Je, ipo siku Taifa la Tanganyika litafufuka? Je, itakuwaje? Je, Zanzibar itakuwepo ama?

Je, ipo siku Taifa la Tanganyika litafufuka? Je, itakuwaje? Je, Zanzibar itakuwepo ama?

Majasusi waliibebesha Tanganyika minyororo ya kuunganishwa na nchi ya Zanzibar.Mwl.Nyerere na umahiri wake wa kuupenda Umoja wa Waafrika akashawishika kuwa bila kuungana Tanganyika na Zanzibar usalama wake ni mdogo.Hakufahamu kuwa kwa kuunganisha mataifa haya maskini kuna gharama kubwa.

Tunashuhudia jinsi Tanganyika inavyonyongwa na minyororo ya Muungano na kutusababishia kero zisizoisha.
Sisi wananchi wa Tanzania ya Tanganyika na Zanzibar tunataka kuandika Katiba Mpya itakayotuwezesha kuijenga Tanganyika imara na Zanzibar huru ili tuungane kwa Haki.
Muungano wa tanganyika na zbar una ajenda nyingi..nyingine muulize lukuvi na yule padri aliyeropoka uchaguzi 2005
 
"kila mtu abaki kwao akubaliane na faida na hasara za kuvunjika muungano"
lakini pia akubaliane na maisha baada ya Muungano.

Kila mtu atalinda mipaka yake, na kila mtu atalipia cha mwenzie atakachotumia, Wazanzibar wanatumia umeme kutoka bara ambao sasa watachagua waulipie au wawe na umeme wao, Wazanzibar wanafanya biashara bara sasa watachagua waje watafute vibali vya kuishi na kufanya biashara bara. Hizo ndio athari za kuvunjika muungano kwao na wakishindwa kulinda mipaka yao shauri yao, sisi tutalinda mipaka yetu.

Yaani hao siku muungano umevunjika, kesho yake wataungana na nchi moja kiarabu fasta na hiyo nchi inajulikana...kule ujombani
 
Tanganyika ilikuwa nchi bandia sijui kwa nini mnataka ifufuke. Hata ikifufuka itasambaratika kikabila kwa sababu ni nchi ya bandia. Zanzibar pekee ndiyo taifa lenye historia, na utamaduni wa muda mrefu.
 
Zanzibar haina uwezo wa kuendesha wizara zilizoko kwenye muungano.

Mf ili Zbar iwe na jeshi lake, itahitaji ndege angalau 5 za kivita. Hii ni zaidi ya bil 500. Itahitaji meli angalau mbili za kivita, hii ni zaidi ya bil 200.

Itahitaji rada za kijeshi, hii ni zaidi ya bil 50.

Hadi hapo tu, Zbar itahitaji zaidi ya trilioni 1, kujenga jeshi lake. Kwa uchumi wa Zbar, watahitaji miaka 100 kujenga jeshi lake lenye uwezo angalau wa kukabiliana na wanamgambo kama Alshababu.

Kimsingi, nje ya muungano Zbar is a failed state
Mkuu, kaangalie kwanza kinachoendelea Sri lanka urudi ku comment tena...
Huu uoga ndo unatukwamisha kama nchi..
Znz ina ukubwa wa 2,461 square km, tunadai haijiwezi Kwa kuwa ni ndogo, lakini kuna nchi nyingi ndogo zaidi zinajisimamia zenyewe!
Mfano, nchi ya Malta ukubwa wake ni 316 square km, na ni nchi huru, and so is Bahrain yenye 760 square km!

Hiyo Sri Lanka unayosema, tatizo lake halitokani na udogo wa eneo, ina ukubwa wa 65,610 square km. Mbona Singapore yenye square km 728 tu ina uchumi imara kuliko nchi nyingi kubwa?
 
Tanganyika ilikuwa nchi bandia sijui kwa nini mnataka ifufuke. Hata ikifufuka itasambaratika kikabila kwa sababu ni nchi ya bandia. Zanzibar pekee ndiyo taifa lenye historia, na utamaduni wa muda mrefu.
Tanganyika ina tofauti gani na mataifa kama Zambia, Malawi, Uganda, Kenya, nk ambayo yapo na hayajasambaratika?!
 
Wazungu wanawaza kuungana kila siku huku afrika bara maskini kuna nchi inaitwa Tanzania wapo wananchi wenye mawazo ya utengano, wapo vijana wamechoka kuziwazia fursa zote zilizopo na wameamua kuwazia kujitenga.

Mungu muumba wa kila kitu na atuondolee mawazo haya meusi ndani ya akili zetu.
Wazungu gani wanawaza kuungana kila siku ?
 
Wazungu wanawaza kuungana kila siku huku afrika bara maskini kuna nchi inaitwa Tanzania wapo wananchi wenye mawazo ya utengano, wapo vijana wamechoka kuziwazia fursa zote zilizopo na wameamua kuwazia kujitenga.

