Je, inawezekana Waziri pale Uingereza kusafiri na timu ya mpira kama Man UTD au Man City au ni hapa kwetu tu?

Je, inawezekana Waziri pale Uingereza kusafiri na timu ya mpira kama Man UTD au Man City au ni hapa kwetu tu?

Imenishangaza sana kuona waziri mzima wa michezo badala ya kuwa bize kushughulikia sera ili ziinue michezo kuhakikisha taifa letu linag'ara kimichezo badala yake anazurula na ndege hadi Algeria.

Nadhani tuna tatizo kubwa sana linalopelekea tuwe na safari ndefu la kuinua michezo kama watungaji na wasimamizi wa sera ndio Hawa!!!
Tena ana Phd
 
Mpira/Michezo ni sehemu ya Ujasusi. Ndio maana wengine wanagharamia pakubwa usivyoweza kuona malipo yake.

Shida hawa wetu hujiendea tu kushangaashangaa.
 
Kwa mawazo kama haya nadhani alhaj mwinyi hakukosea kwamba Tanzania kwenye soka ni kichwa cha mwendawazimu waziri hawezi kuimarisha michezo kwa kuzurura na team kwa kisingizio kwamba anawaongezea hamasa waziri anatakiwa apambane kukarabati sera ili zilete tija. Sio kurukia rukia tu kwenye mafanikio ya watu
Una haki upi kwamba waziri haimarishi sera na kuzisimamia?. Asingeandamana na timu bado mngeongea mkisema waziri anafanya kazi gani wakati team inakwenda mpaka Algeria bila ya kuwa na kiongozi wa msafara mwenye cheo serikalini.

Nongwa ni tatizo letu.
 
Hamasa ya ushindi kaka, tatizo usimba unakusumbua sana ukichanganywa na wivu.
Ni inchi gani imeshatoa pesa kama hamasa kwa timu binasfi ?

Tupunguze mihemko.

Tunaona kote duniani serikali zinatoa zawadi au ahadi kwa timu za taifa,
Na sio timu binafsii...

Nauliza tu kwamba wakati timu moja ndogo hapa inchini ilishindwa kushiriki Mashindano ya CAF mwaka juzi sababu ya kukosa nauli ya kwenda nje ya inchi,

Serikali ilikuwa wp?
 
Una haki upi kwamba waziri haimarishi sera na kuzisimamia?. Asingeandamana na timu bado mngeongea mkisema waziri anafanya kazi gani wakati team inakwenda mpaka Algeria bila ya kuwa na kiongozi wa msafara mwenye cheo serikalini.

Nongwa ni tatizo letu.
Ni wapi duniani ushasikia hayo?
Ndege nzima imejaa watu wa comedy na watu wasioeleweka,

Wanasaidia nn kwa mfano.
 
Ni inchi gani imeshatoa pesa kama hamasa kwa timu binasfi ?

Tupunguze mihemko.

Tunaona kote duniani serikali zinatoa zawadi au ahadi kwa timu za taifa,
Na sio timu binafsii...

Nauliza tu kwamba wakati timu moja ndogo hapa inchini ilishindwa kushiriki Mashindano ya CAF mwaka juzi sababu ya kukosa nauli ya kwenda nje ya inchi,

Serikali ilikuwa wp?
Rais ni mwanasiasa ukumbuke hilo, anapoweka ukaribu na vilabu kama Yanga anakuwa akiweka ukaribu na mamilioni ya wapiga kura, haya matendo ni akiba za kisiasa.
 
Imenishangaza sana kuona waziri mzima wa michezo badala ya kuwa bize kushughulikia sera ili ziinue michezo kuhakikisha taifa letu linag'ara kimichezo badala yake anazurula na ndege hadi Algeria.

Nadhani tuna tatizo kubwa sana linalopelekea tuwe na safari ndefu la kuinua michezo kama watungaji na wasimamizi wa sera ndio Hawa!!!
Waziri ni jinsia gani !!
 
Hakuna kosa. Rais Macron alikuwepo wakati Ufaransa anacheza fainali kombe la Dunia.
 
Viongozi wetu sio wajinga, wanajua sana kucheza na akili zetu.
Asilimia kubwa ya Watanzania akili zipo kwenye ushabiki wa Simba na Yanga tu, mradi kuna kucha tu.
Kwenye English Premier Legue umeshaona kuna mgeni rasmi /mwanasiasa anakuja uwanjani?
Kwenye fainali tu za FA ndio anakuja mgeni rasmi kutoka Royal family (sio mwana siasa)
 
UMEMYONA MAMA WAKATI WA KuTOA ZAWADI.

PUNGUZA KASIRIKO HATA CAF WALITAMBUA UWEPO Wake
 
Hakuna kosa. Rais Macron alikuwepo wakati Ufaransa anacheza fainali kombe la Dunia.
Usitoe mfano wa timu za taifa kwa sababu timu za taifa huwakilisha taifa lakini hizi club ni biashara binafsi. Wewe unajua tuna timu nyingi tu hushiriki Mashindano ya kimataifa mbona hatjawahi ona waziri kaenda
 
Una haki upi kwamba waziri haimarishi sera na kuzisimamia?. Asingeandamana na timu bado mngeongea mkisema waziri anafanya kazi gani wakati team inakwenda mpaka Algeria bila ya kuwa na kiongozi wa msafara mwenye cheo serikalini.

Nongwa ni tatizo letu.
Hakuwa na sababu yoyote ya kupiga hela za walipa kodi kwenda safari ambayo hata asingeenda bado yanga ingecheza vizuri tu naona tu wako pale kujijenga kisiasa.
 
Mbona hawakumsindikiza Mandonga kule Kenya?
Au mpango ndo umeanza?
Kabisa Hawa wasahaulifu sana Tanzania tuna michezo mingi na timu nyingi zikienda kuomba support serikalini utasikia serikali inasema sisi kazi yetu ni kutunga na kusimamia sera sasa hili la yanga mbona nguvu nyingi sana waache kiki za kijinga
 
Posho ndugu yangu, hapo anarudi na posho zake saafi kabisa huku amesafisha macho kwenda nchi za watu [emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom