Je, inawezekana kila kitu ni mpango wa Mungu?

Jambo la imani halihitaji uthibitisho, linahitaji kuamini.

Sitaki imani, ukiamua kufuata imani, utajuaje imani yako ni sahihi au si sahihi bila uchunguzi? Na ukifanya uchunguzi kuhakiki imani yako kama ni ya kweli au la, bado upo kwenye imani au unatoka kwenye imani na kwenda kwenye uthibitisho?
 
Acha kukariri "maandiko" usiyoelewa maana yake. Unaelewa maana ya neno "kuuawa"?
Umeshindwa nini kuweka ufafanuzi wewe unayejua maana? Wewe umesema kuwa kutokana na mzazi kuwa na dhambi hivyo anazaa mtoto mwenye laana ndio maana anapata magonjwa. Mungu ni mwenye haki atampaje mtoto magonjwa kutokana na dhambi ambazo mtoto ajazitenda?
 


Mungu mwenye haki atawatesaje watoto wasio na hatia kwasababu tu ya dhambi za wazazi wao?
 
Mkuu uzi hahusiani nahao ulio wataja jikite kwenye maada, usimlazimishe kila mtu asome ulicho soma, nivyema zaidi ungetupia hapa tuchambue pumba na mchele.
 
Mkuu uzi hahusiani nahao ulio wataja jikite kwenye maada, usimlazimishe kila mtu asome ulicho soma, nivyema zaidi ungetupia hapa tuchambue pumba na mchele.
Unajuaje uzi hausiani na hao niliowataja kabla hujawasoma?
 
Mkuu ikiwa kila kitu ni mpango wa Mungu? inawezekana kamfanya huyu jamaa kuwa na moyo mgum! Je ikiwa Mungu atamchoma atakuwa kamtendea haki?
 
Unapokosea wewe ni kufanya imani kuwa kama utabiri,kwa sababu kwenye utabiri hauwezi kutabiri jambo ambalo limeshapita ila kwenye imani unaweza kuamini jambo ambalo limeshapita na hauwezi kupata ukweli juu ya jambo hilo.

Na uthibitisho haufanyi jambo kuwepo au kutokuwepo,mie kama nimefanya kosa lakini ukakosekana uthibitisho wa kuonesha kuwa kweli nimefanya kosa hali hiyo haiondoi uhalisia wa kwamba nimefanya kosa,sasa kuamini si jambo lenye kuhitaji matokeo ya kile unachokiamini kama ilivyo kwenye kutabiri.

Wewe mwenyewe unasema imani haihitaji uthibitisho,kwahiyo hata tukitaka kujadili imani ipi sahihi na ipi sio sahihi lazima tukumbuke kuwa imani haihitaji uthibitisho.

Kwahiyo kutaka kujua usahihi wa imani hakufanyi utoke nje ya hiyo imani,maana kama ni hivyo kungekuwa hakuna haja ya kuamini bali tungefanya tu uchunguzi moja kwa moja ili kupata majibu yasio ya imani.
 
Mwenyezi MUNGU ni Mwenye nguvu na mwenye hekima na ni mjuzi na muweza juu ya kila kitu
 
Mkuu ikiwa kila kitu ni mpango wa Mungu? inawezekana kamfanya huyu jamaa kuwa na moyo mgum! Je ikiwa Mungu atamchoma atakuwa kamtendea haki?
Mungu atakuwa hajamtendea haki kama akimchoma. Maana umeshasema kuwa Mungu ndiye aliyemfanya huyu jamaa kuwa na moyo mgumu. Kwahiyo sio mapenzi yake huyu jamaa kuwa na moyo mgumu bali ni Mungu.
 
Mungu atakuwa hajamtendea haki kama akimchoma. Maana umeshasema kuwa Mungu ndiye aliyemfanya huyu jamaa kuwa na moyo mgumu. Kwahiyo sio mapenzi yake huyu jamaa kuwa na moyo mgumu bali ni Mungu.
Pengine Mungu ili azionyeshe gadhabu zake mtu kama huyu lazma awepo. Ni kama kwa Farao, 2 Utanena hayo yote nikuagizayo; na ndugu yako Haruni atanena na Farao, ili awape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.
3 Nami nitaufanya mgumu moyo wa Farao, nami nitazifanya kuwa nyingi ishara zangu na ajabu zangu katika nchi ya Misri.
4 Lakini Farao hatawasikiza ninyi, nami nitaweka mkono wangu juu ya Misri,
 
Imani haihitaji uthibitisho, imani sahihi inahitaji uthibitisho.

Unaelewa tofauti?
 
i alwayz wonder , ikiwa mungu alinileta duniani halafu anataka nirudi tena huko heaven, sasa alinileta huku ili iweje, c angetuacha tuu huko peponi, mh something is wrong somewhere
 
Maelezo yako hapo ni kwamba imani haihitaji uthibitisho,ila ukitaka kujua imani yako kama ni sahihi kwa kufanya uchunguzi basi utakuwa umetoka kwenye hiyo imani na kwenda kwenye uthibitisho.

Hivyo hauwezi tena kuja kusema et imani sahihi inahitaji uthibitisho,maana ukishapata uthibitisho hakuna tena imani hapo.

Unajichanganya mwenyewe.
 

Hujui set theory, hujui subset ni nini.

Kwa mantiki yako nikikwambia kwamba Dodoma ni mkoa, Bunge liko katika Mkoa wa Dodoma.

Mkoa wa Dodoma upo nchini Tanzania.

Nikikwambia Bunge hilo lililopo mkoani Dodoma lipo nchini Tanzania, utabisha.

Utasema Bunge lipo mkoani Dodoma, halipo Tanzania!
 
Kosoa katika kile nilichokieleza au fafanua unapoona sikupaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…