Mungu muumba wa kila kitu na atuondolee mawazo haya meusi ndani ya akili zetu.
Nchi huru kuungana na kufanya mambo yao kwa umoja kama vile EAC, ECOWAS, SADC, EU, nk ni jambo jema na hakuna anayepinga..
Tatizo ni nchi moja kugeuka koloni la nchi nyingine🙄
 
Wazungu wanawaza kuungana kila siku huku afrika bara maskini kuna nchi inaitwa Tanzania wapo wananchi wenye mawazo ya utengano, wapo vijana wamechoka kuziwazia fursa zote zilizopo na wameamua kuwazia kujitenga.

Mungu muumba wa kila kitu na atuondolee mawazo haya meusi ndani ya akili zetu.
Hakuna mtu aliyekataa kuungana..kuungana kunafaa sana tena sana..ila hili la serikali mbili..moja ikiwa kupe wa kutaka apewe kila kitu yeye hatoi hata kidogo ni upuuzi uliopitiliza.

Yafaa sasa twende kwenye serikali moja tu mana ndio lilikua lengo la huu muungano tangu awali.

Kwangu mimi tujishindwa kuwa na serikali 1 basi tatu..ikisindikaka hilo bora kila mtu achukue fito zake akae na mavi yake kwao.

Kuliko huu upuuzi wa sasa wa serikali 2.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ifanyike kura ya maoni kuamua kuhusu kuendelea kuwepo kwa Tanganyika na Zanzibar/Pemba, kwenye muungano wa nchi hizi mbili au la!. Matokeo ya kura hiyo kwa taifa la Tanzania, yata -uimarisha muungano au kupata kibali cha kuzirudisha nchi mbili huru za awali, zitakazo jiunga kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki yenye mfumo wa " Federation" kama zitaamua kufanya hivyo au kubaki kama zilivyokuwa kabla ya kuunganishwa kisanii.
Ccm wataiba kura kulazimisha watu wakubaliane na muungano huu wa kinyonyaji usio na usawa hata kidogo.

Mbaya zaidi watalazimisha serikali 2 kama ile katiba pendekezwa ambayo wanaipigia upatu.

Ccm wamelewa madaraka mbaya zaidi uchubwa madaraka ndio ugonjwa wao mkuu.

Serikali 1 au 3 tofauti na hapo Tanganyika irudi zenji wabaki visiwani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Zanzibar haina uwezo wa kuendesha wizara zilizoko kwenye muungano.

Mf ili Zbar iwe na jeshi lake, itahitaji ndege angalau 5 za kivita. Hii ni zaidi ya bil 500. Itahitaji meli angalau mbili za kivita, hii ni zaidi ya bil 200.

Itahitaji rada za kijeshi, hii ni zaidi ya bil 50.

Hadi hapo tu, Zbar itahitaji zaidi ya trilioni 1, kujenga jeshi lake. Kwa uchumi wa Zbar, watahitaji miaka 100 kujenga jeshi lake lenye uwezo angalau wa kukabiliana na wanamgambo kama Alshababu.

Kimsingi, nje ya muungano Zbar is a failed state.

Hawa wazee wanaokaribia kurudi kwa Maulana wasithubutu kuharibu future ya watoto wao na wajukuu wao kwa kuvunja muungano!
Hi I unafahamu Zanzibar wanapata zaidi ya bajeti yao toka bara
 
Tanganyika ilikuwa nchi bandia sijui kwa nini mnataka ifufuke. Hata ikifufuka itasambaratika kikabila kwa sababu ni nchi ya bandia. Zanzibar pekee ndiyo taifa lenye historia, na utamaduni wa muda mrefu.
Tanganyika kama ilivyokuwa Zanzibar na Pemba, haikuwahi kuwa bandia kamwe!. Ilikuwa nchi huru iliyotambulika kimataifa hivyo na kuwa na kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa, kama ilivyokuwa Zanzibar baada ya uhuru. Hoja hapa ni kuwa haikudumu muda mrefu baada ya kupata uhuru. Ilitambulika kama Tanganyika wakati wa ukoloni na miaka na kudumu kwa miaka minne kabla ya kuunganishwa na Zanzibar/Pemba kwa maslahi ya kisiasa. Kubali au kataa, wanasiasa wanapotosha sana ukweli ili kuendelea kupata vyeo. Nikiwa mtoto mdogo miaka ya sitini, nimeishuhudia nchi hii ikiwa kama Tanganyika hadi ilivyo sasa kama Tanzania.
 
Zanzibar haina uwezo wa kuendesha wizara zilizoko kwenye muungano.

Mf ili Zbar iwe na jeshi lake, itahitaji ndege angalau 5 za kivita. Hii ni zaidi ya bil 500. Itahitaji meli angalau mbili za kivita, hii ni zaidi ya bil 200.

Itahitaji rada za kijeshi, hii ni zaidi ya bil 50.

