Je, ipo siku Taifa la Tanganyika litafufuka? Je, itakuwaje? Je, Zanzibar itakuwepo ama?

Tanganyika ipo ila imevalishwa koti la Tanzania, tena wengine wanaiita ' Tanzania bara'.
JokaKuu Nguruvi3 Kalamu Pascal Mayalla Chige zitto junior mtu chake
Upo sahihi kabisa, kwa sababu Tanganyika haipo kisiasa tu lakini maeneo mengine yote, bado Tanganyika ipo, ni suala la muda tu!!

Yaani haina tofauti na zama za USSR... haidhuru hata kama watu walikuwa wanaiita Soviet lakini jina Russia HALIKUFA, and it's a matter of time, kama ilivyotokea back 1991, hatimae Russia kurejea kuwa Russia na sio Soviet tena!!

Na uniona iliyokuwa imezaa USSR wala haina tofauti sana na hii yetu... HOFU dhidi ya two world blocks.

Kwa mfano, ingawaje vitabu vyetu vya shule vinatuambia ni Nyerere ndie aliasisi muungano, declassified CIA Files zinaonesha muungano ulikuwa engineered na CIA baada ya kuzihofia harakati za Umma Party ambazo zilionesha dalili ya kutokea "Another Cuba in East Africa"!

Kwahiyo njia pekee ambayo CIA waliona inaweza kuzuia kuibuka kwa a new Cuba in EA ni kumtumia Mwalimu apeleke wazo la muungano kwa Karume!

Na kwavile hata Karume mwenyewe alizihofia sana harakati za Umma Party, akaona namna pekee ya yeye kuendelea ku-survive ni kweli kuungana na Tanganyika kama njia ya kuivunja miguu Umma Party, kwa sababu, hatimae hata kama Umma Party wangeanzisha choko choko, choko choko hizo zisingekuwa tena dhidi ya Karume na Zanzibar yake bali dhidi ya Nyerere na Tanzania yake!

In fact, hata Nyerere mwenyewe alimuhofia Abdulrahman Babu na Umma Party yake!!

Sasa muungano uliojengwa kwa misingi ya hofu badala ya matakwa ya wananchi, ni muungano ambao mara zote utakuwa unasubiria CHAIN BREAKER.

Na ndo maana, CCM Bara watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha inaendelea kuongoza Zanzibar manake, especially the old CUF, ile kuingia tu madarakani kule ZNZ ingekuwa ndo mwanzo wa safari ya kuelekea kuelekea mwisho wa Tanzania!!

Hata kama watu wangeanza na proposals za serikali 3 huku ZNZ wakipewa kile wanachoita mamlaka kamili, bado ingekuwa ni suala la muda tu kabla ya kugundua hata hayo mamlaka kamili yameshindwa kuwaondoa kutoka kwenye kivuli cha Tanzania-Bara, na namna pekee ya kuondokana na hicho kivuli, ni kugawana fito!!!
 
Kwa sasa nchi ilipofika, we cant go back again.
Wacha tuendelee na mfumo huu huu wa muungano...
 
Dola la Tanzania lilishaundwa Aprili 26. 1964, na waasisi wetu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Karume. Kuthubutu kuvunja Muungano ni uhaini. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania si suala la sera ya chama chochote. Jadilini mengine.
 
Tanzania ni moja kama kuna haki, usawa kwa wote, vivyo hivyo Dunia.
Mipaka na kujitambulisha kimakundi fulani kunasabishwa na ubinafsi wa kuwanyonya wengine (ulioasisiwa na watawala/wanasiasa).
Madai ya uwepo wa Tanganyika na Zanzibar kwa sasa ni matokeo ya kukosekana kwa uwazi, haki na usawa katika Tanzania.
 

Sasa kwanini nyinyi ndio munaoing'ang'ania Zanzibar?
 
Muungano usivunjwe tuwe na serikali moja tu..kwanini ccm wanalazimisha serikali 2.?

#MaendeleoHayanaChama
Hili ndio jibu sahihi.
Sijui kwa nini watu hupenda mizungukoooo bila ya sababu.

Ni kitu gani kinachozuia kuwepo kwa serikali moja katika nchi moja?

Lengo tokea mwanzo wa kuungana lilikuwa ni hilo, la serikali moja baada ya kuondoa hofu zisizokuwa na sababu zilizokuwepo visiwani.

Sasa watu wanazungukazunguka tu na serikali tatu,. Tatu za nini?
 
Hiyo moja itakuwa umezaji wa walio wachache hivyo kupoteza utawala wao wa ndani.
 
Poa ila Muungano wa sasa unaipendelea Zanzibar.
 
Wazungu wanawaza kuungana kila siku huku afrika bara maskini kuna nchi inaitwa Tanzania wapo wananchi wenye mawazo ya utengano, wapo vijana wamechoka kuziwazia fursa zote zilizopo na wameamua kuwazia kujitenga.

Mungu muumba wa kila kitu na atuondolee mawazo haya meusi ndani ya akili zetu.
 
Hiyo moja itakuwa umezaji wa walio wachache hivyo kupoteza utawala wao wa ndani.
Mkuu 'Proved', "utawala wa ndani" wa nini katika nchi moja ya watu wote walio sawa?
Tafadhali, tuache kuzungushana na maneno yasiyo na maana.

Huku kulembalemba, na kuwaachia waarabu mwanya wa kuweka nyufa ndani ya muungano ndiyo sababu tunayo matatizo haya sasa hivi.
Hawa wenye chokochoko walitakiwa kudhibitiwa kungali mapema kabisa.
 
Ifanyike kura ya maoni kuamua kuhusu kuendelea kuwepo kwa Tanganyika na Zanzibar/Pemba, kwenye muungano wa nchi hizi mbili au la!. Matokeo ya kura hiyo kwa taifa la Tanzania, yata -uimarisha muungano au kupata kibali cha kuzirudisha nchi mbili huru za awali, zitakazo jiunga kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki yenye mfumo wa " Federation" kama zitaamua kufanya hivyo au kubaki kama zilivyokuwa kabla ya kuunganishwa kisanii.
 
CCM Zanzibar wanataka serikali 2 kwa kuwa zinawahakikishia kubaki madarakani bila kubeba gharama za kulinda madaraka hayo. Namaanisha jeshi, polisi na usalama wa taifa.
CCM bara wanaogopa kusema wanataka serikali moja kwa sababu hawataki kuwakera wenzao wa Zanzibar.
Wapinzani Zanzibar wanataka 3 kwa kudhani ndiyo itawapa uwezekano wa kuingia madarakani
 
Kila kikundi kinajaribu kulinda maslahi yake. Si ishara nzuri!! ...Huu ndio wakati muafaka kwa wananchi kupewa mwanya wa kuwaamulia wanaoshindana kwenye kura ya maoni. Huko mbele ya safari kuna uwezekano wa kushuhudia yale yaliyompata Rais, Gotabaya Rajapaksa wa Sri lanka ambapo wananchi wamediriki kwenda Ikulu kufanya pikniki na kufurahia mema ya nchi angalau kwa muda mfupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…