Unaamini yesu ni mungu pia unaamini ni mwana wa mungu je hapo kutakuwa na miungu wangapi tukimjumuisha na roho mtakatifu?
Yesu ana majina mengi tu ,wewe unashangaa kuitwa mwana wa Mungu ,unashangaa pia kuitwa Mungu
Hata Wayahudi walishangaa ,akawapiga swali ambalo hakuna aliyejibu
Na Mimi nitakupiga hilo swali ukilijibu NASILIMU
Mathayo 22:41-45 (SUV)
41 Basi, Mafarisayo walipokuwa wamekusanyika, Yesu aliwauliza,
42 akasema, "Mwaonaje katika habari za Kristo? Yeye ni mwana wa nani?" Wakamwambia, "Wa Daudi."
43 Akawaambia, "Imekuwaje basi Daudi, katika Roho, kumwita Bwana, akisema,
44 'Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume, Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako'?"
45 "Basi, ikiwa Daudi anamwita Bwana, amekuwaje mwanawe?"
Yesu alinukuu Zaburi 110:1, ambapo Daudi alisema:
"Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume, Hata niwafanye adui zako kuwa chini ya miguu yako."
Yesu alitumia aya hii kuwaonyesha Mafarisayo kwamba Masihi (Kristo) si tu Mwana wa Daudi kwa nasaba, bali pia ni wa hali ya juu zaidi, akiwa Bwana. Hii ilionyesha asili yake ya Kiungu, jambo ambalo lilikuwa gumu kwa Mafarisayo kulielewa.