Hadi hapo tu, Zbar itahitaji zaidi ya trilioni 1, kujenga jeshi lake. Kwa uchumi wa Zbar, watahitaji miaka 100 kujenga jeshi lake lenye uwezo angalau wa kukabiliana na wanamgambo kama Alshababu.

Kimsingi, nje ya muungano Zbar is a failed state.

Hawa wazee wanaokaribia kurudi kwa Maulana wasithubutu kuharibu future ya watoto wao na wajukuu wao kwa kuvunja muungano!
Hiyo ni hela ya mboga kwa Oman. Usichukulie Zanzibar poa namna hiyo, nyuma yake kuna mataifa makubwa tajiri ya kiarabu. Zanzibar ikiachiwa huru tuu, soon inakuwa extended arm ya Oman na kujenga jeshi imara ni sekunde tu.
 
Tanganyika kama ilivyokuwa Zanzibar na Pemba, haikuwahi kuwa bandia kamwe!. Ilikuwa nchi huru iliyotambulika kimataifa hivyo na kuwa na kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa, kama ilivyokuwa Zanzibar baada ya uhuru. Hoja hapa ni kuwa haikudumu muda mrefu baada ya kupata uhuru. Ilitambulika kama Tanganyika wakati wa ukoloni na miaka na kudumu kwa miaka minne kabla ya kuunganishwa na Zanzibar/Pemba kwa maslahi ya kisiasa. Kubali au kataa, wanasiasa wanapotosha sana ukweli ili kuendelea kupata vyeo. Nikiwa mtoto mdogo miaka ya sitini, nimeishuhudia nchi hii ikiwa kama Tanganyika hadi ilivyo sasa kama Tanzania.

Kama siyo nchi bandia kwa nini Watanganyika hawakupiga kelele Nyerere alivyoiua na kuleta Tanzania? Walikaa kimya kwa sababu ni nchi bandia iliyoletwa na mkoloni. Tofautisha na Zanzibar ambayo Wazanzibari hata ukiwakuta London au Sweden au Canada wanajitambua kama Wazanzibari. Mie safari zangu zote duniani sijawahi kukutana na Mtanganyika.
 
Serikali moja imeshashindikana, hakuna siku Zanzibar itakubali kumezwa kabisa na Tanganyika.
Hili ndio jibu sahihi.
Sijui kwa nini watu hupenda mizungukoooo bila ya sababu.

Ni kitu gani kinachozuia kuwepo kwa serikali moja katika nchi moja?

Lengo tokea mwanzo wa kuungana lilikuwa ni hilo, la serikali moja baada ya kuondoa hofu zisizokuwa na sababu zilizokuwepo visiwani.

Sasa watu wanazungukazunguka tu na serikali tatu,. Tatu za nini?
 
Taifa la watu wa Tanganyika. Taifa alilopewa baba wa Taifa hili hayati Mwl Julius Nyerere. Ilakutokana na vita baridi moja ya mashirika ya kijasusi yakaipa taarifa tanganyika kile siku za mbele kitatokea na kwa nn kile kisiwa lazima kiwe kama Taifa moja. Well nisiandike zaidi yahiki nimepata kukisikia.

Ila mission hii bado ni mbichi japo maana kuwepo kwa Znz nikufufuka kwa Tanganyika nakufa kwa znz nikuwepo kwa Taifa moja Tanzania.

End
Pendekeza njia Bora za kufanikisha znz inakufa bila mtikisiko Ili kupata Tz moja.
 
Kama siyo nchi bandia kwa nini Watanganyika hawakupiga kelele Nyerere alivyoiua na kuleta Tanzania? Walikaa kimya kwa sababu ni nchi bandia iliyoletwa na mkoloni. Tofautisha na Zanzibar ambayo Wazanzibari hata ukiwakuta London au Sweden au Canada wanajitambua kama Wazanzibari. Mie safari zangu zote duniani sijawahi kukutana na Mtanganyika.
Maamuzi yanayofanywa na wanasiasa ni nadra sana kuyahoji hasa ukiwa mwananchi usiyekuwa na nafasi yoyote kwenye siasa. Hivyo hivyo haikuwa rahisi wakati huo kuhoji maamuzi ya Nyerere na Karume kufikia uamuzi wa kuunganisha nchi mbili zilizokuwa zimepata uhuru wake muda mfupi. Tanganyika ilikuwa mali ya watanganyika wakati Zanzibar na Pemba zilikuwa mali ya Sultan wa Oman, Muungano ulioundwa baada ya uhuru ulikuwa na hila ndani yake ikiwa ni kumuondoa mwarabu katika umiliki wa visiwa na kuunda muungano wenye kuzingatia uafrika zaidi, kwa kumpora mwarabu haki yake kwenye visiwa vile. Umeuliza, kwa nini watanganyika hawaidai nchi yao? .... Jibu ni kwamba muda ulikuwa haujafika na kwa kuwa ni mchakato wa kisiasa, huenda hivi tunavyozungumza utashika kasi kwa kutegemea siasa na wanasiasa wa sasa wanavyonyumbulika.
 
Back
Top Bottom