Je, inawezekana kila kitu ni mpango wa Mungu?

Sawa mkuu nimekwelewa vizuri sana, swali kabla sijatenda dhambi Mungu anajua nitatenda dhambi?
Kwanza kabisa. Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo?

Maana kama hayupo, msingi mzima wa swali unakuwa umevunjika.
 
Mleta mada usipende kumuhusisha Mungu kwa mambo mengine tunayojitafutia sie wenyewe binadamu kwa upumbavu wetu.....nikupe mfano. Unafikiri sie kutawaliwa na kina Mwinyi, Mkapa, na Kikwete ilikuwa ni kusudio la Mungu kwetu? Kwanini Mungu atuletee marais wapuuzi na wasio na huruma nasi, je Mungu alitaka sie tuteseke kihivi? Mungu alitupa maarifa ya kuchagua zuri na baya sie kwa makusudi tukawachagua wapuuzi na wakatumia lugha ya baba yao kiongozi shetani kwa kutudanganya wananchi wao kuwa nchi yetu ni ya kimasikini LAZIMA tukaze buti kukubali shida huku wakituibia, nasi kwa ujinga wetu tukawaamini. Kwa sasa tumepata kiongozi maridadi na anayetupenda kwa kutuhamsha ili tuwe na mawazo chanya bado kuna wasaliti wanampinga na kuunga mkono ujinga tuliofanyiwa na viongozi waliopita. Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba hata raia wa kawaida anaona shida kuwa na maendeleo na kuanza kuwalilia kina Mkapa, Kikwete eti warudi kututesa tena, si ujinga huu. Hivi nani aliyeturoga?
 
Unaruhusiwa kuamini unavyotaka.

Ila. Ukileta jambo JF kujadiliana, lishatokanka kwenye imani.

Wenye kutaka facts wataukiza kwa msingibwa fact.

Imani hata mavi yako unaruhusiwa juyaabudu kama Mungu.

Lakini ukija JF na kutuambia "mavi yangu ni Mungu, kuleni mpate sakramenti ya Mungu". Watu watakuuliza kwa misingibkadhaa. Kiimani, ki fact etc.

Kusema Mungubwako yupo ni sawa na kutaka kutulisha mavi. Kama unataka kulabmwenyewe sawa. Ukishatuletea habari hapa kutaka kutulisha mavi yako kwamba ni sakramenti ya Mungu, ni lazima kujihoji.

Mpaka sasa huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.
 
Binadamu kumchambua Mungu ni sawa na chungu kumuuliza mfinyazi kwa nn unanifinyanga hivi..
Kila kitu kipo wazi soma maandiko haya:

Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;(Yohana10:14)

Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.(Tito 1:15)

Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.
Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu.
Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.
Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, Wala usione ni taabu kurudiwa naye.
Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi (Mithali 3:1-12)
 
Kifonikitu kibaya au kizuri kwako? Akija mtu akwambie akuue sasa hivi, utafurahi au uta[pinga habari hiyo?
Mtazamo wangu juu ya kifo kama naona ni kitu kizuri au kibaya unahusu nini tena hapa?
 
Mungu atampimaje mtu wakati yeye Mungu ni muweza wa kujua kitakachotokea mbele. Au sifa ya kujua ya sasa na ya badae Mungu hana? Kama anayo basi atapimaje mtu wakati jibu analijua?
 
Mimi nina visa viwili tu naomba unieleze kwamba kama si Mungu nini.
1.Kisa cha Tundu Lisu kupigwa risasi idadi ile then asifiwe utasema Mungu hajahusika kumuepusha na kifo?!
2. Kuna Bwana mmoja sitomataja lakini yupo hadi sasa alitekwa yaan alikua ndani ya basi walipofika sehemu flani basi likasimamishwa porini wakaamuru abiria wote kushuka,theni wakapanda wote isipokua huyo bwana,basi likaja gari lenye vioo vyeusi akasafirishwa huku anatajiwa makosa yake na kwamba mwisho wake umefika. Alivyofikishwa mahali flani akashushwa porini akakabidhiwa kwa jamaa,theni gari likageuza yule aliyekuwa amepangiwa kumumaliza jamaa kumbe wamesoma naye UDSM akasikitika sana akamwambia mshikaji kweli Una Mungu yaani ni wewe ndo umeletwa nikumalizie..ndo akawa amepona.
Kwa visa hivi eti hakuna mkono wa Mungu?
 
