Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Sawa.Nilichomaanisha ni kwamba kama unachokiamini ni jambo la kweli basi itabaki kuwa hivyo na si kwamba uthibitisho ndio unafanya imani yako iwe kweli na ukikosekana uthibitisho hufanya imani yako kuwa si ya kweli hata kama ni ya kweli.
Ndiyo maana nikasema kwamba uthibitisho umekuja kudhihirisha tu kwamba alichokiamini Einstein lilikuwa ni jambo la kweli,na kama imani ya Einstein ingekuwa si ya kweli basi pia uthibitisho ungedhihirisha hilo.
Kumbuka tunazungumzia imani,hivyo hauwezi kusema imani fulani si ya kweli kisa hakuna uthibitisho maana tumeona hata Einstein hakuthibitisha imani yake hadi pale baadaye ilipokuja kuthibitika.
Ila unaweza kujua imani isiyo sahihi kama hiyo ya kuamini wewe ni Bill gate.
1.Unaweza kuamini jambola uongo kuwa kweli.
2. Unaweza kuamini jambo la kweli kuwa kweli
3. Unaweza kuamini jambo la kweli kuwa uongo
4. Unaweza kuamini jambo la uongo kuwa uongo.
1. Hata ukikosa uthibitisho, kukosa uthibitisho hakufanyi jambo la kweli kuwa la uongo
2. Hata ukikosa uthibitisho, kukosa uthibitisho hakufanyi jambo la uongo kuwa kweli
Sasa kamaunataka kujua unaloaminini kweli au uongo utafanyaje?
1. Bila uthibitisho huwezi kujua lolote kwa hakika, hata kama unachoamini ni kweli, bila uthibitisho hutajua hilo, utaamini tu.
2. Ukikosa uthibitisho, hilo halithibitishi kwamba unachoamini ni kweli au si kweli, inawezekana si kweli ndiyo maana hujapata uthibitisho, inawezekana ni kweli, ila wewe umeshindwa kupata uthibitisho tu.
Sasa,utajuaje kwamba umekosa uthibitishokwa sababu unachotaka kuthibitisha si kweli na hivyohakina uthibitisho, au nikweli na umekosa uthibitisho tu? Bila uthibitisho huwezi kujua tofauti ya haya mawili.
Na hapo ndipoumuhimu w authibitisho unapokuja.
Uthibitisho una umuhimu gani?
Uthibitisho una umuhimu wa kutunyambulishia hususan pale ambapo hatujui kwamba tumekosa uthibitisho kwa sababu uthibitisho haupo na imani ytu ni potofu au kwa sababu upo na tumeshindwa kuupata tu.
Ndiyo maana nakutakaunipe uthibitisho.
Ukishindwa kuthibitisha,hata wewe mwenyewe unabaki huna hakikakama umeshindwa kuthibitisha kwa sababu unaamini uongona hakuna uthibitisho, au umeshindwakuthibitisha kwa sababu ya mapungufu yako tu na uthibitisho upo.
Thibitisha, usilazimishe.
Thibitisha Mungu yupo.