamaa ni wapiTamaa zako mwenyewe ndiyo zinakufanya uibe. Maamuzi yako mwenyewe ndiyo yanakufanya uibe.
Unafanya kile unachoamua kufanya wewe mwenyewe, hakuna anayekulazimisha kufanya chochote kile, kila kitu ni hiari yako mwenyewe.
Kwa akili zako wewe hata kama BWANA MUNGU atajitokeza na kusimama mbele yako na kukuambia "mimi ni MUNGU", bado utamwambia athibitishe. Na hata kama atathibitisha kuwa kweli yeye ni MUNGU, bado wewe kwa akili zako utakataa kuwa yeye siyo MUNGU.Hujathibitisha. Umelazimisha.
Kama vitu complex vinahitaji muumba, unaelewa hilo linathibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo na halithibitishi Mungu yupo?
Hujathibitisha. Unahubiri kwa povu.Kwa akili zako wewe hata kama BWANA MUNGU atajitokeza na kusimama mbele yako na kukuambia "mimi ni MUNGU", bado utamwambia athibitishe. Na hata kama atathibitisha kuwa kweli yeye ni MUNGU, bado wewe kwa akili zako utakataa kuwa yeye siyo MUNGU.
Wewe ni kama chumvi iliyoharibika ambayo haifai kutumiwa kwenye chakula wala kutupwa jalalani. Chumvi ikiharibika hata itiwe nini haiwezi kuwa na manufaa tena. Chumvi iliyoharibika hutupwa chini na kukanyagwa na watu!
Laana ya watumishi inakunyemelea...Tubu mapemaHujathibitisha. Unahubiri kwa povu.
Thibitisha Mungu yupo.