Mtazamo hauwezi kuwa katika kweli ukaendana na uthibitisho?
Ukishasema mtazamo utabaki kuwa ni mtazamo tu na uthibitisho ni kitu kingine,yawezekana huo mtazamo ndio ukawa ukweli wenyewe au sivyo.
 
Mungu yupo sababu kakuumba wewe na wewe huwezi kujiumba, na umeumbwa uwe mbishi, Mungu huumba atakavyo.
 
Sawa mkuu nimekwelewa vizuri sana, swali kabla sijatenda dhambi Mungu anajua nitatenda dhambi?
Jibu nindiyo, BWANA MUNGU anajua kama utatenda dhambi kabla hata hujaitenda. Mfano mzuri BWANA MUNGU alijua kama Kaini anataka kumuua ndugu yake na ndiyo maana alimwambia hivi; "dhambi iko inakuotea mlangoni nayo inakutamani wewe, lakini yakupasa uishinde".

Kama Kaini angemsikiliza BWANA MUNGU na akaamua kuishinda dhambi, basi asingemuua Abeli.
 
Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo na si hadithi tu?
 
Kwa nini Bwana Mungu na si Bibi Mungu?

Huoni Bwana Mungu ni mfumodume wa watu tu wamejipangia?
 
Mungu atampimaje mtu wakati yeye Mungu ni muweza wa kujua kitakachotokea mbele. Au sifa ya kujua ya sasa na ya badae Mungu hana? Kama anayo basi atapimaje mtu wakati jibu analijua?
Hakuna mtu atakayeweza kukupa jibu la kueleweka la swali hilo.

Kwa sababu huyo Mungu hayupo.

Nishawahi kuuliza hilo swali watu wakalipiga danadana tu.
 
Mkuu unajuaje kiongozi wasasa ni maridadi? Unaweza kujua miaka kumi ijayo huyu wasasa atazalisha kitu gani?
 
Mungu angekuwepo si tu Tundu Lissu angekuwa hajapigwa risasi, bali pia dunia nzima kungekuwa hakuna risasi, bundukibwala silaha.

Na wala kifo kisingekuwepo.

Nakushangaa unasema Mungu yupo kwa sababu Tundu Lissu hajauawa na risasi, wakativmamilioni ya watu wanauawa kwa risasi kila mwaka.

Na huyo Tundu Lissu, simuombei, lakinibkama mimi na wewe, kuna siku atafariki.

Kuwepo kwa silaha, bunduki, risasi na watu kupigwa risasi kunaonesha Mungu hayupo.

Hakuoneshi Mungu yupo.

Mungu angekuwepo tungekuwa hatujui bunduki ni nini, risasi ni nini na hata wazo la kumfanyia mwenzako vibaya lisingeweza kufikirika.

Mungu unayemsema yupo alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu hawafikirii kufanyiana ubaya?
 
Upo sahihi kabisa, mimi nacho taka kujua je, kilakitu ni mpango wa Mungu?
 
Unazidi kuongea pumba tu,sijui ukileta imani Jf.. ndio nini sasa?!!!

Kama nina uhuru wa kuamini sasa tatizo liko wapi kuja kujadili imani yangu hapa JF?

Au kuna aliyekulazimisha kuamini kile anachoamini? wewe ukiona mtu anasema kuna Mungu(imani) unaweza kuacha kujadili maana hauamini,sio kukataza watu wasijadili imani.

Suala la Mungu ni imani na wewe kitendo cha kujadili hapa unajadili imani,hauwezi kulitoa hili jambo kwenye imani kisa wewe unajadili au linajadiliwa JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…