Je, ipo siku Taifa la Tanganyika litafufuka? Je, itakuwaje? Je, Zanzibar itakuwepo ama?

Muungano wa tanganyika na zbar una ajenda nyingi..nyingine muulize lukuvi na yule padri aliyeropoka uchaguzi 2005
 

Yaani hao siku muungano umevunjika, kesho yake wataungana na nchi moja kiarabu fasta na hiyo nchi inajulikana...kule ujombani
 
Tanganyika ilikuwa nchi bandia sijui kwa nini mnataka ifufuke. Hata ikifufuka itasambaratika kikabila kwa sababu ni nchi ya bandia. Zanzibar pekee ndiyo taifa lenye historia, na utamaduni wa muda mrefu.
 
Mkuu, kaangalie kwanza kinachoendelea Sri lanka urudi ku comment tena...
Huu uoga ndo unatukwamisha kama nchi..
Znz ina ukubwa wa 2,461 square km, tunadai haijiwezi Kwa kuwa ni ndogo, lakini kuna nchi nyingi ndogo zaidi zinajisimamia zenyewe!
Mfano, nchi ya Malta ukubwa wake ni 316 square km, na ni nchi huru, and so is Bahrain yenye 760 square km!

Hiyo Sri Lanka unayosema, tatizo lake halitokani na udogo wa eneo, ina ukubwa wa 65,610 square km. Mbona Singapore yenye square km 728 tu ina uchumi imara kuliko nchi nyingi kubwa?
 
Tanganyika ilikuwa nchi bandia sijui kwa nini mnataka ifufuke. Hata ikifufuka itasambaratika kikabila kwa sababu ni nchi ya bandia. Zanzibar pekee ndiyo taifa lenye historia, na utamaduni wa muda mrefu.
Tanganyika ina tofauti gani na mataifa kama Zambia, Malawi, Uganda, Kenya, nk ambayo yapo na hayajasambaratika?!
 
Wazungu gani wanawaza kuungana kila siku ?
 
Nchi huru kuungana na kufanya mambo yao kwa umoja kama vile EAC, ECOWAS, SADC, EU, nk ni jambo jema na hakuna anayepinga..
Tatizo ni nchi moja kugeuka koloni la nchi nyingine🙄
 
Hakuna mtu aliyekataa kuungana..kuungana kunafaa sana tena sana..ila hili la serikali mbili..moja ikiwa kupe wa kutaka apewe kila kitu yeye hatoi hata kidogo ni upuuzi uliopitiliza.

Yafaa sasa twende kwenye serikali moja tu mana ndio lilikua lengo la huu muungano tangu awali.

Kwangu mimi tujishindwa kuwa na serikali 1 basi tatu..ikisindikaka hilo bora kila mtu achukue fito zake akae na mavi yake kwao.


Kuliko huu upuuzi wa sasa wa serikali 2.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ccm wataiba kura kulazimisha watu wakubaliane na muungano huu wa kinyonyaji usio na usawa hata kidogo.

Mbaya zaidi watalazimisha serikali 2 kama ile katiba pendekezwa ambayo wanaipigia upatu.

Ccm wamelewa madaraka mbaya zaidi uchubwa madaraka ndio ugonjwa wao mkuu.

Serikali 1 au 3 tofauti na hapo Tanganyika irudi zenji wabaki visiwani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hi I unafahamu Zanzibar wanapata zaidi ya bajeti yao toka bara
 
Tanganyika ilikuwa nchi bandia sijui kwa nini mnataka ifufuke. Hata ikifufuka itasambaratika kikabila kwa sababu ni nchi ya bandia. Zanzibar pekee ndiyo taifa lenye historia, na utamaduni wa muda mrefu.
Tanganyika kama ilivyokuwa Zanzibar na Pemba, haikuwahi kuwa bandia kamwe!. Ilikuwa nchi huru iliyotambulika kimataifa hivyo na kuwa na kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa, kama ilivyokuwa Zanzibar baada ya uhuru. Hoja hapa ni kuwa haikudumu muda mrefu baada ya kupata uhuru. Ilitambulika kama Tanganyika wakati wa ukoloni na miaka na kudumu kwa miaka minne kabla ya kuunganishwa na Zanzibar/Pemba kwa maslahi ya kisiasa. Kubali au kataa, wanasiasa wanapotosha sana ukweli ili kuendelea kupata vyeo. Nikiwa mtoto mdogo miaka ya sitini, nimeishuhudia nchi hii ikiwa kama Tanganyika hadi ilivyo sasa kama Tanzania.
 
Hiyo ni hela ya mboga kwa Oman. Usichukulie Zanzibar poa namna hiyo, nyuma yake kuna mataifa makubwa tajiri ya kiarabu. Zanzibar ikiachiwa huru tuu, soon inakuwa extended arm ya Oman na kujenga jeshi imara ni sekunde tu.
 

Kama siyo nchi bandia kwa nini Watanganyika hawakupiga kelele Nyerere alivyoiua na kuleta Tanzania? Walikaa kimya kwa sababu ni nchi bandia iliyoletwa na mkoloni. Tofautisha na Zanzibar ambayo Wazanzibari hata ukiwakuta London au Sweden au Canada wanajitambua kama Wazanzibari. Mie safari zangu zote duniani sijawahi kukutana na Mtanganyika.
 
Serikali moja imeshashindikana, hakuna siku Zanzibar itakubali kumezwa kabisa na Tanganyika.
 
Pendekeza njia Bora za kufanikisha znz inakufa bila mtikisiko Ili kupata Tz moja.
 
Maamuzi yanayofanywa na wanasiasa ni nadra sana kuyahoji hasa ukiwa mwananchi usiyekuwa na nafasi yoyote kwenye siasa. Hivyo hivyo haikuwa rahisi wakati huo kuhoji maamuzi ya Nyerere na Karume kufikia uamuzi wa kuunganisha nchi mbili zilizokuwa zimepata uhuru wake muda mfupi. Tanganyika ilikuwa mali ya watanganyika wakati Zanzibar na Pemba zilikuwa mali ya Sultan wa Oman, Muungano ulioundwa baada ya uhuru ulikuwa na hila ndani yake ikiwa ni kumuondoa mwarabu katika umiliki wa visiwa na kuunda muungano wenye kuzingatia uafrika zaidi, kwa kumpora mwarabu haki yake kwenye visiwa vile. Umeuliza, kwa nini watanganyika hawaidai nchi yao? .... Jibu ni kwamba muda ulikuwa haujafika na kwa kuwa ni mchakato wa kisiasa, huenda hivi tunavyozungumza utashika kasi kwa kutegemea siasa na wanasiasa wa sasa wanavyonyumbulika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…