Hapana, kulikuwa na tawala za kimakabila ambazo msingi wake ulijengwa kutokana na ukoo uliosimikwa toka enzi za mababu na mabibi ndizo zilizotoa viongozi kwa kuzingatia vigezo walivyojiwekea. Viongozi hawa walioulikana kama machifu,watemi, mangi, mwami, wafalme na malkia walitawanyika katika eneo lote la Tanganyika na mifano ipo.
Huko Iringa kwa wahehe, kulikwa na chifu Mkwawa na ukichimba sana utakuta kuwa wahehe walikuwa na eneo lao la utawala. Wanyamwezi walikuwa na chifu wao wa unyanyembe Milambo, waha walikuwa na mwami wao,akina Mtare, Ruhinda, Ruhaga, Ruyangwa nk. Huko Moshi kulikuwa na Mangi, akina Shangali, .... Tanga akina Kimweri, Kusini kule akina Mputa.
Hawa wote walikuwepo hata kabla ya wakoloni kuingia Afrika na wakati huo utaratibu wa Utaifa na maeneo yake kutengwa kama nchi ulikuwa bado haujaingia.