Bepari2020
JF-Expert Member
- Nov 7, 2020
- 2,072
- 2,453
Maamuzi yanayofanywa na wanasiasa ni nadra sana kuyahoji hasa ukiwa mwananchi usiyekuwa na nafasi yoyote kwenye siasa. Hivyo hivyo haikuwa rahisi wakati huo kuhoji maamuzi ya Nyerere na Karume kufikia uamuzi wa kuunganisha nchi mbili zilizokuwa zimepata uhuru wake muda mfupi. Tanganyika ilikuwa mali ya watanganyika wakati Zanzibar na Pemba zilikuwa mali ya Sultan wa Oman, Muungano ulioundwa baada ya uhuru ulikuwa na hila ndani yake ikiwa ni kumuondoa mwarabu katika umiliki wa visiwa na kuunda muungano wenye kuzingatia uafrika zaidi, kwa kumpora mwarabu haki yake kwenye visiwa vile. Umeuliza, kwa nini watanganyika hawaidai nchi yao? .... Jibu ni kwamba muda ulikuwa haujafika na kwa kuwa ni mchakato wa kisiasa, huenda hivi tunavyozungumza utashika kasi kwa kutegemea siasa na wanasiasa wa sasa wanavyonyumbulika.
Tanganyika ikirudi utaliunganishaje kama taifa? Nyerere aliyeweza kuyaunganisha makabila ya Tanganyika ameshakufa. Tena enzi zile makabila yalikuwa madogo, leo makabila yana mamilioni ya watu. Tanganyika lazima isambaratike. Zanzibar pekee ndiyo taifa la kihistoria litabaki.